Saalah (Silent Ocean): Anavyotakatisha na kutorosha pesa nchini, Uhujumu Uchumi, Kuteka na Kutesa watu, anavyolindwa na viongozi

Kwamba zaidi ya milioni 100 zinapotea mwenye mali hajui?
Wewe unafikiri 100m inapotea muda gani kwa mtu mwenye kuzungusha stock ya $250,000? Unajua stock count wengine wanafanya muda gani?
Kijana unaemuamini anaweza kuiba kidogokidogo bila kuathiri turnover yako siku unapiga hesabu ndio unakuta stock ya 100m haipo.
 
Hongera
Umefanya uthubutu usiotarajjwa.

Natumaini mpaka sasa TCRA washapewa tenda ya kukusaka legally na illegally. Nikikumbuka kesi ya Jamhuri dhidi ya Maxence Melo aliyeamua kulinda kanuni za JF kutotoa details za whistleblower aliyeisaidia serikali kujua wizi wa mafuta bandarini, badala ya serikali kudeal na taarifa kama ni kweli au la iliamua kumshtaki msamaria aliyetoa taarifa.

Jambo lingine ni wazi mama yetu ambaye kuanzia juzi ameanza kutrend kisiasa, siyo mtu wa kumuamini na hakika hana tofauti na wanasiasa wanaotabasamu wakiwa wamekanyaga migongo ya wavujajasho wanaoonewa na kunyanyaswa kila iitwapo leo.

Tatu, kwa kuwa umedeclare interest kuwa wewe ni askari hapo Central hakikisha una play low as you can wasikugundue kwa sababu kama akina Salaah wanasema wamemuweka mfukoni namba moja wetu basi usidhani wanatania. Wanaua na hawafanywi kitu.

Nne. Laana ya damu za watanzania waliokufa kwa kukosa huduma bora za afya, waliouawa na genge la Silent Ocean na hata wanaolia kudhulumiwa na hao majambazi itawwfikia wahusika wote. Mungu atashughulika nao kwa namna itakayowafaa

Tano. Fahamu kuwa mpaka sasa Eliudi anaweza muda wowote akalambishwa vumbi na huyo subian mwenye roho ya uasi. Mtajua anaishije na anawezaje kutotema bungo la kumwaga siri

Sita. Nina mashaka na ushiriki wa Tanzania hususani hawa matajiri kwenye maeneo yenye migogoro Afrika na duniani. Money laundry mara nyingi inatumika kufadhili uhalifu dhidi ya binadamu
 
Kwahiyo we mkuu ukitishiwa utoe mali zako kesho tu asubuhi unakabidhi ? Kwanini asingeenda Polisi kipindi anatishiwa na ushahidi kabisa?

Hii kesi nayo kakubali iishe kizembe sababu alikua anaweza lipwa bila salaah kuingizwa.

Sababu haiwezekani mtu ulomkabidhi asimamie duka akakubali ameiba 22.5 m na dukani kuna upotevu wa zaidi ya 200+ m na yeye akakubali kesi iishie hapo?

Nasikitika tu kusema huyu Eliud ndo amekosea biashara haihitaji roho nyepesi na kuukubali vitu kirahisi .
 
Nakuhakikishia HAWEZI
 
Kuna mtu mmoja raia wa nje ameniambia kuwa taifa lao wamefuatilia yanayojiri bongo wamethibitisha kuwa nchi inauzwa kwa highest bidder

Wao wanachojali ni akaunti zao kutuna bila ukomo
 
ki mafia zaidi
 
Pius ni mshenzi na mbinafsi and fate has dealt him accordingly. Eliud ni muaminifu ila ni mzembe sana na amestahili kilichomkuta, ajifunze.

Salaah ni mfano wa jinsi matajiri wengi wanavyoishi, wanapenda kumaliza biashara at all cost. Hawa entertain mambo ya pending na viporo kwenye kazi. Ndio maana wengi wao ni wakatili ukiingia kwenye 18 zao.

Jamaa alitaka kumsaidia dogo kwa nia njema kabisa ila mwisho wake ndio huu. Alipewa hadi ushauri wa kuajiri accountant akapuuzia mwishowe kapigwa hela ndefu bila kujijua na kuzirudisha hawezi. Kama hii story ni ya kweli, I can imagine namna huyo Salaah anajutia uamuzi wa kwenda extra mile kwa mtu mpumbavu.

C'est La Vie.
 
Kbsa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mwendazake nilikuwa na mwelewa sana na ndio maana wapuuzi kama hawa alikuwa anadeal nao mwenyewe baada ya kupata ripoti kutoka TISS, muhimili wa mahakama hushaoza toka zamani enzi ya mzee wa Msoga.TISS nao tayari washafungwa mikono awamu hii ila hawa jamaa wanapiga kazi na wanaripoti ya kila kinacho endelea ,sema hawa waarabu wengi wanashare na wanasiasa wetu, haijalishi wa upinzani au wa serikalini na ndio maana vyombo vyetu vya dola hawawezi kudeal nao wanaishia kwa panya road basi,hao wakiwagusa dk sifuri simu ya kiongozi fulani.

Chuma walikuwa wanamzushia sana ila njia aliyo ichaguwa kudeal nao ilikuwa sawasawa,nchi kuna wapuuzi wana mambo ya kis#nges#nge sana bila kuwa katili zidi ya matendo yao ,wataendelea kuiharibu nchi na mama moyo huo hana,kudeal na Mafia inabidi uwe na moyo wa kikatili.

Nape alisema "acheni legacy yake ijitetee" ila kila mda unavyoenda ndivyo Chuma kinajizihirisha ubora wake. Hapo unajiuliza kuna kampuni ngapi zinakwepa kodi kama wafanyavyo Silent na huyo mwaarabu anaye agiza mbolea.Tanzania makusanyo kwa mwezi yalikiwa hazidi 1tr,ila alivyo ingia chuma mpaka aanaondoka zilifikia mpaka 2tr sababu alikuwa hacheki nao hawa wapuuzi.
 
Kwa kweli kama mtu mnyonge anaenda kufungua kesi kisha police wanasema huyu mtu hatuwezi kumfungulia kesi hakika tunahitaji Katiba mpya isiyo bagua huyu ni nani?
Afrika issues sio katiba,issues ni kuisimamia na kuiishi katiba.Kenya wale wamebadilisha katika yao na still bado wanataka kuibadilisha tena ila kuna ufisadi na umafia wa kutisha.

Ndio maana issues si kulisikia neno la Mungu issues ni KULITII na KULIISHI NENO LA MUNGU. Same too katiba issues si kuwa na katiba nzuri issues ni KUITII na KUISHII KATIBA kwa kila mmoja wetu ambapo kwa nchi yetu haiwezekani sababu kuanzia huko mahakamai,bungeni na serikalini rushwa na ufisadi umetamalaki, halafu unategemea hao hao ndio waisimamie katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…