Sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010

Sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010

........Kwa akili za watanzania wengi watamchagua tu Kikwete, tatizo huko vijijini wanajua chama kimoja tu CCM. Hivyo Kikwete akigombea mwakani na bila shaka atagombea kupitia CCM, lazima ashinde tu kwa ushindi mkubwa.
Mie wala sitojihangaisha kupiga kura.

Ni vizuri ukapiga kura kumchagua kiongozi unaemtaka. Wengi wanaodhani atashinda kwa kishindo wasipopiga kura, ni dhahiri kuwa mtu usiemtaka anakuwa na nafasi kubwa ya kushinda endapo wengine watampa kura zao.

Sioni jinsi gani JK atashindwa uchaguzi ujao. Japokuwa nahisi kuwa hatapata kura nyingi sana kama alivyopata katika uchaguzi uliopita (kura zitapungua sana).
 
100% Nina uhakika huyu jamaa tunaweza kumtoa Moi alitolewa watu walikuwa wanamuita MTUKUFU sembuse huyu? natolea mfano wa moi kutolewa ila mambo yaliyotokea baada ya yeye kutolewa tuaachane nayo kwanza, kinachotakiwa huyu jamaa na kabinet yake(his kids) wasirudi tena .

Wishfull thinking!
Wananchi wa Kenya huwezi kuwafananisha na wananchi wa Tanzania. Wakenya hawako tayari kuumia na kuvumilia tofauti na Watanzania ambao ni wavumilivu na wepesi kudanganyika kwa vipande vya fedha na zawadi ndogo ndogo.

Pia, utawala ukiwa mbovu wanaoelewa wajibu wao katika kurekebisha mambo kwa njia ya ballot box ili kuleta mabadiliko yanayohitajika ni wachache ukilinganisha na wengi ambao hawaelewi - wale 70% wafuata upepo! Kwa hali hiyo si rahisi kumtoa JK kama unavyofikiria ama unavyotaka. Inahitajika mass mobilization ya nguvu. Nani wa kufanya kazi hiyo ya mobilization is an issue which is being discussed here at JF daily and there is no tangible consesus!
 
Sioni jinsi gani JK atashindwa uchaguzi ujao. Japokuwa nahisi kuwa hatapata kura nyingi sana kama alivyopata katika uchaguzi uliopita (kura zitapungua sana).
Usishangae ni jinsi gani atashindwa. Hivyo hivyo ambavyo kura zake zitapungua ndivyo anavyoweza kushindwa kwa sababu zinaweza kupunmgua hadi kufikia kiwango cha kutotosha
 
Wishfull thinking!
Wananchi wa Kenya huwezi kuwafananisha na wananchi wa Tanzania. Wakenya hawako tayari kuumia na kuvumilia tofauti na Watanzania ambao ni wavumilivu na wepesi kudanganyika kwa vipande vya fedha na zawadi ndogo ndogo.

Pia, utawala ukiwa mbovu wanaoelewa wajibu wao katika kurekebisha mambo kwa njia ya ballot box ili kuleta mabadiliko yanayohitajika ni wachache ukilinganisha na wengi ambao hawaelewi - wale 70% wafuata upepo! Kwa hali hiyo si rahisi kumtoa JK kama unavyofikiria ama unavyotaka. Inahitajika mass mobilization ya nguvu. Nani wa kufanya kazi hiyo ya mobilization is an issue which is being discussed here at JF daily and there is no tangible consesus!

Huyu tunaweza kumtoa kabisa na wala sio ndoto za alinacha...kumobilaizi watu tunaweza kabisa lakini punda unaweza kumpeleka hadi mtoni tu basi.wakimrudisha Awamu ya lala salama watu watakaolalamika tutatoana macho nao hapa.
 
