Saalah (Silent Ocean): Anavyotakatisha na kutorosha pesa nchini, Uhujumu Uchumi, Kuteka na Kutesa watu, anavyolindwa na viongozi

Watu gani hao wajinga hivyo na je hio laki 2 ilikuwa kwa siku au mwezi?
 
Hizi tuhuma zote cyprian musiba alishazisema kwa utofauti kipindi cha magufuli na hawakufanywa chochote tatizo lenu watanzania ni wasahaulifu
Silent Ocean imeanza ku-operate tena lini?
Kuna mtu alieleza humu kuwa GSM alitembea kwa magoti ikulu kumuomba mwamba amsamehe, mwamba akamkazia akalipe kodi ya serikali, jamaa kwa kuanza akaifunga silent ocean?

Uliusoma uzi ule? Uli-comment?
 
Mkuu shutma za familia ya GSM zipo tangu utawala wa kikwete na hawakuwahi kufanywa chochote

Kama hutojali unaweza kutujuza katika miaka 6 aliyodumu madarakani Mwamba Jiwe, JPM aliwafanya nini hawa GSM?
Watu wanapenda sana Kutengeneza narrative. Kifupi Gsm amekua kipindi cha Jpm, kipindi cha Kikwete Gsm ilikuwa kampuni ndogo mno, Kaka Yake Gsm ndio alikuwa kipindi cha Mkapa mpaka Kikwete.
 
Wakae chini wafanye mahesabu wamalizane. Kwanini Mwarabu hataki? Au mali iliyotaifishwa thanani yake ni pungufu ukilinganisha na deni? Kwanini Huyo Eliud hajakuja na mahesabu hata kama ni makadirio ya deni na thamani ya mali anazodai ameporwa? Hizi ni details muhimu lazima aweke wazi.
 
inasikitisha vipenyo wanaona wanaruka uzi kama hawauoni.

jk/mama anaiharibu sana nchi!

r.i.p magu.
 

kuna uwezekano wa Eliud na Pius wakawa mchongo mmoja, katika hali ya kawaida haileti picha kuwa badala kuwa na kisasi kwa aliekuibia uwe na kisasi kwa anaekudai wewe.
 
Hamna anything of substance kwenye andiko lako zaidi ya kutumia emotional language na kumtuhumu Mwsrabu kwa mambo ambayo hayahusiani na ishu unayoishadidia. Waafrika ni majizi makauzu na magumashi siku zote. Mtu kapewa mtaji wa zaidi ya dolari laki 2 elfu 50 na mzigo juu tena kwa nia nzuri kabisa, halafu kaboronga kupitia mtu wake mwenyewe. Kwanza utaje kiasi cha deni na thamani ya mali iliyotaifishwa.
 
Wengi humu sio wafanyabiashara na hawajui hata wafanyabiashara wanapitia Changamoto gani. Nchi hii hata uwe mwema vipi as long as unafanya biashara na unaingiza Hela mamlaka lazima zije zitengeneze mazingira ya Upigaji.
 
Ni jambo la kusikitisha pia ni funzo kwetu sote. Salaah na Eliud walifanya biashara ya kuaminiana (dhamana ilikuwa wao wenyewe). Biashara yoyote isiyokuwa na legal bond- collateral (dhamana) inahitaji uaminifu na uwazi wa hali ya juu sana kwani mkishindwana unalipa wewe in person, haina mahakama wala police.
Ukisoma taharifa utangundua kabisa Salaah alikuwa na nia nzuri kabisa ya kibiashara kati yao (wheather legal or illegal). Salaah alikuwa anampa advice Mr. Eliud jinsi ya ku-deal na aina ya biashara wanayofanya (hesabu lazima zikae sawa). Kuwe na reconciliation ya mahesabu kati yao (yakifanywa na wahasibu wao)
Mtu ukiwa ndani ya mfumo wa aina hii ya biashara unatakiwa ujiandae kabisa kuwa migogoro yake umalizwa kibabe, hakuna mahakama wala police.
Eliud anawakilisha jamii kubwa ya wafanyabiashara ivyo wao kwa pamoja wanatakiwa kutumia kisa hiki kama funzo. Ukiaminiwa kwa syle hii basi kuwa very smart, mfanye alikuwaamini kama ni mmoja wa wamiliki wa biashara yako, aelewe kila hatua ufanyao( kuhusiana na biashara) otherwise mambo yatakuwa magumu sana.
 
