Sababu kuu ya Gazeti la Tanzania Daima kunyang'anywa leseni ni hofu ya CCM kuhusu kuangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu

Sababu kuu ya Gazeti la Tanzania Daima kunyang'anywa leseni ni hofu ya CCM kuhusu kuangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi wa mwaka huu ni lazima ulete jambo jipya Tanzania .
 
Hilo la kufungiwa kwa Tanzania daima nilikutegemea sana, maana hilo gazeti halimtukuzi Yesu. Na kuelekea uchaguzi mkuu, vyombo vyovyote rasmi vya habari vitadhibitiwa, na vitatakiwa kuhubiri mambo ya Yesu tu na ccm yake, kwa kisingizio cha maslahi ya nchi.
Na hapo ndio huwa nasema sifa ya kwanza ya kiongozi inatakiwa ASIWE MSHAMBA.

UJINGA UNAZIDI SASA
 
Hakuna njia inayoweza kutumiwa na vyama vya upinzani, hasa wakati huu kuelekea kwenye uchaguzi kuyapunguza spidi hayo magazeti yanayoandika habari za kuabudu?

Kuna mamilioni ya wanachama na wapenzi wa vyama hivi, hawawezi kuhamasishwa kuacha kuyachangia haya magazeti?

CCM wameifanya hii kuwa vita, kwa nini msitafute kila njia ya kuwakabili kila sehemu wanakogeukia?

Hii ndiyo njia pekee inayotakiwa kutumika wakati huu. Mapigo yanajibiwa papo kwa hapo bila kuchelewa.

Wekeni staha pembeni, hawa sio watu wa kuwapa heshima hata kidogo..
 
Hii ndio sababu kuu kuliko zote , hizo zingine ni porojo tu

Serikali ya awamu ya 5 kwa miaka yote iliyoingia madarakani imekuwa ikifungia Magazeti yote makini yanayokosoa utendaji mbovu , uonevu na ukiukwaji wa haki za binadamu uliokithiri kuliko wakati wote tangu wakoloni waondoke nchini Tanzania .

Mawio na MwanaHalisi ni miongoni mwa Magazeti yaliyoshindwa kutukuza watawala kizandiki na kumuabudu binadamu kama Mungu alivyoelekeza , yalikuwa ni wahanga wa kwanza wa uharamia uliosimamiwa kikamilifu na Dr Abbas ( ambaye siku ikifika atalipia uharamia huu maana hana kinga yoyote )

Tanzania Daima imeliwa Timing muda mrefu sana na ilikuwa inalindwa na jumuiya za kimataifa tu (nitafafanua ) , sasa kwa vile ccm ina hofu ya kuangukia pua kwenye uchaguzi mkuu wameamua kuondoa gazeti pekee linaloweza kuandika habari za siasa kwa usahihi na kubakisha vikaragosi vyao .

Nawakumbusha kwamba hakuna mahali popote katika dunia hii ambapo SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU .

Itaendelea .....
Useless thinking.
Gazeti siyo muhimu kwenye ulimwengu wa e news.
 
Huyu jamaa ni kama Idd Amin Dadaa tu.
 
Attachments

  • Mkoloni Mweusi.jpg
    Mkoloni Mweusi.jpg
    54.1 KB · Views: 1
Hilo la kufungiwa kwa Tanzania daima nilikutegemea sana, maana hilo gazeti halimtukuzi Yesu. Na kuelekea uchaguzi mkuu, vyombo vyovyote rasmi vya habari vitadhibitiwa, na vitatakiwa kuhubiri mambo ya Yesu tu na ccm yake, kwa kisingizio cha maslahi ya nchi.
Mkuu hapo kwa Yesu unapomzungumzia yesu huyu tumia herufi ndogo ili kumtofautisha na Yesu Mnazarethi.
 
Hakuna njia inayoweza kutumiwa na vyama vya upinzani, hasa wakati huu kuelekea kwenye uchaguzi kuyapunguza spidi hayo magazeti yanayoandika habari za kuabudu?

Kuna mamilioni ya wanachama na wapenzi wa vyama hivi, hawawezi kuhamasishwa kuacha kuyachangia haya magazeti?

CCM wameifanya hii kuwa vita, kwa nini msitafute kila njia ya kuwakabili kila sehemu wanakogeukia?

Hii ndiyo njia pekee inayotakiwa kutumika wakati huu. Mapigo yanajibiwa papo kwa hapo bila kuchelewa.

Wekeni staha pembeni, hawa sio watu wa kuwapa heshima hata kidogo..
Tayari kazi imeanza
 
UKWELI HUU HAPA!

Ni kwamba Tanzania daima pamoja na kuwa gazeti lililokuwa linajiendesha kibiashara, limepata mtikisiko kimapato kutokana na kupoteza soko na mauzo yake kupungua sana.

Hii imetokana hasa na sababu kuu mbili.

Kazi kubwa inayofanywa na JPM, imewafanya wananchi wengi kutoyafuatilia magazeti yenye habari kinzani, labda kwa kuyaona kama hayaendani na uhalisia wanaouna wa kile kilichopo live nchini.

Na kile kisemwacho na magazeti ya mlengo huo kwa sasa!

Hasa baada ya kuaminiwa sana enzi za JK, na matokeo baada ya GEAR ya angani.

Na chadema ilivyobadilika kutoka sera zake za awali,
Na kile inachokihubiri kwa sasa!

Lakini sababu kuu ya pili ni mabadiliko ya teknolojia ya mitandao ambapo kila asilimia kubwa wanazipata habari nyingi mitandaoni.kutoka kwenye simu zao viganjani na hivyo kuyafanya magazeti kupambana na wakati mgumu kwenye soko.

Nguvu pekee iliyokuwa ikiliendesha gazeti hilo ni pamoja na fedha kutoka akaunti za chama cha chadema ambazo hazikuwa rasmi kwa gazeti hilo.
Baada ya TAKUKURU kuanza uchunguzi, imekuwa mwiba mchungu zaidi na hasa baada ya kuonekana tanzania daima ilikuwa chaka la ufujaji wa pesa za chama hicho.

Ushahidi ni wafanyakazi wa Tanzania daima kutolipwa mishahara yao kwa takriban miezi sita mfululizo mpaka sasa.

Kilichofanyika na uongozi wa Tanzania daima na chadema kwa pamoja.

Wameona watafute mbinu ya kusitisha huduma kwa kutafuta sababu itakayoipaisha pia.
Hivyo wakaamua kuchapisha kwa makusudi habari ambayo walijua itawafanya kuchukuliwa hatua na serikali.

Nayo si nyingine zaidi ya huyo askofu bagonza ya kuitisha MAANDAMANO SIKU YA SABASABA,
Eti wakiwa na nguo nyeupe.
Endelea kutunga uongo
 
Yale mafuriko ya Lowasa, hayakumweka madarakani, ndio hivi leo umeme kila mahali, std geji, hospitali, barabara, ndege etc ccm itolewe madarakani, au baadae mtakuja sema mmeibiwa kura na tume sio huru!
 
Hoja ya kijinga sana ! umeishia darasa la ngapi ? ajira hakuna na uchumi umekufa lakini unakenua tu !
 
Back
Top Bottom