Sababu 5 kwamba nyumba yako ipo katika hatari ya kuungua kwa moto wa short ya umeme

Sababu 5 kwamba nyumba yako ipo katika hatari ya kuungua kwa moto wa short ya umeme

Ndg ww ni jembe!! Ahsante sn na ubarikiwe. Kuna mafundi wabishi. Ngoja , kwanza nitamtolea photocopy nae apige msuli.
 
Mkuu umesahau wanaoiba umeme, niliwahi shuhudia short ndani ya ukuta, ulikuwa mzinga wa hatari sana, kumbe jamaa alikuwa amemega ndani kwa ndani, nikamwambia aite tanesco waje wamsaidie, weeeee, alikuwa mkali balaa.
 
Ahsante mkuu kwa uchambuzi wa kina sana,ila nina maswali machache naomba ufafanuzi.

1: Huu mfumo mpya wa kusokota pamoja nyaya zile ziingiazo kwenye mita sio hatari kwa baadae magamba yatakapo chunika kwa jua kali?

2: Ukifunga mita(luku)sita katika waya huo uliosokotwa kwa matumizi ya single phase katika kila mita je!?waya utaweza kuhimili matumizi ya kila mita kwa wakati mmoja?

Natarajia majibu ya kiufafanuzi mtaalamu wangu.
 
Ahsante mkuu kwa uchambuzi wa kina sana,ila nina maswali machache naomba ufafanuzi.

1: Huu mfumo mpya wa kusokota pamoja nyaya zile ziingiazo kwenye mita sio hatari kwa baadae magamba yatakapo chunika kwa jua kali?

2: ukifunga mita(luku)sita katika waya huo uliosokotwa kwa matumizi ya single phase katika kila mita je!?waya utaweza kuhimili matumizi ya kila mita kwa wakati mmoja?

Natarajia majibu ya kiufafanuzi mtaalamu wangu.

1.Usokotaji wa waya hauna tatizo,insulator(gamba la waya) za service line zimetengenezwa maalumu kukabiliana na mazingira ya jua kali na mvua,ni ngumu kwa waya ya service line kubanduka insulator yake kwa sababu tu za kimazingira!

2.Uwezo wa waya mmoja wa service line kuweza kuhudumia mita sita za LUKU kutategemeana na matumizi ya kila mteja mwenye mita husika.

Kama matumizi yao wote kwa jumla hayazidi Kilowatt-Hour rating ya waya husika haina tatizo.

Mfano nyumba ya kuishi inaweza kuwa na vyumba sita,nyumba hii hufungwa waya mmoja wa service line kuingiza umeme katika nyumba hiyo ambao una kidhi mahitaji ya vyumba hivyo sita kama ikitokea vyote vipo in full power.

Hakuna tofauti kama nyumba hiyo hiyo wakaja wapangaji tofauti na kila mmoja akataka kufunga mita yake.Kwa sababu kila chumba kitafungwa mita hivyo utakua na mita sita,hapo hakuna kitakacho badilika katika matumizi kwani waya ule wa service line uliyo fungwa utabaki kuwa na uwezo wa kuhudumia vyumba vyote hivyo sita.

Mita haiongezi wala kupunguza chochote katika matumizi ya umeme cha msingi mpango wa kihuduma wa umeme wa mara ya kwanza katika nyumba hiyo utabaki uleule.

Kinacho angaliwa kuhusu waya wa service line ni Jumla ya Kilowatt-hour ya nyumba husika.kama Kilowatt-hour itabaki ileile uwezo wa waya hauta athirika kwa kuongeza idadi za mita hata zikifungwa kumi,cha msingi matumizi yasizidi kiwango kile ambacho kilitumika kuombea service line hiyo.

Tatizo litaanza kama ikitokea Matumizi yatazidi kiwango cha Kilowatt-hour zaidi ya yale yalio tumika kuomba service line hapa haita jalisha kama mita ni moja au zaidi!
 
Nashukuru kwa majibu yako mazuri ndg trañsistor. Nimeelewa.mungu aendelee kukupa maarifa na ujuzi kwà ajili ya taifa letu.ila nina swali jingiñe mkuu;

kama kila chumba kina matumizi ya pasi, jokofu, jiko, feni, TV, Radio na taa 4 kwa wakati mmoja....

je! huo waya unaweza kuhimili?
 
ahsante sana kwa Elimu hii, naomba kujua kama nimenunua wire 2.5 zile single zenye rangi tatu red, black , njano je zinaweza kutumika kufanya wiring za socket na taa? bila kutumia wire ya 1.5?
 
ahsante sana kwa Elimu hii, naomba kujua kama nimenunua wire 2.5 zile single zenye rangi tatu red, black , njano je zinaweza kutumika kufanya wiring za socket na taa? bila kutumia wire ya 1.5?

Bila shaka mkuu waweza kuzitumia vizuri kabisa.Ila katika socket ya cooker kama utaweka tumia waya kuanzia 4mm na kuendelea.
 
Uko vzr ndugu,,taa 4 na fridge.tv na computer kwa lisaa limoja nitatumia unit ngapi?
 
Uko vzr ndugu,,taa 4 na fridge.tv na computer kwa lisaa limoja nitatumia unit ngapi?

Du mkuu swali lako zuri lakini hivyo vitu vina size zake in term of wattage,nadhani ungenitajia kila kimoja hapo kina watt ngapi ningekupa jibu sahihi!
 
Back
Top Bottom