Naomba niandike haya ili tuweke kumbu kumbu sawa.
1. Mimi ni mfanyakazi wa maabara kuu ya taifa kwa miaka sita sasa kwahyo kwa sehemu ninafahamu nini kinaendelea hapa.
2. Tumekua kimya na kwa sababu ambazo zipo wazi tumeamua kufanya kazi kwa uwezo wetu wote ili kuwasaidia watanzania katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa huu wa mlipuko.
Swali la kujiuliza ni kweli kuna uhujumu wowote unaofanywa na hii maabara? Na kama upo je ni kwa faida ya nani? Pengine kamati ilioundwa inaweza kuja na majibu lakini kabla ya hayo majibu tujiulize kama inaweza kwenda kinyume na kile alichokisema mkuu?
Nimeamua kuandika baada ya kuwepo kwa mijadala mingi mitandaoni ikijaribu kuwaza juu ya ubora wa maabara yetu na vipimo vyake, na kama mfanyakazi wa maabara hii niliposikia hili kwa mara ya kwanza kabisa nlistuka na leo asubuhi nikawahi kwenye database ya wagonjwa wote waliopimwa na kujaribu kuangalia kama kweli hayo yanayosemwa kama ni ya kweli au la?
Cha kushangaza ni kuwa hakuna hata jina moja lililotajwa na mheshimiwa jana lipo kwenye database yetu hapa! Wengi wa wanaofanya kazi maabara wanajua kuwa wakati mwingine mfumo unaotumika ni wa sample kuwa na patient numbers na hivyo kufanya vigumu kutrace majina ya mgonjwa kama huna hiyo patient number kwenye system. Yes! Lakini nimefuatilia majina yote yaliyotajwa jana kuanzia mapokezi hadi sehemu majibu yanatolewa nimeshindwa kuliona jina hata moja!
Nikasema ngoja nijisumbue, nikamtafuta mtu wa IT anisaidie kama naweza pata majina hayo lakini kwa kushirikiana nae tumekosa kuona jina hata moja!
Mwisho nimebaki kuwa na maswali mengi sana
1. Je mh raisi alidanganywa? Je waliomdanganya walifanya hivo kwa maslahi ya nani?
2. Je mh raisi alikuwa anafanya propaganda kuhamisha mjadala? Kwa hili amefanikiwa.
Kitu ambacho wengi wenu hamuwezi kujua ni kuwa sample ikiletwa hapa tunazitenganisha za wale waliokwisha fariki(ambazo ni nyingi) na zile za wagonjwa wakawaida waliopo wodini
Na kwa sababu ya udogo wa mortuary facilities zetu tuliombwa kuzifanyia kazi za wale waliokwisha kufa ili wazikwe mapema! Na naweza kusema ni wengi sana wanaokufa kwa ugonjwa huu! Ukichukua sample kumi za wagonjwa waliokufa basi sita hadi nane zinakuwa positive!
Mengine tukae kimya tusubiri mda utuamulie la kusema
huyu ni mfanyakazi wa maabara ya taifa anatufungua macho.