Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Habari JF.
Waziri mkuu wa zamani wa Congo Matata Mponyo na kiongozi moja wa kanisa, wamedai kwa nyakati tofauti kuwa Rais Kagame anataka kuipanua Rwanda. Mpango huo wa Kagame ni kushinikiza utawala wa majimbo nchini Congo na baadae kuliingilia jimbo moja kwa kuliomba kupiga kura ya kujitenga na kujiunga na Rwanda.
Jimbo hilo ni maeneo ya Mashariki yakijumuisha Kivu kusini na kaskazini. Eneo hili lina Watusi wengi ambao ni kabila la Kagame na pia kuna raslimali nyingi kama madini, misitu, uvuvi, udongo wenye rutuba, wanyama pori nk.
Viongozi hao wawili pia wamedai vita vya Mashariki ya Congo vinachangiwa na Kagame kufanikisha mpango wake Ovu. Pia wanadai Kagame ametumia vikundi vya uasi ambavyo vimetafuta muafaka kwa kuandikishwa jeshini na vina mpango wa kuasi baadae kwa kudai taifa lao huru la KIVU.
Waziri wa nchi za nje wa Rwanda Leo ameitisha mkutano wa dharura na wanahabari wa kimataifa na wa ndani na kuwashutumu viongozi hao wa Congo kwa uchonganishi. Amesema Rwanda inataka kuona maelewano mazuri baina ya jirani zake wote ikiwepo Congo. Anedai pia maridhiano na Uganda yanaendelea na yamefika pazuri. Amesema Congo ni rafiki mzuri wa Rwanda na angependa uhusiano huo mzuri udumu na usivurugwe kwa kauli hizi tata.
NB: Jamhuri hiyo itaitwa RWAKI kwa maana ya Rwanda na Kivu.