Kikwete and CCM are devils we know. Opposition we don't know. If opposition wins we don't know what they will do. It's better to stick with the devils we know. So we must bring back Kikwete.
vichwa vingine bwana!!!! sasa ukim-support Manji ndo unakuwa ze comedi original au??!!!
 
ninaposema kumtoa simaanishi kuingia msituni.i mean wananchi wasimpigie kura.kwa watz hakuna mtu ambaye yupo tayari kwenda msituni even me myself hata wewe hapo.kinachotakiwa ni sisi wenyewe kufunguka macho ...la sivyo tusije kulaumiana hapa.awamu ya lala salama itakuwa ya hatari sana huyu jamaa akirudi.

Fanya Kazi ya kufukuza upepo!
 
100% Nina uhakika huyu jamaa tunaweza kumtoa Moi alitolewa watu walikuwa wanamuita MTUKUFU sembuse huyu? natolea mfano wa moi kutolewa ila mambo yaliyotokea baada ya yeye kutolewa tuaachane nayo kwanza, kinachotakiwa huyu jamaa na kabinet yake(his kids) wasirudi tena .

Pengine Moi alitoka kwa vile kulikuwa na watu wa kumtowa , lakini kwa mwendo kama wa CHADEMA nafikiri bado tubakie nae Muungwana.
 
........Kwa akili za watanzania wengi watamchagua tu Kikwete, tatizo huko vijijini wanajua chama kimoja tu CCM. Hivyo Kikwete akigombea mwakani na bila shaka atagombea kupitia CCM, lazima ashinde tu kwa ushindi mkubwa.
Mie wala sitojihangaisha kupiga kura.

Ukweli ni kuwa wanaogopa kuwapa kina Slaa na Lipumba. Hawajafika Ikulu miparaganyiko mitupu. Hebu tupeni mbadala ili tuone hiyo 70% tuifanyie kazi . Si wanafata upepo tu bali tuone upepo wa mbadala ili ufuatwe.
 
Huyu tunaweza kumtoa kabisa na wala sio ndoto za alinacha...kumobilaizi watu tunaweza kabisa lakini punda unaweza kumpeleka hadi mtoni tu basi.wakimrudisha Awamu ya lala salama watu watakaolalamika tutatoana macho nao hapa.

Chonde baba , Punda ni nani? Watanzania? Ama kweli tutapewa kila majina sisimizi, .......!
 
Kikwete and CCM are devils we know. Opposition we don't know. If opposition wins we don't know what they will do. It's better to stick with the devils we know. So we must bring back Kikwete.

Meaning? CCM wana hatimiliki ya kuendesha nchi? Kikwete na viongozi wenzake ni Watanzani kama tulivyo watanzania wengine wote including opposition. Which means, by your so called definition of 'devils' we are all devils as Tanzanians kwa hiyo there is nothing to worry about letting the opposition our fellow 'devils' (Tanzanians) take over from CCM!
 
- Atarudi tu tena kwa kishindo, wananchi wengi bado hatuelewi umuhimu wa kura zetu! Iispokuwa the best thing ni kuendelea kujaribu kuwaamsha hao 70%, cha ajabu ni kwamba wengine wako humu JF.

Respect.

FMEs!
..harudi! wewe si tomaso!subiri utaona.
 
Kwani yeye mwenyewe amesema anataka tena kuendelea na awamu ya pili? Mie nadhani ameshatambua kwamba hana uwezo wa kuongoza nchi, na bila shaka atakaa pembeni ampishe mtu mwingine.
 
Jamani, kuwa na mawazo tofauti ni jambo jema. Je, kama sio yeye ni nani mnampendekeza badala ya muungwana? Na huyo anayependekezwa ana rekodi gani ya utendaji itakayo washawishi wapiga kura kumpigia yeye. Je, katika miezi kumi hii ijayo ana uwezo na rasilimali za kutosha kummuza?. Kama majibu yapo sawa, vinginevyo tuongeze nguvu kwenye wabunge-tupate watu makini ambao wanaweza kusimamia serikali/kuikosoa,kuikemea na kuiondoa. Tunahitaji-strong institutions. Kumbuka hata ukipata mtu mwingine adhaniwaye kuwa ni mtendaji (power corrupts), kama taasisi (watchdog) ni dhaifu, hakuna lolote jipya, maana baada ya miezi 18 madarakani, atalegea tena na hadithi itakuwa ileile!.
 
