MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Mahusiano ya Rwanda na serikali ya Uingeleza, siku za nyuma yalikuwa mazuri.
Mwaka 2022, mwezi wa nne, enzi za waziri mkuu, Rishi Sunak, serikali zote zilisaini mkataba wa mamilioni ya Euro.
Baada ya waziri mkuu wa sasa kuingia madarakani, mkataba huo ulizikwa, na serikali ya UK ikaiomba Rwanda ipotezee, isifatilie deni lililobaki.
Kwa mahusiano yaliyokuwepo, Rwanda ilikubali.
Hivi karibuni, Lord Collins, waziri wa UK anaeshughulikia maswala ya Africa, alitangaza kuwa Rwanda ina mkono katika vifo vya watu 70, waliouliwa na kundi la waasi wa serikali ya Uganda, lijulikanalo kama ADF.
Kauli hii, ilipelekea pia serikali ya Uingeleza kuiwekekea vikwazo Rwanda, kwa kuhusika na mgogoro wa vita vya mashariki mwa Congo.
Mkataba wa nchi hizi mbili, ulikuwa wazi. Na rwanda, haikuacha deni hilo kishelia. Hivyo, imeiomba serikali ya UK kuhakikisha inalipa Milioni 50 Euro baada ya kusitisha mkataba wa kupeleka wahamiaji haramu nchini Rwanda.