Unapo deal na matajiri lazima utumie akili kubwa sana. Mimi kuna mmoja 2020 wakati wa corona alitufanyia roho mbaya tukaenda police mpka mahakamani afu jamaa anasema madogo nilitaka kuwakomoa tuu ile case iliisha na najua atakuwa kasahau kabisa lakin sisi kinyongo kipo moyoni hata ichukue miaka elfu ipo siku yake ya kuonja ubaya wetu na uzuri ni kwamba hatajua kamwe ni nani anamtendea huo ubaya now tupo tunajitafuta kwanza tupate hizo hela alizotumia kutufanyia ukatili ndo tutaenda sawa sasa
 
Hivi huwa mnasoma na kuelewa? Dogo hatafuti huruma wala hisani kwa Saalah. Anakubali makosa yake yaliyotokana na elimu yake na kumuamini Pius sana.

Ina maana anachotaka kutoka kwa Salaah ni haki yake sio msaada.

Katika mali na pesa alizochukua Salaah kwa huyo dogo ni zaidi ya kiasi ambacho alikuwa anamdai au kuliko hasara aliyokuwa ameipata.

Na alichukua kimabavu hadi mizigo ya watu wengine iliyokuwa njiani toka China ambayo iliagizwa kupitia kwa Eliud.

Muwe mnasoma na kuelewa. Waalimu wenu itakuwa walipata taabu sana
 
Mkuu kuna watu humu muda mwingine wanatia hasira mno, why hamsomi to understood?haraka ya nini ?hupewi star humu kwa kuwa wa kwanza to comment, tena comment iliyojaa uzuzu, JFimeingiliwa na virus wa dot com
 
Na hili ndio la msingi, mambo yasiwe mengi, arudishiwe kiasi kilichozidi
 
Hujui Bashite alichowafanyia. Akawapora ghorofa. Alafu watu wakawa wanatetea hawa wapuuzi
Bashite alichofanya aliwadanganya kuwa mzee JPM anahitaji hilo ghorofa, na jamaa wakampa Kwa roho moja ila mwisho wa siku wakaja kujua kuwa haikuwa Order ya Mzee

Kwahiyo Kwa lugha nyepesi unaweza kusema kwamba bado waliendelea Kula na utawala JPM kama kawaida, na ndio maana ata Bashite alipowambia issue ya Mzee kuwa anataka kitu fulani haikuwa suprise kwao na akawapiga kirahisi

Bashite alikuwa ni Right-handed man wa Mzee kwahiyo ilikuwa ni ngumu sana kumshtukia pale anapoamua kutumia Jina la Mzee kwenye mishe zake, na mbaya zaidi hao jamaa wanapata jeuri kutoka Msoga kwahiyo hakuna wa kuwagusa
 
Sawa,ila kwa ushauri wako kwa dogo unaona afanyeje au achukue hatua zipi?
Maana kwenye vyombo husika hao wakina salah wamekaba kote!
Ila ukiangalia bado kuna room ya wao wakazungumza wakamalizana
Ila,inajulikana matajiri wa kibongo ni wajehuri, hapo dogo mumshauri am amtafute mjomba sijui kaka mkubwa wa salah azungumze nao,wao watazungumza na mdg wao wanaweza kuyaweka sawa
Unaweza kuja kuona jambo linaisha kiuwepesi na maisha yakaendelea

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…