Rwanda Wameweza; Tanzania Tumeshindwa Wapi???

Rwanda Wameweza; Tanzania Tumeshindwa Wapi???

AljuniorTz

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2009
Posts
544
Reaction score
18
Nchi ya Rwanda ambao walikuwa ktk vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka kadhaa, lakini sasa wanakuja kwa kasi ya hali ya juu ktk uwanja wa Sayansi na teknolojia.

Sehemu kubwa ya mafanikio yao yametokana na nia na ari ya kuijenga upya nchi yao baada ya vita.
Sehemu kubwa ya wafanyakazi wa Rwanda kuanzia viwandani hadi serikalini ni vijana watupu, ambao baadhi yao wamesomea nchini mwao na sehemu kubwa nje ya nchi, sasa wamerudi kuiendeleza nchi yao.

Mfano mdogo wa ambao umewezeshwa na Wanyarwanda wenyewe ni MRADI wa VITAMBULISHO VYA TAIFA (National ID) ambao umesimamiwa na wao wenyewe kupitia RITA (Rwanda Information Technology Authority
RITA website said:
Rwanda is on a fast track development program aimed at making the economy dynamic ICT based by the year 2020.

A vision plan has been drawn up in collaboration with vastly experienced consultants and advisers. Many projects are due to come online over the next few years, ranging from the establishment of the government owner fiber backbone to putting computers into school classrooms. However, there is one project which is of utmost importance and urgency for the country; that is the introduction of a National ID Card.

Implementation of a National ID, driving license and Smart Card System Project calls for the introduction of an electronic, durable National ID Card which is mandatory for all citizens above the age of 16.

In the first phase of this project the citizens were introduced to a simple but robust and durable bar-coded ID card which contained verified elementary data such as name, address and photograph.

The purpose of this phase was to provide every citizen with a Smartcard based on a national ID. The smart card will include additional information that is useful to various entities in Rwanda such as health, traffic, Social Security fund and other like information.

The National ID Card is going to be used for identification and used as a banking document. The project is championed by the Ministry of Local Government (MINALOC) and will be sponsored by the government of Rwanda.

In the East African community (EAC), Rwanda has been the first country to introduce on electronic ID with Finger Printing System.

Currently the National ID cards are produced and distributed to the 16-year old and above citizens.

Mfano mwengine wa pili ni kwamba wiki hii inayoisha leo; Rwanda kupitia wizara yake ya sayansi, Teknolojia na Utafiti wa kisayansi wamezindua mradi mafuta ya mitambo ya viwandani yatokanayo na matunda kama maparachichi na mimea mingine.

Je serikali yetu ya Tanzania inafanya jitihada gani... (1)... ktk kupiga hatua kuelekea kny maendeleo ya kweli kiviwanda na teknolojia (fiber backbone ipo ktk ardhi yetu sasa, tunaitumiaje)??? (2)... kuhakikisha inaweka mkakati mzuri wa kuwaajiri vijana wasomi wa kitanzania waliopo hapa nchini na wale walio huko unyamwezini??? Kila siku tumeng'ang'ana na wazee tu, vijana wataajiriwa lini walete changamoto mpya ktk kuongoza vita ya maendeleo???

"...Wivu sina eeh ila roho inauma..."; wenzetu walikuwa ktk uwanja wa vita kwa miaka kadhaa (tulijitolea kuwahifadhi wakiwa wakimbizi hapa Tza); wameipata amani ndani ya miaka michache wamepiga hatua kubwa sana ya kimaendeleo. But sisi kila siku tunapiga siasa, maendeleo ya kweli ni mwendo wa kinyonga, je tutafika kweli???

Wadau tunaweza kuchangia na kuelimishana zaidi vipi 2naweza kujikwamua.

Thanx
 
Nchi ya Rwanda ambao walikuwa ktk vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka kadhaa, lakini sasa wanakuja kwa kasi ya hali ya juu ktk uwanja wa Sayansi na teknolojia.

Sehemu kubwa ya mafanikio yao yametokana na nia na ari ya kuijenga upya nchi yao baada ya vita.
Sehemu kubwa ya wafanyakazi wa Rwanda kuanzia viwandani hadi serikalini ni vijana watupu, ambao baadhi yao wamesomea nchini mwao na sehemu kubwa nje ya nchi, sasa wamerudi kuiendeleza nchi yao.

Mfano mdogo wa ambao umewezeshwa na Wanyarwanda wenyewe ni MRADI wa VITAMBULISHO VYA TAIFA (National ID) ambao umesimamiwa na wao wenyewe kupitia RITA (Rwanda Information Technology Authority)

Mfano mwengine wa pili ni kwamba wiki hii inayoisha leo; Rwanda kupitia wizara yake ya sayansi, Teknolojia na Utafiti wa kisayansi wamezindua mradi mafuta ya mitambo ya viwandani yatokanayo na matunda kama maparachichi na mimea mingine.

Wadau tunaweza kuchangia na kuelimishana zaidi vipi 2naweza kujikwamua.

