Sababu kuu ya Gazeti la Tanzania Daima kunyang'anywa leseni ni hofu ya CCM kuhusu kuangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu

Sababu kuu ya Gazeti la Tanzania Daima kunyang'anywa leseni ni hofu ya CCM kuhusu kuangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu

Hilo la kufungiwa kwa Tanzania daima nilikutegemea sana, maana hilo gazeti halimtukuzi Yesu. Na kuelekea uchaguzi mkuu, vyombo vyovyote rasmi vya habari vitadhibitiwa, na vitatakiwa kuhubiri mambo ya Yesu tu na ccm yake, kwa kisingizio cha maslahi ya nchi.
Ni kweli kabisa halimtukuzi yesu. Bali linamtukuza anaelimiliki.
 
"Serikali ya awamu ya 5 kwa miaka yote iliyoingia madarakani imekuwa ikifungia Magazeti yote makini yanayokosoa utendaji mbovu , uonevu na ukiukwaji wa haki za binadamu uliokithiri kuliko wakati wote tangu wakoloni waondoke nchini Tanzania"

Mkuu, by the quotation above, you have nailed it.
Tanzania Daima halijawahi kuwa gazeti makini. Mbona hawalifungii Mwananchi. Umeshawahi kuona Mwananchi linaisifia Serikali?
 
Hii ndio sababu kuu kuliko zote , hizo zingine ni porojo tu

Serikali ya awamu ya 5 kwa miaka yote iliyoingia madarakani imekuwa ikifungia Magazeti yote makini yanayokosoa utendaji mbovu , uonevu na ukiukwaji wa haki za binadamu uliokithiri kuliko wakati wote tangu wakoloni waondoke nchini Tanzania .

Mawio na MwanaHalisi ni miongoni mwa Magazeti yaliyoshindwa kutukuza watawala kizandiki na kumuabudu binadamu kama Mungu alivyoelekeza , yalikuwa ni wahanga wa kwanza wa uharamia uliosimamiwa kikamilifu na Dr Abbas ( ambaye siku ikifika atalipia uharamia huu maana hana kinga yoyote )

Tanzania Daima imeliwa Timing muda mrefu sana na ilikuwa inalindwa na jumuiya za kimataifa tu (nitafafanua ) , sasa kwa vile ccm ina hofu ya kuangukia pua kwenye uchaguzi mkuu wameamua kuondoa gazeti pekee linaloweza kuandika habari za siasa kwa usahihi na kubakisha vikaragosi vyao .

Nawakumbusha kwamba hakuna mahali popote katika dunia hii ambapo SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU .

Itaendelea .....
Lipo wazi Hilo, sababu kuu ndo hio.
 
Ukiona mtu hata anaota CCM kuangukia pua 2020 unapaswa utilie shaka fuse zake kichwani kama ni nzima au zimeshaungua.

Kwa mwenendo wa siasa za nchi CCM bado ina miongo kadhaa madarakani.
 
Magazeti ninayonunua yote ni bora. Sijawahi kusoma hata kutazama fronts za gazeti hili. Nadhani ni la hovyo, lifungwe tuuu
 
Back
Top Bottom