Baada ya kutafakari sana, nimepata sababu 51 za kwanini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi aamue kutoshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani. Ninajua kwamba ni "mtaji" kwa upande wa kina Makamba na vile vile ana "sura nzuri" na bla bla bla..
Sasa kati ya hizo 51 nitaanza na zile mbili za mwisho yaani ya 50 na 51. Bila ya shaka na wewe unaweza kuwa na za kwako.. hivyo nawakaribisha wale ambao wanaweza kukisikia au kuchangia sababu zile nyingine 49!
51: Alisema kuwa akichaguliwa tena ataleta vijana na kuwa watu wa rika "lake" waanze kuachia ngazi. Well, kwa vile yuko rika moja nao basi na yeye aungane nao! -HALAFU NANI ATEKELEZE HILI SASA?
50: Hajui kwanini Tanzania ni maskini licha ya kuwa kwenye utumishi wa serikali kwa karibu miaka 30 sasa! Kiongozi asiyejua chanzo cha tatizo ataweza vipi kuliondoa isipokuwa kuziba tu dalili zake. UMEJUAJE KUWA HAJUI. ULIMUULIZA AKASEMA HAJUI. HAPA NI MANDONDOCHA TU YENYE CHUKI BINAFSI NDO YATADANGANYIKA.
49: Aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Ahadi hii haionekani kutekelezeka. Inaonekana ametimiza ahadi ya maisha bora kwa kila muwekezaji wa kigeni! YAANI ITOKEE KWA GHAFLA WE UKO REAL KWELI?
48:Alitangaza kuwa wizi umefanyika Benki Kuu kwa kukombwa mabilioni; badala ya kuacha uchunguzi wa jinai akaunda Kamati kuchunguza jinai. Matokeo yake ni kucheleweshwa kwa upatikanaji wa haki. YAANI ASITUMIE SHERIA BALI UDIKTETA?
47: Serikali yake imeshindwa kutekeleza maazimio yote ya wananchi wa Tanzania kama yalivyoanishwa na wawakilishi wao Bungeni katika maazimio kufuatia Kamati Teule ya Kuchunguza Richmond. Matokeo yake ni kuchochea mgawanyiko mkubwa kabisa wa kimaslahi katika historia ya taifa letu. IMESHINDWA KWELI? HAKUNA WALIOJIUZULU HATA KABLA YA VIKAO VYA BUNGE KUISHA. ANGEKUWA RAIS MWINGINE UNAFIKIRI SPIKA ANGERUDISHWA KUTOKA ZIARA YA NJE?? SI BADALA YAKE UNGEPITISHWA MSWADA WA NISHATI?
46: Aliahidi kupitia mikataba yote mikubwa ya madini ili kutengeneza hali ya "win win win". Hadi hivi sasa hakuna mkataba hata mmoja uliopitiwa na kusahihishwa na badala yake serikali yake imetangaza kuwa mabadiliko ya sheria ya madini yataendelea kuwanufaisha wawekezaji wa sekta hiyo. UNA UHAKIKA?
45: Akiwa ni Mwenyekiti wa Chama Tawala ameshindwa kuleta nidhamu ndani ya chama na matokeo yake wanachama wake mashuhuru wanatukanana na kuitana majina hadharani. Kile kilichoitofautisha CCM miaka ya nyuma sasa hakipo tena. KWANI ALIIKUTA NIDHAMU HUMO. ALICHOONDOA NI WOGA NA SIYO NIDHAMU. HAKUKUWA NA NIDHAMU HUKO HATA KIDOGO. AU KUSEMA NYERERE ANAZEEKA VIBAYA ENZI ZILE ALIPOKUWA HAI NDIYO NIDHAMU?
44: Aligawa fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa kile kilichojulikana kama "mabilioni ya Kikwete" Hadi hivi sasa haijaoneshwa ni kiasi fedha hizo zimeweza kubadilisha maisha ya waliozipata na kurudisha faida. ALIGAWA KWA NANI? KWA MANUFAA YA NANI? NI WANANCHI MASKINI. ULITAKA AKUPE WEWE?
43: Aliahidi kuunda Baraza dogo la Mawaziri lakini matokeo yake Baraza lake limekuwa kubwa na lenye ufanisi mdogo. BARAZA LIWE NA MAWAZIRI WAWILI?
42: Alidai hadharani kuwa anawajua vigogo wa kuuza madawa ya kulevya na kuwa amewapa muda wajirekebishe. Miaka minne baadaye hajatuambia kama watu wale wamejirekebisha au la. HATUJAAMBIWA AU HUJAAMBIWA?
41: Aliahidi kuwa hakuna mwanafunzi wa Kitanzania anayehitaji elimu ya juu ambaye atashindwa kuipata. Lakini serikali yake iliwarudisha vijana wa Kitanzania waliokuwa wanasomea shahada mbalimbali ikiwemo Uhandisi na Udaktari kutoka Ukraine kwa kudai kuwa serikali haina fedha. Vijana wale 30 ingewagharimu shilingi milioni 400 tu kwa muda wa miaka minne. Kiasi hicho ni sawa na kiasi kilichochangwa na serikali kuipongeza Taifa Stars kwa kuifunga Togo! KWA MUDA UPI?
40: Amewaruhusu watendaji wake wakubwa kutumia vyeti vya kielemu ambavyo havitambuliki na vyenye utata. Miongoni mwao ni Waziri wa Fedha Bw. Mustafa Mkullo na Naibu Waziri wa Ulinzi na JKT Bw. Emmanuel Nchimbi. AMERUHUSU KWELI?
