#COVID19 Rwanda yaanza kutoa chanjo ya ziada kwa wazee na wenye maradhi nyemelezi

#COVID19 Rwanda yaanza kutoa chanjo ya ziada kwa wazee na wenye maradhi nyemelezi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wizara ya afya ya Rwanda imetangaza kuwa itaanza kutoa dozi ya tatu kwa wazee na wale ambao wana maradhinyemelezi kuanzia leo Jumanne.

Wizara hiyo inasema utekelezaji huo utafanywa kwa awamu na utaanza katika mji mkuu, Kigali.

Waziri wa nchi wa Rwanda anayehusika na huduma za afya ya msingi anasema dozi ya tatu itatolewa kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 50.

Wale kati ya miaka 30 na 50 watapata tu chanjo ya ziada ikiwa wana maradhi nyemelezi .

Shirika la Afya Ulimwenguni linasema kikundi hiki kinapaswa kupata chanjo ya ziada, kwani wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa baada ya chanjo yao ya kwanza.

Wafanyakazi wa afya pia wanastahiki dozi ya tatu.

Kati ya idadi ya watu wapatao milioni 13, zaidi ya Wanyarwanda milioni tatu wamechanjwa hadi sasa.

BBC Swahili
 
Nchi zinazojali raia wake zinachukua hatua, hawa wengine wapo busy na vijembe
 
Mhhhh!!!, Hizo chanjo jinsi zinavyorundikwa miilini mwetu baadaye zikianza kushindana itakuwa kizaazaa.
 
Back
Top Bottom