Mkuu Ruta mie nilishastuka siku nyingi kuhusu zoezi hili la kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu katiba mpya ambayo inatakiwa itumike katika uchaguzi ujao 2015. Niliwahi kuandika kwamba usanii utafanyika na kuandika katiba nyingine ambayo itakuwa kama ya chama kimoja na hivyo kuipa magamba nafasi kubwa ya kubaki madarakani. Naomba tu kama katiba kama hiyo ikiandikwa Watanzania tuikatae kwa sauti moja.
Cha kushangaza tume hiyo ina watu chungu nzima waliowahi kushika nyadhifa mbali mbali nchini lakini hawa wote hawaongei ila ni Warioba tu!!! Sijui huyu Mzee ndiye msemaji wa tume hiyo!? Dalili kusema kweli za kupata katiba ambayo itaungwa mkono na Watanzania wengi zinazidi kufifia lakini kama tuwajuavyo magamba watachakachua matokeo ya kuunga/kutoungwa mkono kwa katiba hiyo mpya na hivyo itapita kwa kishindo na hivyo kuwawezesha magamba kutawala Tanzania milele!!!