Elections 2010 Sababu Nyingine ya Kutoichagua CCM

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
mwalimu.jpg

Ridhiwani Kikwete akiwa na mwalimu aliyemsomesha darasa la kwanza 1987 katika Shule yaMsingi Matangini Mwl. Sophia Makong'o, alipomtembelea nyumbani kwake mjini Nachingwea. Kulia ni mtoto wa Mwl. Makong'o, Husna, ambaye alisoma naye Ridhiwani darasa la kwanza katika shule hiyo.

Angalia maisha ya mwalimu aliyemfundisha huyu Kingmaker wetu yalivyo leo. Tulitegemea mwalimu huyo baada ya miaka 23 awe ana maisha mazuri zaidi lakini kumbe leo analilia kitanda cha kamba kisicho na godoro.

Attachments

  • mwalimu.JPG
    mwalimu.JPG
    62 KB · Views: 206
Inasikitisha sana, jamaa hata hakuona noma na tabasamu lake la uongo huku kukiwa na vitanda vya kamba pembeni.
 
huyu riz1 atakuwa mwehu kama mak.mba, yaani haoni soni hata kidogo juu hali dhalili ya mwalimu wake eti anatabasamu halafu anamwambia mwalimu wake chagua ki.wete. ajabu
 
Masikini hajavaa hata viatu.......kuna wana roho ngumu...
 
Ridhiwani Kikwete akiwa na mwalimu aliyemsomesha darasa la kwanza 1987 katika Shule yaMsingi Matangini Mwl. Sophia Makong'o, alipomtembelea nyumbani kwake mjini Nachingwea. Kulia ni mtoto wa Mwl. Makong'o, Husna, ambaye alisoma naye Ridhiwani darasa la kwanza katika shule hiyo.

Angalia maisha ya mwalimu aliyemfundisha huyu Kingmaker wetu yalivyo leo. Tulitegemea mwalimu huyo baada ya miaka 23 awe ana maisha mazuri zaidi lakini kumbe leo analilia kitanda cha kamba kisicho na godoro.

Kama ukiangalia vizuri picha ya huyo mrembo Husna unahisi kama vile anatoa message fulani kwa watazmaji......najua JF kuna wataalam wa Arts wanaweza kututafsiria hiyo picha ya Husna
 
Kichuguu,
Nadhani hii ni living room-sleeping room combined.
 
Lakini kosa la Riz1 ni lipi hapo? wangapi wetu walau tunawakumbuka watu waliotufikisha hapa tulipo?
 
Kosa ni jinsi huyu mama anavyodanganywa, JK alimwahidi maisha bora miaka 5 iliyopita, leo hii mtoto wake Ridhiwani, anamtembelea tena huyu mwalimu wake akiomba amchangue JK kwa maisha ya kasi mpya.

Mwalimu mwambie, HATUDANGANYIKIII
 
huyu dogo anapenda sifa kweli,hata hamuonei huruma huyu mwl ambaye hata kwa kumuona tu unajua ana maisha magumu na ni mgonjwa!
 
Hapo mnajaribu kufananisha au kulinganisha visivyo linganishika, mwalimu alimfundisha kijana akaelekea mjini, mambo safi.

Ninavyoweza tafsiri hii picha ni kuwa watu wengi hukimbilia mijini ili kuwa na maisha bora. Hata hawa viongozi wetu tukiwachagua kama wabunge wote wanahamia DAR na kusahau waliowachagua. Kuna msemo unasema "Usiache mbachao kwa msala upitao". Mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa vijijini yanahitaji watu wenye uzalendo, wanaopenda wote tuendelee, wenye mitazamo ya kusaidia masikini.

Wananchi wameshapewa ahadi nyingi na wanasiasa, lakini hawajui nini ni haki yao na nini sio, walimu walipotaka kugoma kisa mshahara ni mdogo, wengi wetu tuliona kugoma sio suluhisho lakini pengine kugoma kungeweza kumsaidia mwalimu huyu walau akaweza kujikwamua. Hapo inaonyesha kesha kata tamaa ya maisha, anasubiri siku zake alale kwa heri. Huyo binti alitamani kuwa mwalimu lakini hana tena matumaini zaidi ya kufikiria kwenda mjini pengine zali litamwangukia.

Tanzania bila CCM inawezekana, kura yako ni ukombozi wako, piga kura kwa kufuata hoja na si kwa mazoea!
 
Lakini kosa la Riz1 ni lipi hapo? wangapi wetu walau tunawakumbuka watu waliotufikisha hapa tulipo?

