Sababu 5 kwamba nyumba yako ipo katika hatari ya kuungua kwa moto wa short ya umeme

Du mkuu swali lako zuri lakini hivyo vitu vina size zake in term of wattage,nadhani ungenitajia kila kimoja hapo kina watt ngapi ningekupa jibu sahihi!
mkuu apa naomba pia uitoe ellimu kuhusu jinsi ya kucalculate yan formula
 
Yaani nimeipenda na nimeelewa kupita maelezo, safi sana mtoa somo
 
Nawakumbusha tena
Thanks mkuu ila kuna post no #60 hukuijibu tangu 2015 mpk leo naimani mdau alihtaji jibu lako.

Otherwise nami nimepata kitu ila hii ya kuweka cut out kabla ya LUKU ipoje? Ina maana ziwepo mbili? Baada ya mita na kabla ya mita?

Pia Tanesco wasiponiwekea naweza weka Mwenyewe na fundi wangu?

Nitafrahi kusikia kutoka kwako
 
Asante sana mkuu, umetupatia elimu nzuri sana kuhusu masuala ya umeme, vifaa vyake na matumizi yake pia. Mungu akuongoze uendelee kuwa na moyo huo huo.
 
natoa pongezi nyingi kwako kwa mafundisho uliyoyatoa ubarikiwe sana
 
Nashauri mods, hili tatizo la nyumba kuungua kwa sababu ya short ya umeme limekuwa kubwa sana. Hii elimu aliyoitoa mkuu Transistor ni muhimu iwepo kila wakati watu waipitie ili wailimishe wengine. Ushauri wangu huu uzi uwe STICKY..
hakika!
 

Naona mfumo wa cutout wameondoa siku hizi, hasa katika hizi mita za luku,wanatumia mfumo wa Circuit breaker,japo inatakiwa wafunge vyote.

Huruhusiwi kufanya chochote nyuma ya mita(kabla umeme haujaingia katika mita).

Unaruhusiwa kufunga vilinda circuit vingi uwezavyo ndani ya nyumba yako baada ya umeme kupita kwenye mita.

Chunguza mita yako kama ina circuit breaker,vifaa ambavyo vipo kama switch vimewekwa katika mazingira ambayo ni rahisi kufikia kuwasha na kuzima vifaa hivi hufungwa katika mita,sababu hutumika kuzima umeme nyumba nzima pale inapo tokea tatizo la umeme,mfumo huu ni ulindaji wa mali ya mteja dhidi ya majanga ya umeme ambavyo nilazima vifungwe naTANESCO wenyewe.



Kama mita haina vifaa hivi basi utahitaji kufungiwa CUTOUT au kifaa hicho

Cutout zinafungwa na mafundi wa TANESCO tu,na si fundi wa kawaida.
 

Attachments

  • upload_2018-3-8_12-7-9.png
    66 KB · Views: 331
Kama unahitaji ushauri wowote pia karibu
 
Mkuu hapa nimeelimika sana,tunashukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…