Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,370
- Thread starter
- #41
Uchangiaji wa Mbeya katika pato la taifa haupo relevant na mzunguko wa pesa kwenye jiji la mbeya, Tunduma walikua wanasaisia mno katika hii ishu na kwa sasa wana mkoa wao wa songwe bila kusahau shughuli za uchimbaji madini chunya na chai huko tukuyu, Ukija kwa hapa Mbeya mjini mzunguko wa pesa ni wa kawaida mnoOkay sasa umekuja vizuri. Umekuja kimjadala zaidi.
Ni hivi si kweli kwamba mzunguko wa Pesa Mbeya ni mdogo, kama utakumbuka vizuri Mbeya ni kati ya wanaochangia sana pato la taifa ila serikali imekuwa haiwarudishii wana Mbeya kile wanachostahiki kupitia maendeleo. Uendelezwaji wa mkoa wa Mbeya na jinsi uuonavyo ni matokeo ya nguvu za individuals wa mkoa huo.
Aina ya uwekezaji ambao tulitarajia seikali kuufanya mkoani humo ili ku influence maendeleo ni kama vile uwanja wa ndege (ambao hivi sasa tunao), na miundo mbinu mingine kama barabara majengo ya ofisi na kuviinua vivutio vingine vilivyomo mkoani humo. Siasa zimechangia sana kuua mkoa wa Mbeya.
Kuhusu kukosekana kwa Clubs.
Tatizo kubwa lililopelekea mkoa wa Mbeya kuwa nyuma upande wa clubs and the likes ni suala zima la usalama. Kama utakumbuka kumekuwa na matukio ya ujambazi na upigwaji nondo watu ulishamiri sana hapo mkoani na mida watu kupigwa nondo ilikuwa ni baada ya giza kuingia, mbaya zaidi swala hilo lilihusishwa na imani za kishirikina hivyo unaweza ukaona namna vile jamii inapokuwa na hofu katika kuitikia mabadiliko yanayokuwa yanaletwa ndani ya jamii husika.
Watu watapata wapi ujasili wa kutoka nyumbani usiku kwa ajili kwenda kula bata!? Sasa hivi Mbeya ina recover kutoka kwenye majeraha hayo ya kisiasa, ujambazi na kishirikina.
Pia, to underline that and conclude, Mbeya si wapenzi wa Bongo fleva
Wilaya kama zenye mzunguko mkubwa wa pesa wasanii wanaendaga na kuna kipindi Diamond alienda kufanya show kwa kiingilio cha elf 50 na tiketi ziliuzika kama njugu, Mbeya mzunguko wa pesa ni mdogo na ushahidi unaanzia kwenye bidhaa zinazonunuliwa sana, kwa mfano kwenye maduka ya simu mengi ni tecno na itel ndio zinatoka sana hasa pale kwa mtawa ilomba na maduka ya kabwe, Wachache sana wanaomudu bei za samsung ndio huwa wanaenda dubao phones pale town.
Kwenye usalama hapo hio ni hoja isio na uzito, kuna watu wengi tu wanakwenda majumbani kwao wakitokea city pub na bar nyingi za kila kona ya hili jiji, pia kuna wanaokwenda majumbani kwao usiku wakitokea kwenye biashara zao,
Narudia tena, Huenda wewe ni wakuja au unajifungia sana ndani ukiwa hapa Mbeya, hizi nondohuwa zinakuja kwa haraka na kuisha kwa haraka, zikianza mara nyingi zinadumu kwa wiki 2 tu mara moja kwa mwaka na mara chache mara 2 kwa mwaka, Hizi nondo kwa hapa Mbeya hazitakuja kuzuia watu wachelewe kurudi makwao kutoka city pub, kwenye mikesha ya kanisani au sherehe.