Thanx

We aLJUNIOR,

Achana na sisi bana,

Tuache kulala usingizi tushughulike na SIJUI manininini....sijui Mauvumbuzi?

Acha kwanza tusinzie bana... kwanza mbona nje kuna baridi na ukungu, tunakimbilia wapi!

Kwasasa tunachofanya ni kuzindua ma`mashine au sijui madispensa ya kondom huko mtaani!

Tukimaliza hiyo, tunashughulikia kuunda ma`tume mbalimbali yachunguze jinsi wenzetu wanavyokula pesa.

Halafu mchana wa leo tutajadili kama Zenji ni nchi ama si nchi, saa kumi tunaangalia ufisadi bungeni.

Tukimaliza hayo mambo ,tayari ni wakati wa uchaguzi mpya, 2010 HIYO HAPO,tuko bize na kampeni!

Usituchoshe na mauvumbuzi ya madudu yako hayo ,sijui maparachichi, mapesheni, mambilimbi, utayajua mwenyewe bana.

Ha ha haaa...!! OOhh my motherland Tanzania.

May GOD open your EYES!
 
Last edited:
Kagame instrumentality is a key factor! He does not tolarate curruption, incompetency, ushwahiba, urafiki ktk kazi!

Tz JK na CCM ni opposite!
 
Rwanda wanaweza kwa sababu wananchi wake na viongozi na haswa kiongozi mkuu wanayo attitude ya kuipenda na kuijenga nchi yao. Baada ya RPF kuingia madarakani vijana wengi waliokuwa sehemu mbalimbali duniani walirejea kuijenga nchi yao. Na inaonekana wanayo visheni na hawaendeshi mambo yao kwa staili ya zimamoto.
 
toa CCM madarakani,

Inawezekana kuwaondoa hawa jamaa madarakani ikawa ni njia moja ya kuelekea huko; lakini hao wanaoitwa vyama mbadala wana mkakati gani hasa unaotekelezeka ktk kuhakikisha kwamba tunavuka salama kwenda ktk maendeleo ya kweli???

We aLJUNIOR,

Achana na sisi bana,

Tuache kulala usingizi tushughulike na SIJUI manininini....sijui Mauvumbuzi?

Acha kwanza tusinzie bana... kwanza mbona nje kuna baridi na ukungu, tunakimbilia wapi!

Kwasasa tunachofanya ni kuzindua ma`mashine au sijui madispensa ya kondom huko mtaani!

Tukimaliza hiyo, tunashughulikia kuunda ma`tume mbalimbali yachunguze jinsi wenzetu wanavyokula pesa.

Halafu mchana wa leo tutajadili kama Zenji ni nchi ama si nchi, saa kumi tunaangalia ufisadi bungeni.

Tukimaliza hayo mambo ,tayari ni wakati wa uchaguzi mpya, 2010 HIYO HAPO,tuko bize na kampeni!

Usituchoshe na mauvumbuzi ya madudu yako hayo ,sijui maparachichi, mapesheni, mambilimbi, utayajua mwenyewe bana.

Ha ha haaa...!! OOhh my motherland Tanzania.

May THE GOD open your EYES!

Nimekuelewa jimmy, kama nipo sawa unamaanisha tunashughulishwa na mambo ambayo kwa namna moja au nyengine hayatuletei ubunifu/uvumbuzi mpya ktk kupiga hatua kimaendeleo!!!

Wengineo walio wengi bado wamelala usingizi wa pono!!!
 
"Nabii hatambulikani kwao" Vilevile tujiulize ni kwa nini wasomi na wavumbuzi wa maswala mbalimbali ya sayansi na teknolojia huwa wanakimbilia ughaibuni badala ya kubaki na kuiendeleza Tanzania. Tukiandaa mazingira yatakayowafanya wabaki, watafikiria kubaki nyumbani badala ya kukimbia. Ninaamini wapo wataalamu wengi tu katika fani mbalimbali ambao wangeweza kuiendeleza nchi yetu.
 
Rwanda wanaweza kwa sababu wananchi wake na viongozi na haswa kiongozi mkuu wanayo attitude ya kuipenda na kuijenga nchi yao. Baada ya RPF kuingia madarakani vijana wengi waliokuwa sehemu mbalimbali duniani walirejea kuijenga nchi yao. Na inaonekana wanayo visheni na hawaendeshi mambo yao kwa staili ya zimamoto.
jitihada ya kufanya mambo mazuri wanayo hilo hatukatai na sisi watz tumelala sana aisee hii spidi ya hawa jamaa ni balaa,tatizo kubwa walilonalo hata wafanyeje ubaguzi ndio unawamaliza,hao vijana unaongelea wamerudi kujenga nchi ni watusi lakini wahutu thubutu watarudi wapi?akirudi muhutu anaishia kuwekwa ndani na kuambiwa muuaji,hapo ndipo kagame anapokosea angeijenga nchi vizuri sana kama angeshirikiana na wahutu,hawa jamaa hawana kauli rwanda,wanaona kama nchi yao imeporwa na ndio kitu kinazusha vita miaka yote,sasa pamoja na jitihada hizo wanazofanya kumbuka hawa jamaa ambao ndio wanajiita wenye nchi wakikurupuka tena ni mapanga kwa kwenda mbele na safari hii sijui kama watabakisha mtu katika hii jamii ingine
 
As has been said many times and was repeated by Mrs Clinton recently;

A failure of leadership is what plagues most of Africa and in particularly Tanzania. There is absolutely no excuse for the pathetic state our country is in. We are blessed beyond belief, from natural resources to people.

