S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

Je mwenyewe aliyejenga akiamua kuivunja vp?
Sheria ina mruhusu

Ova
Rejea hapa

"Kufuatia uamuzi huo, mwaka 2004 wanafamilia watano wa mzee Pazi walifungua kesi Mahakama Kuu (Divisheni ya Ardhi) kupinga nyumba yao kuuzwa.

Waliiomba Mahakama itamke kuwa wao ndio wamiliki halali wa kiwanja hicho na nyumba iliyokuwemo.

Waliitaka itamke pia kuwa amri ya wao kukamatwa, nyumba yao kuuzwa, wao kuondolewa na kubomolewa haikuwa halali na ilitokana na udanganyifu mkubwa"

Kimsingi hapo shauri la wanafamilia lilikuwa hilo tu mahakama itamke hivyo,na mahakama imefanya hivyo hiyo inaweka uhalali wa kumiliki ghorofa hilo na S.Amon hawezi kutaka kubomoa atapingana na amri ya mahakama
 
Ila
Kutoka nyumba chakavu ya udongo mpaka kumiliki ghorofa tusikate tamaa wadau,ipo siku tutatoboa tu hata ikiwa uzeeni..ingekuwa mimi hapo muda huohuo nataka nione mikataba ya wapangaji hili nianze kula hela za kodi

View attachment 2203922
Ila itaondoka na wengi,labda watakaokuja kufaidika ni wale ambao hawausiki kabisa
 
Taarifa kutoka Mahakama ya Rufaa inaonyesha kwamba Mbunge wa Mstaafu wa ccm Mh Sauli Henry Amon , ameshindwa kesi Mahakamani baada ya Familia ya Bushiri Pazi kurejeshewa nyumba iliyouzwa kwa mnada mwaka 2001 .

Ilikuwa hivi , Kampuni ya S.H.AMON ilishinda mnada wa nyumba namba 113 , Kitalu 4 , Block 17 ambayo ilikuwa mali ya Bushiri Pazi , iliyokuwa Kariakoo , Ilala , DSM , S.H.AMON alilipa Tsh mil 105 katika mnada uliofanyika 13/5/2001 , hii ilikuwa nyumba ya kawaida tu , baada ya kuinunua Sauli akaibomoa na kuporomosha jengo la ghorofa nane .

Mnada huo ulipingwa Mahakamani na Bushiri Pazi , ambaye alidai haukuwa halali , Baada ya danadana nyingi za kisheria kwenye Mahakama mbalimbali kwa miaka 20 , Hatimaye Ndugu Bushiri Pazi amerejeshewa nyumba yake , ila sasa si ile ya chini tena , ni ghorofa 8 .

FB_IMG_1651155082401.jpg


Chanzo : KYELA FM
 
Back
Top Bottom