Sababu Fainali za CAF Kuchezwa nyumbani na ugenini

Sababu Fainali za CAF Kuchezwa nyumbani na ugenini

📝Watu wengi Sana wamekua wakijiuliza ni kwanini falinali za kilabu bingwa afrika na zile za shirikisho zinapigwa home and away mpaka Leo na wengine wakaenda mbali zaidi na kusema mfumo huoo ni wa hovyo sana Bora mechi iwe inapigwa moja tu kwenye neutral ground.

📝 Majib ya swali hili na lawama hizi tayar yalishajibiwa na aliyekua rais wa shirikisho la mpira barani Africa (CAF) bwana Ahmad Ahmad swali hili aliulizwa alipokuja kuzindua mashindano ya afcon ya chini ya umri wa miaka 17 nchini Tanzania.

📝 Jamaa alisema sabaabu kuu ni moja tu ambayo ni issue ya mashabiki, mashabiki wetu wa Africa bado hawana Ile passion au wapo wenye passion lakini hawapo vizuri kiuchumi kwahiyo ni ngumu kwa mashabiki kusafiri kwenda nchi fulani.

Mfano yanga akiingia fainali na Mc Alger na fainali ikachezewa let's say morroco ni mashabiki wachache Sana wataweza kuhudhuria fainali hizo kutoka Tanzania, Algeria pamoja na morroco penyewe na fainali ni watu hivyo itapoteza mvuto.

🧠itachukua muda Sana kuwa na fainali moja katika mashindano yetu haya makubwa.

#africanfootball

View attachment 2618855
Kwa mfano Yanga akafika fainal je ataanzia wapi nyumbani au ugenini
 
Hapo wametumia hiyo mbinu ili kupata pesa kupitia viingilio wana piga kila upande

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Pamoja na hayo, binafsi home and away naiona ipo vizuri. Na sababu zilizotolewa ni halisi kabisa. Mechi ya SImba na Yanga tu kuna watu wanapend a kuitazama LIVE and DIRECT lakini wanashindwa kusafiri kisa pesa, sasa itakuwa kwenda nje ya Tanzania..!! Hata ndugu MAWEED anayesema mfumo huu ni wa kizamani, yeye mwenyewe si wa leo, ni wa zamani hukoo..!!
 
Ni kweli, Africa mashabiki bado ni changamoto. Mfano mechi ya jana (Al Ahly vs Esperance) tena nusu fainali kabisa naona inapigwa bila mashabiki, uwanja mtupu kabisa.
 
Swala sio umbali bali ni uchumi, waafrika wengi ni wachovu sana kiuchumi na tuliona hata kwenye kombe la dunia lililofanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Waliokuwa wanajaa viwanjani ni mashabiki wa kutoka nje ya bara la Afrika na hata wananchi wa Afrika Kusini wenyewe wengi walibaki kukodoa macho kwenye runinga tu.

Jana nimeshangaa mechi inachezwa ya nusu fainali klabu bingwa Afrika kati ya Esperance de Tunis na Al Ahli jijini Tunis huku sehemu kubwa ya uwanja ukiwa tupu kabisa.

Afrika kuna tatizo sana na hadi pale tutakaposhughulikia matatizo ya kiuchumi na kufanya watu wengi wawe na maisha mazuri viwanja vyetu bado vitaendelea kubaki tupu tu kwa miongo mingi ijayo.
 
Back
Top Bottom