Tatizo hapa ni kuwa sioni mtu ndani ya CCM anayeweza kumzuia Kikwete asigombee tena, na mtu anayeweza akafanya tofauti na Kikwete ndani ya CCM. Kwa upande wa upinzani pia, ingawa kuna watu ninaaona wanaoonyesha kuwa wanaweza kufanya zaidi ya Kikwete, bado nina wasiwasi na uwezo wao katika utekelezaji kwa vile wanaonekana kushindwa kuongoza kikundi kidogo tu cha chama chao, hivyo itakapofikia wapewe jukumu la kuongoza nchi nzima nina wasiwasi kuwa kunaweza kutokea balaa kubwa zaidi.
 
Tatizo hapa ni kuwa sioni mtu ndani ya CCM anayeweza kumzuia Kikwete asigombee tena, na mtu anayeweza akafanya tofauti na Kikwete ndani ya CCM.

Sawasawa kabisa, wasema kweli - wote ni wale wale.

Kwa upande wa upinzani pia, ingawa kuna watu ninaaona wanaoonyesha kuwa wanaweza kufanya zaidi ya Kikwete,

Ni kweli wenye uwezo wapo tena wengi tu.

bado nina wasiwasi na uwezo wao katika utekelezaji kwa vile wanaonekana kushindwa kuongoza kikundi kidogo tu cha chama chao,

Hapana, kwanza umesema mwenyewe kuwa wanaoonyesha uwezo wapo halafu hapo hapo unasema bado una wasi wasi na uwezo wao, mbona unajichanganya mkuu ? Pili, siyo lazima kiongozi wa juu wa chama ndio agombee - huo ni muono wa kiCCM.

hivyo itakapofikia wapewe jukumu la kuongoza nchi nzima nina wasiwasi kuwa kunaweza kutokea balaa kubwa zaidi.

Lile lile la janja ya nyani kuwa kuchagua upinzani ni kukaribisha vurugu - yaani hiyo ni balaa gani kuzidi hii hali ya sasa. Jamani tusitafute visingizio visivyo na mshiko kuirudisha CCM madarakani kama tunalipenda taifa letu. Kumrudisha huyu jamaa madarakani ni kukaribisha balaa kubwa zaidi, period.
 
Mag3

Kuwa na mawazo mazuri ya kuongoza nchi ni tofauti kabisa na kuongoza nchi. Kuna watu wengi wana mawazo mazuri ya kuipeleka nchi hii mahala pema lakini hawana uwezo wa kuingoza nchi hii kufikia malengo hayo. Kikwete alikuja na mawazo mazuri lakini ameshindwa.

Kinachonifanya niwe na wasiwsi pia na viongozi wa upinzani ni jinsi wanavyoshindwa kujiongoza wenyewe ndani ya vyama vyao; kila leo wana migogoro itokanayo zaidi na matumizi ya mabavu katika uongozi na ubadhilifu wa pesa za vyama vyao. Hiyo naichukulia kuwa ni reflection ya uwezo wao wa kuongoza; ukishindwa kuongoza kaya yako huwezi kuongoza kijiji. Ni kutokana na failure ya aina hii ndani ya CCM ambapo walishindwa kuongozana ikafikia wanatumia mabavu ya kufuta majina na kupeana rushwa, ndiyo maana hata Kikwete naye ameshindwa kuongoza nchi.

Sijasema kuwa tuicahgue CCM kwa vile upinzani hawawezi; ninachoonyesha ni frustration zangu kuwa nimekutana ana kwa ana nichague kuliwa ama na SIMBA au CHUI.
 
Back
Top Bottom