Sababu kwa nini Ulaya ina tatizo dogo sana la ajira

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Hizi ndio sababu kwa nini tatizo la ajira sio kubwa sana Ulaya

1. Ulaya ina makampuni mengi sana
Nchi nyingi za Ulaya kama Germany, United Kingdom, France nkzina makampuni mengi sana makubwa kama BMW, Siemens, Volkswagen nk
Makampuni haya yanatoa mamilioni ya ajira, direct na indirect

2. Nchi za Magharibi zina viwanda vingi sana
Wazungu wali industrialize mapema sana tangu karne ya 18 kupitia tukio la kihistoria linaloitwa Industrial Revolution.
Hivyo hadi leo wana:
* Viwanda vingi (takribani milioni 2.6)
  • Teknolojia ya hali ya jui
  • Utafiti mwingi
Hivi vyote vinatengeneza ajira nyingi.

3. Elimu yao inaendana na soko la ajira
Vyuo na colleges zao zinafundisha skills zinazotakiwa na makampuni.
Mfano:
Engineering
IT
AI
Medicine
Manufacturing
Ndiyo maana watu wengi wakienda kusoma masters Ulaya wanapata kazi hukohuko

4. Serikali zinasaidia biashara
Serikali zao zimejenga miundombinu bora, sheria nzuri za biashara
mikopo yenye mashartia nafuu kwa biashara
Hivyo makampuni mengi yanafunguliwa → ajira zinaongezeka.

5. Watu wachache kuzidi nafasi za kazi
Nchi nyingi za Ulaya zina watu wachache wanaozaliwa sasa.
Kwa mfano katika Germany na Italy kuna upungufu wa wafanyakazi.
Ndiyo maana hata wanaruhusu wahamiaji kuja kufanya kazi.
Wazungu walijitahidi kupunguza uzaaji usio na mpango, waliweka sheria kali zinazowabana wazazi wasiotimiza majukumu yao, mfano mwanaume kumzalisha mwanamke na kumwacha alee watoto peke yake. Sheria hizi zilisaidia kukuza watoto walioelimika na kupunguza watoto wasio wa lazima ambao wangeleta mzigo kwenye soko la ajira

Tanzania ikitaka kupunguza tatizo la ajira inapaswa kuwa na makampuni mengi, makampuni yatahitaji watu, watu ndio hao waliopo nchini, watu watapata ajira kupitia makampuni either kwa kuajiriwa direct au kujiajiri wao wenyewe kama effect za uwepo wa kampuni hizo

Ili makampuni yawe mengi Tanzania inapaswa kuwa na viwanda vingi, ku improve sekta za kilimo, utalii, ujenzi nk. Pia lazima kuwepo sheria rahisi za ujenzi wa viwanda ili ku attract viwanda vingi nchini, na kuwepo kodi nafuu sana kwa wafanya biashara wanaoanza. Ni vyema kodi zikapandishwa kidogo kidogo kwa mfanya biashara pale atakapofanikiwa

MFANO WA MAKAMPUNI NA VIWANDA VINAVYOHITAJIKA TANZANIA
1. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya magari na pikipiki
Mfano kutengeneza spare parts za magari, spanners, washers, matairi, engine oils nk

2. Viwanda vya kutengeneza electronics
Nyaya za umeme, Charger za simu, TV, power banks, monitors, ear phones, earbuds nm

3. Makampuni yanayofanya food processing
Kusindika nyama, samaki, tomato paste, tambi, maziwa, juisi, biskuti, chocolate, pipi nk

4. Makampuni ya Fertilizer & Chemicals
Kutengeneza fertilizers, vifaa vya plastics, kemikali za viwandani, dawa za kusafisha chooni, dawa za kuua wadudu shambani nk

5. Makampuni ya saruji na vifaa vya ujenzi
Kwa sababu ujenzi unaongezeka sana Africa, basi Tanzania inahitaji viwanda vingi zaidi vya cement, mabati, tiles, vioo, aluminium nk

6. Makampuni ya Software & AI
Mobile apps, fintech, AI software, cyber security

7. Makampuni ya meli na logistics
Shipping companies, cargo airlines, logistics companies

8. Makampuni ya Tourism technology
Safari booking platforms, Travel apps, eco tourism companies

9. Makapuni ya Renewable energy
Kutengeneza solar panels, batteries etc

10. Makampuni ya uchimbaji madini

NB: Rasilimali kubwa zaidi Tanzania ni watu milioni 68+ huku zaidi ya 70% ni vijana, meaning nguvukazi ipo. Bila makampuni na viwanda hatutoboi
 
Vyote hivyo ni uongo ,viwanda vinatengeneza bidhaa ili wakauze wapi? Kila nchi ikiwa na viwanda vingi unafikiria nan atamuuzia mwenzie?

Uchumi wa pesa ni utapeli kwa nchi za afrika .Zamani watu walitegemea chakula tu na mambo mengine ila sasa maisha lazima yawe magumu ; bills lukuki mpaka kifurushi mtu unatumia mpaka elfu 5 kwa siku na zaidi.

Uchumi wa pesa umeshindwa kuweka usawa duniani ,zaidi ni unyonyaji kwa mataifa madogo.
 
Ndugu Tanganian Nakupinga kwa mifano. China bilashaka inaviwanda vingi duniani inawezakua nchi ya kwanza au yapili lakini bado anakua mteja muhimu wa bidhaa,maligafi na tech za nchi nyingine.2 USA inaviwanda vingi sana na pia ina matajir wengi sana levo za kidunia lakin yeye mwenyewe bado mteja wa viwanda wa mazao ya viwanda vyake pia ni mteja wa maligafi na bidhaa kwa nchi nyingine hata nchi za ulaya zina viwanda vingi na bado wao wenyewe wakawa wateja na bado wananunua maitaji nje ya nchi zao kwaiyo kusema kila mt akiwa na viwanda basi soko litakufa au wateja watakosekana sio kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…