Swala sio umbali bali ni uchumi, waafrika wengi ni wachovu sana kiuchumi na tuliona hata kwenye kombe la dunia lililofanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2010.
Waliokuwa wanajaa viwanjani ni mashabiki wa kutoka nje ya bara la Afrika na hata wananchi wa Afrika Kusini wenyewe wengi walibaki kukodoa macho kwenye runinga tu.
Jana nimeshangaa mechi inachezwa ya nusu fainali klabu bingwa Afrika kati ya Esperance de Tunis na Al Ahli jijini Tunis huku sehemu kubwa ya uwanja ukiwa tupu kabisa.
Afrika kuna tatizo sana na hadi pale tutakaposhughulikia matatizo ya kiuchumi na kufanya watu wengi wawe na maisha mazuri viwanja vyetu bado vitaendelea kubaki tupu tu kwa miongo mingi ijayo.