Sababu Fainali za CAF Kuchezwa nyumbani na ugenini

Kwa mfano Yanga akafika fainal je ataanzia wapi nyumbani au ugenini
 
Hapo wametumia hiyo mbinu ili kupata pesa kupitia viingilio wana piga kila upande

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Pamoja na hayo, binafsi home and away naiona ipo vizuri. Na sababu zilizotolewa ni halisi kabisa. Mechi ya SImba na Yanga tu kuna watu wanapend a kuitazama LIVE and DIRECT lakini wanashindwa kusafiri kisa pesa, sasa itakuwa kwenda nje ya Tanzania..!! Hata ndugu MAWEED anayesema mfumo huu ni wa kizamani, yeye mwenyewe si wa leo, ni wa zamani hukoo..!!
 
Ni kweli, Africa mashabiki bado ni changamoto. Mfano mechi ya jana (Al Ahly vs Esperance) tena nusu fainali kabisa naona inapigwa bila mashabiki, uwanja mtupu kabisa.
 
Swala sio umbali bali ni uchumi, waafrika wengi ni wachovu sana kiuchumi na tuliona hata kwenye kombe la dunia lililofanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Waliokuwa wanajaa viwanjani ni mashabiki wa kutoka nje ya bara la Afrika na hata wananchi wa Afrika Kusini wenyewe wengi walibaki kukodoa macho kwenye runinga tu.

Jana nimeshangaa mechi inachezwa ya nusu fainali klabu bingwa Afrika kati ya Esperance de Tunis na Al Ahli jijini Tunis huku sehemu kubwa ya uwanja ukiwa tupu kabisa.

Afrika kuna tatizo sana na hadi pale tutakaposhughulikia matatizo ya kiuchumi na kufanya watu wengi wawe na maisha mazuri viwanja vyetu bado vitaendelea kubaki tupu tu kwa miongo mingi ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…