Sababu kuu ya Tanzania kutoendelea ni unafiki wa watu wake


Na siku zote Unafiki na Upumbavu huwa vinaenda pamoja hivyo huenda linalowagharimu hao Wananchi hapa ni haya Mawili.
 
Tusiopelekeshwa na njaa tunawaunga mkono CDM, haya yanayotokea sasa ni ya muda tu yatapita,
 
Watu wakianza kulalamikia ccm unaweza kudhani wao wanautofauti na wanaoiongoza hiyo ccm, kumbe masikini Nyani haoni kundule.
 
Wataalamu kibao wapo na hawana kazi wewe Kiazi unamuona mwele tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo ni sifa kuwa na wataalam wengi wasiotumika ilhali tukiwa na changamoto za kutosha hapa nchini?Donor country inayoshindwa kuwatumia wataalam wake iliowasomesha kwa gharama kubwa ni sahihi?Ulitaka nani awatumie kutunufaisha na kuongeza fursa na wigo wa ajira?Hivi hamjielewi kuwa kwa utetezi wa namna hii mnajidhalilisha?
 
Nakubaliana na ndugu mtoa hoja kwa 100%.
Matatizo ya mtanzania yanatokana na mtanzania mwenyewe. Hali ya kisiasa yuliyokuwa nayo 100% ni unafiki na uoga usiomithilika.
Tunahitaji toba.
 
Huwezi kuamini namna watz walivyo wajjinga. Utazimia ukijua ukweli na hata viongozi wetu ni mazuzu mpaka inatisha.
 
Duh! Kumbe wewe ni Mnafiki! Ok
 
Halafu unakuta IP Address Yake inasoma Indiana@USA
#Mtaalamghost
 
Kuna tatizo kwenye bongo zetu sio bure.Nakwasababu wajinga ni wengi wale waliojanjaruka wanatumia hiyo fursa kuburuza wengine nakwaubongo lala wetu tunaona sawa tu.Tukitoka hapo tunalaumu wazungu kutuhujumu kumbe tatizo ni sisi wenyewe.
 
,Nakukubali sana mkuu isipokuwa nina mashaka na Mbowe anaweza naye akawa nafiki. Kwa sasa chama ambacho naona kina muelekeo wa chama cha siasa ni ACT wazalendo. kina katiba inayofanana sana na ile ya ccm ya zamani na azimio la arusha kimtazamo na naona ndicho chama pekee kinachoweza kumkomboa mtanzania. CDM imekaa kama saccos ya kabila fulani hivi na sio chama. CCM ndo usiombe ni genge la wezi na watekaji. HIVI NDIVYO NIONAVYO MIMI
 
Naunga mkono hoja. Maana hata hapo umeandika unafiki mtupu ukimpigia chapuo mnafiki mkuu.
 
Kutoendelea kivipi? Kiuchumi au kisiasa? Kuendelea kiuchumi jibu lake sio siasa ila teknolojia na elimu ya uchumi, kisiasa ni kuwa na amani na demokrasia na uhuru wa kujieleza na hotuba.

Sisi waafrika tunarubuniwa na wa magharibi kusema eti uongozi bora ndiyo chanzo cha uchumi bora, lakini tunadanganyika na kurubuniwa ili tusiendelee kiuchumi na kubaki na mvutano wa kisiasa kusababisha vurugu ambazo zinatukwamisha kimaendeleo hasa kwenye vita vya kisiasa au kikabila.

Jibu la maendeleo ambalo wazungu hawapendi tulipate, ni sayansi na teknolojia kuunda bidhaa zetu wenyewe kuanzia mashine za viwanda, vifaa na madawa ya hospitali hata magari mpaka computer na simu. Hapo sijataja meli na ndege na silaha. Wazungu hawataki tujitegemee kwa hayo, hivyo wanaturubuni tufikiri chanzo cha umasikini wetu ni siasa za uongozi ili tupigane na wao waingilie kututawala na kuchukua malighafi zetu.
 
Punguza mtazamo hasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…