Rwanda yaidai UK Euro millioni 50 za mkatapa wa wahamiaji kutoka UK

Rwanda yaidai UK Euro millioni 50 za mkatapa wa wahamiaji kutoka UK

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Mahusiano ya Rwanda na serikali ya Uingeleza, siku za nyuma yalikuwa mazuri.

Mwaka 2022, mwezi wa nne, enzi za waziri mkuu, Rishi Sunak, serikali zote zilisaini mkataba wa mamilioni ya Euro.
Baada ya waziri mkuu wa sasa kuingia madarakani, mkataba huo ulizikwa, na serikali ya UK ikaiomba Rwanda ipotezee, isifatilie deni lililobaki.
Kwa mahusiano yaliyokuwepo, Rwanda ilikubali.

Hivi karibuni, Lord Collins, waziri wa UK anaeshughulikia maswala ya Africa, alitangaza kuwa Rwanda ina mkono katika vifo vya watu 70, waliouliwa na kundi la waasi wa serikali ya Uganda, lijulikanalo kama ADF.

Kauli hii, ilipelekea pia serikali ya Uingeleza kuiwekekea vikwazo Rwanda, kwa kuhusika na mgogoro wa vita vya mashariki mwa Congo.

Mkataba wa nchi hizi mbili, ulikuwa wazi. Na rwanda, haikuacha deni hilo kishelia. Hivyo, imeiomba serikali ya UK kuhakikisha inalipa Milioni 50 Euro baada ya kusitisha mkataba wa kupeleka wahamiaji haramu nchini Rwanda.
 
Dawa ya Deni ni kulipa TU
KAZI ni kipimo cha utu
 
Anachokitafuta PAKA atakipata tu... tatizo la waafrika na baadhi ya waarabu wakiwa karibu na hao wazungu wanajisahau na kudhani kuwa same acts and plans which they make together while in good terms make them look the same, which in reality the white folks always look down on them.. balaa huja baadae anapokuja farao ambaye hamjui Moses... mifano haiishi...Sadam Hussein, Osama Bin Laden, Gaddafi, Mobutu, Savimbi, n.k ... safari hii mpaka kwa wa kwao Zelensky wanampiga spana sembuse PAKA!!!... Bob Marley alisema Time will tell...
 
Huyu jamaa amechanganyikiwa anapimishana misuli na mkoloni mkongwe UK😀😀😀.Sasahivi mabeberu wapo kwenye phase ya kumpa jina baya as a WAR LORD and a DIKITETA wakimaliza hapo phase inayofata............The end!!
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Huyu jamaa amechanganyikiwa anapimishana misuli na mkoloni mkongwe UK😀😀😀.Sasahivi mabeberu wapo kwenye phase ya kumpa jina baya as a WAR LORD and a DIKITETA wakimaliza hapo phase inayofata............The end!!
Kwani kosa lake nini? Makubaliano yanasema nini? Au unahisi ni mkataba wa kikoba! Huyo mkoloni anaongoza kwake, na jama yupo kwake.
 
Hapewivhata senti, mkataba wenyewe wa kibubusa, si ameshapewa ile down payment ambayo hata hakuitolea jasho? Atulie, almasi za congo nazo zimeanza kuchacha, ni muda tu atakuwa sawa na kaka yake Burundi.
 
Back
Top Bottom