39: Licha ya kuahidi kutatua tatizo la nishati chini ya uongozi wake Tanzania imezidi kukabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kuliko wakati mwingine wowote huku nchi yetu ikiwa na vyanzo vya kutosha kabisa nishati hiyo ambayo serikali yake imeshindwa kuviendeleza. KUTATUA KWA SEKUNDE MOJA?
38: Amekuwa akiendeleza safari za nje yeye na viongozi wa ngazi za juu ambazo zimegharimu zaidi mabilioni ya shilingi kwa safari, posho, matumizi ambayo hataki kuyaweka hadharani. UNAJUA SAFARI HIZO ZIMEINGIZA NA ZINATARAJIA KUINGIZA FAIDA KIASI GANI KWA TAIFA?
37: Ameendeleza fikra za uduni wa Mtanzania kwa kutukuza wageni na hivyo kuendeleza kuhukumu taifa letu kwenye utegemezi wa kudumu kwa kupokea misaada ya kiudhalilishaji ya mambo ambayo yamo ndani ya uwezo wa kuzaliwa wa Watanzania. WEWE UNALIPA KODI KIASI GANI? UNAKWEPA KIASI GANI?
36: Serikali yake imeendelea kuwaficha wananchi wa Tanzania mambo muhimu yanayohusu serikali yao na hivyo kuwanyang'anya wananchi usimamizi wa serikali yao kwa kuficha mambo ya Meremeta, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, na Tangold. MTOTO WAKO ANAFUA NGUO YAKO YA NDANI?
35: Akionesha kutokujali sifa za watendaji wake amewateua watu mbalimbali wenye utata wa maadili, na elimu na kuwapa nafasi za kuongoza wizara, na idara nyeti. Miongoni mwao:
- Mustaffa Mkullo - Waziri wa Fedha- ELIMU YAKE HAITOSHI?
- Emmanuel Nchimbi - Naibu Waziri wa Ulinzi na JKT -AMEISHIA LA SABA?
- Andrew Chenge - Alikuwa Waziri wa Miundombinu-YUKO MADARAKANI?
- Peter Noni - aliyesimamia akaunti ya EPA ikichotwa na sasa kapewa Benki ya Raslimali -ALIMTEUA YEYE? MKAPA NI KIKWETE?
- n.k
34: Serikali chini yake imevumilia vitendo vya uharibifu mkubwa wa mazingira na hata kutishia maisha kama yale yaliyotokea huko mgodi wa Mara ambapo watu wamerudhika kutokana na sumu inayotoka mgodini. UNA UHAKIKA NA HILI LA MARA? UTAKUJA UMBUKA BAADAYE.
33: Alitangaza kwa wananchi kuwa msukosuko wa kiuchumi uliokumba dunia usingeleta matatizo ya kiuchumi kwa Tanzania; miezi michache baadaye serikali yake ikaidhinisha zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya "kusisimua" uchumi bila kuweka utaratibu wowote wa kupima mpango huo na kuonesha kitaalamu haja ya mpango huo zaidi ya kuongeza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali. HII NI POROJO SASA NI SAWA NA KUSEMA MVUA HAIJANYESHA LAKINI KUNA MAFURIKO.
32: Ameshindwa kuliongoza Taifa kwa misingi ya Ujamaa ambayo imeanishwa katika Katiba ya Jamhuri na Katiba ya Chama chake na hivyo kuendelea kufanya kazi na kuendesha serikali kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuihifadhi. ALIUKUTA HUO UJAMAA? NANI KAUACHA MKAPA?
31: Licha ya kupigiwa kelele dhidi ya uwekezaji wa kampuni ya India ya Rites Consortium kwenye shirika letu la Reli, aliendelea na kuhakikisha wanawapa mkataba huo. Matokeo yake ni yale yale tuliyoyaona wakati wa Mkapa; mwekezaji kashindwa na anaondoka tajiri! YALE NI MAMBO YA KISHERIA SIYO YA KUKURUPUKA TU. YEYE NI RAIS MAKINI. UMAKINI WAKE NDIO UNAMSULUBU HAPA.
30: Licha ya kubuni na kuhubiri juu ya umuhimu wa Kilimo, ameshindwa kuiongoza CCM kama chama na jumuiya zake kuwekeza katika kilimo kikubwa cha mfano kama chanzo cha mapato endelevu. YEYE AU WALIOMTANGULIA. KWANI AMEANZA KUHUBIRI LINI. NA UMEMPA MUDA GANI KUMPIMA. YAANI MTOTO WAKO WA DARASA LA SITA AMEFELI MTIHANI WA DARASA LA SABA AMBAO HAJAUFANYA?
29:Kama ilivyokuwa kwenye sakata la Richmond, serikali yake imeingia mkataba na kufanya kazi na kampuni ya kitapeli ya Dowans ambayo iliingia nchini kinyemela na kuhalalishwa kwa kutumia maelezo ya uongo. Hadi hivi sasa hajakubali kuanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo. KWANI HUJUI YALIYOTOKEA. MBONA HUKO KIJIJINI ULIKO UMEWEKEWA UMEME NA NYUMBA YAKO YA UDONGO INA SATELITE DISH. MZEE MWANAKIJIJI ACHA LAWAMA ZA POROJO. AU NA WEWE UNAZEEKA VIBAYA?