Rwanda yatuma majeshi yake mpakani na nchi ya DRC Congo, yasema iko tayari kwa vita!

Walidai alipigwa ambush na M-23 lkn utata ni kuwa eneo alilokuwa lilikuwa ni mbali zaidi na walipo waasi (Km 156)

Maafisa aliowaacha waliouwawa ni 11 kwenye mazingira tata sasa

Muhusika inahisiwa ni vigogo walio ndani ya jeshi
Col. Mamadou Mustafa Ndala, huyu alikuwa kamanda wankikosi cha makomandoo.

Huyu alizaliwa mwaka 1978 mpaka umauti unamkuta alikuwa na miaka 35. Kifo chake kilileta simanzi miongoni mwa wananchi waliokuwa wakisumbuliwa na uvamizi wa makundi kadhaa ya wahuni ikiwamo m23.

Huyu mwamba anakumbukwa sana miongoni mwa raia na wanajeshi wenzake Kwa akili kubwa ya kumsoma adui na kukabiliana naye bila uoga.

Mwaka 2013 wakati Rwanda ikiwaunga mkono m23 , aliekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda wakati huo gen. James Kabarebe aliwahi kuwafananisha FARDC na jeshi dhaifu ambalo haliwezi kuuwa hata panya.

Katika mapigano yaliyoanza mei 2013 maeneo ya Kibumba na Rutshuru Col Ndara akisaidiana na vikosi vya walinda Amani wa MONUSCO aliweza kuwalaza chini askari 721 wa m23 huku akikamata mateka 541 upande wa adui.
Kwa upande wake na walinda amani wa MONUSCO FARDC walipoteza askari 201 na 608 majerui ambapo walinda amani 3 wa MONUSCO pia walipoteza maisha.

Baada ya mission hii kukamilika, rais Kabila alimrudisha col Ndara Kinshasa.

Mwaka 2014 Januari, Ndala alipelekwa Jimbo la kivu kaskazini mji wa Beni Kwa lengo la kuendesha operation ya kuangamizi makundi mengine yaliyokuwa yanatishia usalama wa maeneo hayo na wakazi husika.

Akiwa amewahaidi wananchi wa Beni kuwasambaratisha makundi hayo popote walipo, alfajiri ya tarehe 2 January 2014 wakati akielekea msituni kuwasaka waasi mara ghafla gari lake la kivita lilipigwa roketi na kumwangamiza kamanda Ndala na askari wake kadhaa.

Msafara ulishambuliwa na waasi wa ADF-Nalu wenye mafungamano na Uganda.

Baada ya kifo cha Col Ndala, mapfisa kadhaa wa vyeo vya juu ndaninya FARDC walifunguliwa kesi ya mauaji ya col Ndala Kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi cha Dola za kimarekani 20,000 ambapo waliuza taarifa zilizosababisha mauaji ya col Ndala.

Kifo cha Ndala kilipokelewa Kwa majonzi makubwa miongoni mwa raia. Marehemu aliacha make na watoto 3.
 
Umeeleza vizuri Sana,wakubwa wake ndio walimuua mamadou Ndala.
Hawakumpenda.
Hiyo Nchi haina suluhisho waache wapigane tu huku wakicheza sebene.
Maana ni vitu wanavyopenda.
 
Waźipìge tu. PENGINE itakuwa mwisho wà Kagame na Museveni na Tshisekedi
 
Ndara aka gorilla, uyu alikua muarobaini ya ao mbuzi vile tu tama na ubinafsi wa ngese wa chache waka mkatisha jamaa kiboya sana.
 
Kuielewa Drc ni kazi sana nje ya sababu nyingine ,moja ya sababu maafisa wakuu wa FARDC waliona wivu sana mafanikio ya Col Ndala ndipo wakaona wampunguze
 
Umeeleza vizuri Sana,wakubwa wake ndio walimuua mamadou Ndala.
Hawakumpenda.
Hiyo Nchi haina suluhisho waache wapigane tu huku wakicheza sebene.
Maana ni vitu wanavyopenda.
Ustadi wa Ndala kuongoza mapigano Kwa weledi na ustadi wa hali ya juu vilimjengea Imani na ushawishi miongoni mwa raia na askari wa bataliani ya 42 ambayo ilikuwa ni kikosi cha makomandoo aliyokuwa akiongoza licha ya umri wake mdogo hivyo viongozi wakubwa wakaanza kupata hofu juu ya mustakabali wao wa siku za usoni.

Mara kadhaa Ndala alihusika pande za Kivu kutuliza uasi wa raia dhidi ya majeshi ya MONUSCO ambayo raia walitaka waondoke na kurejea kwao Kwa tuhuma za kushindwa kupambana na waasi.

Wakati diplomasia za serikali ziligoma,raia walimsikiliza na kumwelewa col Ndala na hivyo wakasitishia hasira zao dhidi ya walinda amani hao. Wakati raia wakiandamana mitaani Kwa hasira dhidi ya walinda amani wa MONUSCO,Col Mamadou Ndala alipata habari hizo na msafara wake wakawakaribia waandamanaji wenye hasira, col Ndala alishuka kwenye gari na kuwaendea waandamanaji wenye hasira, walipomwona kuwa ni yeye wakampokea kwa vifijo wakipiga kelele za furaha Mamadou.....Mamadou! Mwamba akawatuliza akawaacha na tabasamu na vicheko.

Mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na kiongozi wa MONUSCO nchini DRC bwana Martin Kobler tayari alishatengeneza mafungamano ya karibu na col Ndala kuliko Maafisa wengine waandamizi kwenye jeshi la Congo kutokana na umahiri, na unyumbulifu wa Ndala killa alipo hitajika kukabili tishio lolote la usalama katika eneo.

Baada ya m23 kufurushwa, Ndala alirudishwa Kinshasa na rais Joseph Kabila. Baada ya mabadiliko hayo wananchi waliandamana waakiishutumu serikali kutaka kumdhoofisha Ndala lakini pia lengo la serikali kutoa fursa Kwa makundi ya kuhuni kunawili mashariki mwa DRC.

Ni ukweli ulio wazi kuwa mauaji ya Col Mamadou Ndala yalitengenezwa na viongozi wake ambao kimsingi wengi wao ni vibaraka wa mataifa ya nje yanayonufaika na mgogoro mashariki mwa DRC.

Wakati wa mazishi yake serikali ilimtunukia cheo cha Brig.Gen kwa kuheshimu mchango wake wa ulinzi wa nchi ya DRC.

Baada ya kifo cha Ndala Congo ilishuhudia maandamano makubwa ya raia na wanasiasa wakipinga mauaji ya Ndala huku hali ya usalama mashariki mwa Congo ikizidi kuwa tete kutokana na kushamiri Kwa harakati za makundi ya waasi na mauaji ya raia wasio na hatia.
 
Kabila alihusika kwa asilimia zote hata sio watu wa Western.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…