Uchaguzi 2020 Sababu kuu ya Lissu kushindwa, asilimia 80 ya Watanzania wanaishi Vijijini hawamjui Lissu ni nani, Magufuli anajulikana kila kona Vijijini


Soma kuelewa kilicho andikwa. Ukabila umeuona wapi hapi?

"Ipo tofauti ya kanda ya ziwa, Chatto na usukumani wasikoelimika yaani ambako ujinga tololo ndiyo kwao. Rejea tafiti za TWAWEZA."

Umeshindwa kufahamu kuna usukumani walikoelimika?

Kiswahili hujui, povu tu utafikiri umebugia OmO?

Hoja yako ni ya kijinga zaidi kuliko maelezo.

Soma kuelewa kabla ya kuanza kupayuka kipoyoyo poyoyo.
 
Mbona wagombea wa upinzani ni wengi kuna Membe,Lipumba,Rungwe kwanini CCM mumuwaze Lissu tuu.Mada za Membe zimeisha jukwaani.

Mlishasema CDM imekufa sasa mnashindanaje na kiumbe kilichokufa.
 
Hata watu wasiojulikana hawajulikani ila wana julikana
 
Ni kweli unachokisema na hata mimi nikiwa mmoja wao.
Lakini kiukweli haya ni makundi ya watu wachache miongoni mwa wapiga kura.
Wapiga kura wengi ni wakulima wadogo sana na masikini walaa hawajihusishi na hivuo vyama.
Wafanyakazi,wakulima wakubwa na wafanyabiashara wengi sio wapiga kura,ni wachache mnoo kati yao.
Kama kweli tunaitaka ikulu twendeni vijijini huko ndani ndani haswaa mbona TASAF inafika huko ninyi mnakwama wapii.
 
Kwani kushindwa ni dhambi isiyozungumzika ?!. Si no lazima mshindi apatikane au ?!.

Vinijini unakokusema watu wana hali mbaya sana. After all unazungumzia kukosa office vinijini !!. Miaka mitano yote mmepiga marufuku vyama vingine kufanya shughuli zao za kikatiba . Halafu leo unawaona Cdm kama wazembe ?! Strange
 
Nakwambia magufuli kasababisha umasikini wa kutupwa kwa wakulima. Subirini Muone October 2020.
 
Singida, Kilimanjaro,Arusha, Dar kote huku Lissu atabembea

Kwa sasa ccm watumie hekima kubwa sana.
Maana mioyo ya watu ipo Emotional zaidi. Wanaweza kwenda hata kuvunja gereza alipofungwa Lisu. Yaani wawe makini kwa mtu ambae makini waone alivyopokelewa licha ya mkwara wa police [emoji601] kuwaambia wasifike uwanja wa ndege.
Na wapo watu watakwenda kumwona aliyekufa na kufufuka kimiujiza.
Lisu yupo mioyoni mwa watu.
Hata wana ccm wengi mioyoni mwao kwa walivyotendewa utawala huu wanatamani ufutiliwe mbali.

Maana kuna hati hati ya kubadilishwa katiba ili kuwe na utawala wa kiimla.
 
Mbona Lake Zone CDM ishakufa kitambo.imebakia kidoogo mkoa wa Mara,tena ni kwa sababu ya wabunge walionao ndo maana kidogo CDM inaskikaskika kwa kanda ya ziwa.
 

Tangu lini kanda ya ziwa imekuwa ngome kuu ya CCM? Au unamaanisha ya Magufuli? Halafu, siku hizi CCM nayo inaegemea kwenye ukabila/ukanda? Punguza desperation. Achana na Lissu; atafanya upayuke mengi na kuishia kuwaudhi mabosi wa CCM.
 
Tangu lini kanda ya ziwa imekuwa ngome kuu ya CCM? Au unamaanisha ya Magufuli? Halafu, siku hizi CCM nayo inaegemea kwenye ukabila/ukanda? Punguza desperation. Achana na Lissu; atafanya upayuke mengi na kuishia kuwaudhi mabosi wa CCM.

Umeongea point mkuu

Kwanza nashukuru kwamba hawa hawajatoka ccm watasaidia chadema ishinde

Nape
Makamba January
Ngereja
Makamba Junior
Kinana
Na wengine wengi ambao wametendwa na utawala huu.

Wapo walioonewa kwenye majina hewa na walikuwa wanakaribia kustaafu

Watoto waliokuwa wanasoma udom kufutiwa shule zao na mtoto wa mkulu kuendelea kusoma

Walio vunjiwa nyumba zao na kutokulipwa fidia

Wale ambao wametumbuliwa bila kufuata procedures za kazi na kudharirishwa

Walio bambikiwa kesi mbalimbali na kufungwa.

Yaani Lisu atakuwa anateleza tu maana hawa watu watamsaidia sana kuingia Ikulu.

Sasa vyama viungane watoe mtu mmoja yaani
Lisu apeperushe bendera Bara
Maalimu saif apeperushe bendera Zenji

Alafu wagawane majimbo. Yaani hata kama Lisu atashindwa lakini wabunge wengi wawe upinzani watatoa Rais kabisa .
 
Hahaa eti baada ya uchaguzi Chadema itakufa, sio nyie mliosema haitafika 2020.
 
Kwani uchaguzi umeshafanyika? Au mimi bado siko Tanzania?
 
Aisee hii paranoia mliyopata ni ya next level....

Uzuri wa Lissu ana IQ kubwa mno,hii ni biological lottery alishinda naturally,nyie na mawe IQ zenu ni kama zangu,naona mnatoka jasho la ulimi!

Lissu kaja naona kila mtu kakaa mguu sawa....katest mitambo tuu!
 
Mkuu acha kulinganisha Rais Magufuli na Vitu vya ovyo ovyo kama msaliti Lissu!!
 
Bilabila we ni mwana PCM umeanza lini siasa? umesahau KissCamp
Kanda ya Ziwa ndiko walikovhomewa nyavu na kupasuliwa mitumbwi na Luhaga Mpina kwa baraka za Magufuli, Kanda ya ziwa ndiko walikotaifishwa mifugo na TANAPA, Kanda ya ziwa ndio waliovurugiwa vyanzo vyao vya uchumi kila mahali. Unaongea bila utafiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…