Rwanda yatangaza adhima ya kuwa kituo cha wahamiaji kutoka umoja wa ulaya

Rwanda yatangaza adhima ya kuwa kituo cha wahamiaji kutoka umoja wa ulaya

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuanzisha vituo vya wahamiaji nje ya mipaka yake umeingia hatua mpya huku Rwanda ikitajwa kuwa eneo linalopewa nafasi kubwa ya kuwa mwenyeji wa kituo cha kwanza cha aina hiyo.
Mpango huo ni sehemu ya msimamo mkali zaidi wa baadhi ya serikali za Ulaya kuhusu uhamiaji.

Nchi tano za EU, Denmark, Austria, Ugiriki, Ujerumani na Uholanzi, zimeeleza nia ya kuanzisha kituo hicho kabla ya mwisho wa mwaka, huku kikitarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2027.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, kituo hicho kitaanza kwa majaribio na huenda kikapokea takribani wahamiaji 100. Vyanzo vya kidiplomasia vinasema hakitakuwa kituo cha kizuizini na kwamba baadhi ya wahamiaji wanaweza kupewa fursa ya kubaki na kufanya kazi nchini Rwanda.

Hata hivyo, mashirika ya haki za binadamu na baadhi ya wanasiasa wa Ulaya wanahoji uwezo wa mfumo huo kulinda haki za wahamiaji. Wanakumbusha changamoto zilizokabili mipango kama ile ya Uingereza ya kuwapeleka wahamiaji Rwanda na vituo vya Italia nchini Albania.

Chanzo: Dw swahili
 
Nchi tano za EU, Denmark, Austria, Ugiriki, Ujerumani na Uholanzi, zimeeleza nia ya kuanzisha kituo hicho kabla ya mwisho wa mwaka, huku kikitarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2027.
Madini ya Kongo yamewanogea sasa wanataka wahamie karibu kabisa
 
Kagame bhana akishaua mpinzani wake anatangaza drama ili kuua soo!
 
Back
Top Bottom