Sababu ipi inakufanya mpaka sasa haujaolewa au kuoa? Ni kweli haujampata wa kufanana naye au kukwepa majukumu tu?

Sababu ipi inakufanya mpaka sasa haujaolewa au kuoa? Ni kweli haujampata wa kufanana naye au kukwepa majukumu tu?

Sijaolewa na sidhani kama ntaolewa maana wanaume wengi bado hawajakuwa kiakili, hawapendi majumu na kiufupi hawajui kuishi na mwanamke. Utoto umewajaa mtu yuko na mtu lakini anataka kuishi kama yuko single huo si mtihani

Nadhani kuna aina ya vijana unaowapenda, I mean mume unayedream kuishi nae ambapo inakufanya ujikute unaangukia katika kundi la vijana wenye tabia hiyo.

Amini nakuambia machaguo unayofanya ndiyo yandetermine mume au kijana unayempata.

Mfano: unapenda kijana mpiga pamba sana, msafi muda wote, ananukia. Ndiyo hao walamba lips wanaovaa viboxer wanatembelea ambao wao kazi yao kutaka kulelewa na muda wote wapo club na hotel za hadhi.

Mdogo wangu mmoja nilimuelekeza aachane na group fulani la ujana aende kwenye aina nyingine ya group hakuchukua hata mwaka kaolewa. Ila malalamiko ni siyo choice nilitaka mwanaume mrefu, mweupe mwenye kifua! Nikamwambia acha ujinga tulia kwa ndoa, ana watoto wawili sasa hivi katuliaaaa!!
 
Nipo na 30yrs sijaoa,
Sababu : Ninaowataka wapo High key na Mimi naonekana Low key japo Nina kazi na biashara...

Sema wanawake wakishajipata kimaisha then ipeleke habari za ndoa " Utachapwa maswali mpaka utarudi nyuma"

Mimi Kuna mwanamke alishawahi niuliza kwanini hata gari una?? ...hahaha daah!

Kwasasa Wacha niendelee kujiweka sawa zaidi kiuchumi....Mengine Namwachia SIR GOD
 
Oeni/Oleweni Ndugu Zangu Elimu Ni Bure Sasa Hivi
 
Sijaolewa kwa sababu naishi nyumbani na wazazi wakiniona tu na mkaka ni kosa la jinai, [emoji846]
Mimi mtaani wananiulizaga atakuoa baba yako anavokubana ivo? Huwa napata chamgamoto sana unakuta una mwanaume ila muda wa kuonana nae ni mdogo na mbaya zaidi unakuta mwanaume hajielewi yaan ushamwambia hali ya kwenu ye anafosi utoke tuu au utoroke au ukalale kwake ivii kweeli mwanaume mtu mzima unashauri mwanamke wako atoke usiku yaan atoroke ili tuu mlale wote afu agombane na wazazi wake.
Mi huwa napotezea takataka isiyojali mazingira yangu. Mtu unamwambia sijawai lala nje ya kwetu unakuta linataka kufosi muujiza, mxéew shameles.
 
So wewe huwa unatakaje ndoa au unataka mfumo gani wa mahusiano??
 
Sijaoa kwasababu mwanamke wa kuendana na mimi katika kizazi hiki cha kidijitali hayupo.

Naishia kukutana na wanawake wanaojichatisha ovyo na maex. Nikikomaa sana nawapata wale paka mapepe wanaogawa namba ovyo kila kona. Kwa kifupi sioi ng'o!
 
Kuoa au kutokuoa ni uamuzi wako mwenyewe achana na kupata wa kufanana nae!wewe unataka mwanamke nwenye nyash we unayo?
 
Back
Top Bottom