SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Nimefuatilia kuhusu mechi ya kesho ya Simba na Yanga, nimesikia mechi inatakiwa kuanza saa 11:00 jioni. Najua hata huko nyuma, kuna mechi kadhaa zilianza muda huo ila naona hili ni kosa la kiufundi.
Mechi ikianza muda huo inamaanisha nusu ya mechi itakuwa wakati wa mwanga wa jua na nusu itakuwa kwenye mwanga wa taa (kama kipindi cha pili kinaanza saa 12:00 kitategemea zaidi taa kuliko jua). Nashangaa hata Azam hawajawahi kulilalamikia hili maana hata katika upigaji picha kutakuwa na usumbufu mdogo wa kubadili 'settings' za camera katikati ya mchezo.
Tuamue, mechi iwe jioni au usiku lakini siyo nusu nusu. Hauwezi kukuta hili linafanyika popote kwingine duniani.