Sababu Kubwa kwanini biashara ya mgahawa wa chakula ni bonge moja la idea.

Sababu Kubwa kwanini biashara ya mgahawa wa chakula ni bonge moja la idea.

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
1.watu ni lazima wale wapate nguvu mtu hawezi kufanya matendo ya kununua nguo, viatu, computer, kusafiri, kufukuzia mchumba kama hajala yaani lazima tu kipaumbele kiwe kula

2.rahisi kuikuza kwani ubunifu wako ndo utafanya upate wateja mfano mtu anakula pale mezani ila kuna vipeperushi vya menu, mambo ya tiba kupitia Lishe, maana watu wengi Wana matatizo ndo maana wanaishia kutapeliwa na wanaojifanya watalaam wa kuuza Madawa sijui ya nguvu za kiume sijui gas na vidonda vya tumbo.. Vipi kama mteja akija kula kwako akakutana na kipeperushi kinachomfundisha kujitibu kupitia Chakula huoni kama unamteka akili lazima awe mteja wa kudumu.

3.uendeshaji wake ni rahisi kwani wahudumu wake ukiwa nao hata watatu unaweza kuendesha mgahawa mzuri tu na pia wadada wanaopika na wahudumu posho yao sio kubwa zamani nilisikia ni Kati ya 3000 Mpaka 5000.

4.inakupunguzia hata gharama za wewe za Chakula chako yaani uwe na mgahawa halafu Tena ukiwa nyumbani upike huo si utakuwa ulofa.. Lazima tu ule ofisini kwako maana yake hapo hata bajeti ya Chakula chako binafsi inamezwa na ofisi.

5.watu hawakopi kopi sana Chakula na kama Mtu hata akikopa asipolipa hasara yake ndogo maana mfano Chakula sahani 2000 mtu akiamua akope halafu asione aibu akakukimbia hatakupa hasara sana ila sio kwenye pombe huko mtu anakopa na anaweza akahama kabisa na bar yenyewe asije Tena.

Ni hayo tu ukiweza kuwekeza mradi huo vizuri location nzuri na Safi basi Sidhani kama kuna jambo kubwa sana linahitajika zaidi ya mpangilio mzuri wa viti na meza, gas na mkaa, vyombo, friji na stock ya misosi basi.
 
Hakuan biashara isiyo kuwa na changamoto. Nirahisi kuandika lakini siyo kuifanya.
 
Back
Top Bottom