A lot of countries have done a lot more with a lot less than we have. Rwanda is just another one. If Somalians stopped fighting today it would only be a matter of a few years before they would be better off than us.

As long as these old, incompetent, corrupt fools continue to run our country nothing will change and we will continue to crawl while others run.
 
Good thing rwanda is on our side, alot of rwandese come to study in kenya and alot of kenyans work there. Alot of kenyan companies have also opened shop there. All major construction is being done by kenyans. Karibu rwanda to EAC, tusaidiane.
 
Uongozi Bora,Nidhamu na Uwajibikaji ndio siri kubwa ya Maendeleo ya Wanyarwanda...Kwa Mfumo uliopo sasa ni wazi kuwa Rwanda watakuwa na Maendeleo ya kasi kuliko Nchi yeyote katika Kanda hii ya Afrika Mashariki.....Ni vyema Viongozi wetu wajifunze kutoka kwa serikali ya Kagame!!
 
Kwasasa tunachofanya ni kuzindua ma`mashine au sijui madispensa ya kondom huko mtaani!

Kiongozi gani atazindua matumizi ya hizi mashine?? Ata-inset coin, atabofya whatever instructions, Kondom itatoka... Then what?? ataonyesha matumizi yake?
 
toa CCM madarakani,
Nakuunga mkono asilia mia moja. kwa sababu ndo wamepewa rasilimali zote toka kigoma hadi pemba na toka kilimanjaro hadi mtwara wazisimamie na kuzivuna. Ili kutuongoza na kutuelekeza mbinu za kupata maisha bora. Lakini miaka 45 hakuna. Je si wao wenye matatizo?
 
Kwa vyovyote vile hatuwezi jilinganisha na wanyarwanda hata siku moja, wamekuwa affected na vita, ni wabunifu siyo km sisi.
 
Hatujashindwa, ila bado hatujaamua kufanya kweli.Tumeamua kuwa mafisadi kwanza
 
Msjali,
tumelala usingizi! sema usingizi ukiisha tutaamka tu! Sema tu sijajua kama ni usingizi wa kawaida au ule wa pono!

Kama ni ule wa pono..basi hapo kazi ipo!
 
unajua watanzania tunakosa 'attitude' na kwa kukosa hilo hatujui tunataka nini au tufike wapi! tuanze na nini,(prioritise).tuna watu kibao na wazuri wa mipango lakini viongozi wetu esp tops hawana hiyo elimu ya kuprioritise mambo.wanasikiliza nafsi zao na watu wasiokuwa na vision km kina Kingunge.hapo nchi itaendeleaje? hela za miradi hazitumiki itakavyo.ukiwa mkandarasi wa mradi wa serikali, kila kiongozi analeta bakuli lake anaomba umpe percent kidogo,hivi tutaweza kweli hayo maendeleo?kama president asipouchukia ufisadi kwa vitendo na kukamata key figures hatufiki popote,tusubiri watoke tuchapane makonde ndo tutatia adabu.
 
Good thing rwanda is on our side, alot of rwandese come to study in kenya and alot of kenyans work there. Alot of kenyan companies have also opened shop there. All major construction is being done by kenyans. Karibu rwanda to EAC, tusaidiane.
hawa jamaa wanaboooooa kichizi yani
 
Pamoja na jitihada za kujituma warundi walichota madini mengi sana hapo Kongo wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Wanymlenge walitumika sana. Kagame alikubali kutoa askari wake Kongo baada kujilimbilkizia madini ya kutosha kubadilisha uchumi wa Rwanda.
 
hawa jamaa wanaboooooa kichizi yani

Sawa.. ni ukweli tu wataka sio?? ati mbona Rwanda inaendelea mbele wakati nyie mwa marktime tangia mpewe uhuru?? Here are my reasons.
1. you lack creativity
2. You are so rigid (hate/fear change)
3. Fear competition unlike Rwanda (the EAC issue)
4. Waste alot of time hating and concentrating on your neighbours faults instead of checking your own.
5. You are inherently lazy, mostly due to ujamaa.
6. You education system is by default designed to fail.
7. you have a confidence problem as a country, where you play second feedle to everyone.
8. Paranoia should be your second name, this leads to 'safe' investments, which are not economical.

I can go on forever, I know I will be crucified, but the truth hurts and its about time you learn the truth.
 
Back
Top Bottom