Sababu mfumo wa Kichina wa Chama kimoja hauwezi kufanikiwa Tanzania?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Kuna watu wanajidanganya CCM kwamba chao chao na Tanzania ifuate mfumo wa Kichina badala ya mfumo wa kidemokrasia. Ukweli ni kwamba mfumo inabidi uendane na jamii. Sasa tujiulize kama haya yanawezekana. au la. Kwa mawazo yangu haiwezekani kwenye jamii ya Watanzania kwasababu chache tu

1. Jamii za Watanzania ni watu wa imani sana huwezi kuwa na huu mfumo na ukwawa na uhuru wa kuabudu. Maana huu mfumo wa Kichana unategemea watu wate waamini serikali pekee sio dini yeyote. Yaani wananchi wanatakiwa kuabudu mfumo na chama kimoja na sio dini zao ndiyo maana China huwezi kusikia Bakwata wala TEC

2. Makabila Watanzania ni jamii imetokana na makabila yameunganishwa yakawa nchi lakini kila kabila lina tamaduni zake. Huwezi kutumia mfumo huu wa kichina kama kila jamii ina kabila na mila tofauti. Mfano hata kuzika ni utamaduni wa kidini na kikabila huwezi kwa jamii zetu ukabadilisha hilo na sera ya kuzika eti itoke kwenye chama au serikali!

3. Rushwa tatizo la CCM ni wabinafsi na wengi ni wala rushwa. Ni watu wachache wanaenda CCM kwasababu ya uzalendo. Wenzetu wa China uzalendo uko mbele na wala rushwa wanafungwa au hata kuuliwa. Ndiyo maana hata Nyerere alikubali kushidwa kwamba jamii yetu haiwezi kuwa kama ya China. Hii ndiyo sababu Nyerere alikubali mfumo wa vyama vingi.

4. Maendeleo ya uchumi. Wakati wachina wana amini chama chao kimeleta maendeleo watanzania wengi wanaamini CCM imeleta umasikini!! sasa huwezi kuleta umasikini kwenye nchi halafu ukategemea wananchi waunge mkono chama au mfumo.

Kwasababu hizi chache tunapoteza muda kwa wale wanaofikiria mfumo wa kichina. Je watanzania watakubali mfano serikali na chama tawala kuwatoa watu mimba au kupanga idadi ya watu kwa jamii zetu ? Haiwezekani lakini wezetu wa China ndiyo nguvu ya hicho chama si upigaji tu ni kama dini huko china. Mfumo pekee utakao fanikiwa kwa jamii ya watanzania ni demokrasia bila hivyo utakuwa na jamii ambayo haina usalama wala kuwa wamoja. Tusipoteze muda kama kweli tunataka maendeleo.
 
Huwa nawashangaa sana ccm wakijilinganisha na chama cha kikomunist cha china
 
Mfumo wa China umejijenga kwenye mfumo unaoitwa Confucianism. Soma kwa undani kuhusu huu mfumo na utagundua kuwa mfomo wa chama kimoja siyo msingi wa mafanikio yao.

​

Back
Top Bottom