Sababu kuu nne kwanini wana CCM Uchwara wanaumia sana wakiona Maridhiano ya Kisiasa yananawiri

Sababu kuu nne kwanini wana CCM Uchwara wanaumia sana wakiona Maridhiano ya Kisiasa yananawiri

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Ukweli ni kuwa ndani ya CCM kuna makundi mawili, yaani lile linalokubali Maridhiano ya Kisisa na lile lisilokubali Maridhiano. Kundi hili lisilokubali Maridhiano ya Kisiasa ndio wengi zaidi na wengi wao wamefikia mpaka lugha za kejeli kwa Rais mwenyewe na kama haitoshi wamefikia mpaka kuwakejeli viongozi wa Chama cha CHADEMA kuwa wamelambishwa asali, chama kimejifia na mengineyo.

Sababu zenyewe ni hizi;
  1. Wengi wao ni wanufaika wakubwa wa zile siasa za maji taka, yaani siasa za kuviziana kukatana mapanga na kufungana magerezani.
  2. Wengi wao ule mfumo wa siasa za maji taka uliwabeba na kuwapendelea zaidi kuna mahali ilifikia huwezi kupata kitu chochote kizuri kama huna kadi ya CCM, mfano ajira za waalimu miaka miwili iliyopita waliokuwa wakipewa kipaumbele zaidi ni wale makada wa chama pamoja wenye kadi za chama cha CCM.
  3. Ni kundi pekee ambalo haliamini na wala halikubaliani na utendaji pamoja na jinsi Rais Mama Samia anavyoindesha Serikali yake na hawampendi kabisa yaani wao kila anachokifanya Mama Samia wanaona anakosea.
  4. Kuhusu Maridhiano ya Kisiasa wao wanaona kabisa wanaenda kupoteza au watapoteza zile fursa zao za hapa na pale zilizokuwa zinawaweka mjini kwa sababu itafikia point sio mwana CCM au mwana CHADEMA wote watakuwa wanapewa favour sawa kila sehemu😁.
 
Hao ni Genge S, walinyang'angwa tonge mdomoni siku jpm alipofariki. Hawa watu ni hatari kwa nchi yetu.
 
Wewe uliyeandika huu Uzi una akili Sana natamani Mama ausome !! Yan huu ndio ukweli CCM walifaidika na ushamba wa jiwe
 
Back
Top Bottom