Kosa la kijana wenu ni kuchekelea maisha duni ya mwalimu wake, alitakiwa angalau awe na sura ya huruma kwenye picha hiyo... lakini kwa vile Rizi na CCM yake hawana huruma na wanainchi basi ni kukenua kwa sana tu, ukiwahoji watakujibu wewe si raia etc
 
Kama ukiangalia vizuri picha ya huyo mrembo Husna unahisi kama vile anatoa message fulani kwa watazmaji......najua JF kuna wataalam wa Arts wanaweza kututafsiria hiyo picha ya Husna
Huyu binti mi naona kalazimishwa kukaa pichani,lakini anaonyesha kabisa anasura ya kisasi!!
 
Kama ukiangalia vizuri picha ya huyo mrembo Husna unahisi kama vile anatoa message fulani kwa watazmaji......najua JF kuna wataalam wa Arts wanaweza kututafsiria hiyo picha ya Husna
Yes unachosema ni kweli kabisa kama ungependa kujua msg yenyewe angalia vizuri sehemu ya macho yake yalivyojawa na huzuni pamoja na kukosa tumaini. Licha hata ya kutembelewa na ugeni huo lakini tabasamu limeshindwa kabisa kuganda kwenye uso wake. hata huyo mwalimu wake anmetabasamu kwa kukunja sura ionekane kama imetbasamu lakini wapi mkuu, usifanye mchezo na njaa.
 
Kama ukiangalia vizuri picha ya huyo mrembo Husna unahisi kama vile anatoa message fulani kwa watazmaji......najua JF kuna wataalam wa Arts wanaweza kututafsiria hiyo picha ya Husna
tukianza na RIZ1 ktk mkono wake wa kulia amevaa pete ambayo haina tofauti na pete anazonadi mlizi wa familia yao (yahaya huseni). hivyo inaashiria dogo yupo under full maulinzi kwa 24/7. Cheko la RIZ1 ni bashasha za kupiga picha na kuongeza another image kwenye utalii wa ndani profile.
Turudi kwa HUSNA (mrembo bila vikorombwezo), ukianzia kwenye wajihi utagundua hapo amevunja sanduku kusaka kiwalo latest ambacho zaidi ya hapo hana nguo tena. twende kwenye smile yake haina tofauti na smile ya ile picha maarufu ya MONALISA aliyochora bingwa Leonardo Da Vinci enzi za Art Renaissance. Smile hiyo ipo half sad and half happy. kisaikolojia inaonesha kuwa anajilazimisha kutabasamu ingawa nafsi yake ina ukungu wa maumivu. angalia mikono ya HUSNA inatupa ujumbe kwamba this time cross them, yaani usiwaamini hawa.

mwalimu.jpg

Ridhiwani Kikwete akiwa na mwalimu aliyemsomesha darasa la kwanza 1987 katika Shule yaMsingi Matangini Mwl. Sophia Makong'o, alipomtembelea nyumbani kwake mjini Nachingwea. Kulia ni mtoto wa Mwl. Makong'o, Husna, ambaye alisoma naye Ridhiwani darasa la kwanza katika shule hiyo.

Angalia maisha ya mwalimu aliyemfundisha huyu Kingmaker wetu yalivyo leo. Tulitegemea mwalimu huyo baada ya miaka 23 awe ana maisha mazuri zaidi lakini kumbe leo analilia kitanda cha kamba kisicho na godoro.

Halafu usikute aliwachia shs elfu thelasini ili wabadili mlo wa wki nzima kisha wampigie kura baba yake.
Mungu tunusuru na kizazi hiki cha watawala
 
Kosa ni jinsi huyu mama anavyodanganywa, JK alimwahidi maisha bora miaka 5 iliyopita, leo hii mtoto wake Ridhiwani, anamtembelea tena huyu mwalimu wake akiomba amchangue JK kwa maisha ya kasi mpya.

Mwalimu mwambie, HATUDANGANYIKIII

Ahadi ni za baba yake, Dr. Mkwere na maswahiba zake..the so-called sink tanks of tznian politix, sasa iweje msalaba atwishwe yeye?
 
Kosa la kijana wenu ni kuchekelea maisha duni ya mwalimu wake, alitakiwa angalau awe na sura ya huruma kwenye picha hiyo... lakini kwa vile Rizi na CCM yake hawana huruma na wanainchi basi ni kukenua kwa sana tu, ukiwahoji watakujibu wewe si raia etc

Hata mie leo hii nikikutana na mwalimu wangu wa praimari nikipozi picha lazima niseme 'Cheese', ulitaka anune?

Hakuna hoja hapo.
 
Inaelekea hata hizo stool zimeazimwa kwa jirani kutokana na ugeni huu mkubwa.
 
Kwani hawa jamaa(Riz1 na Ki-wete)huwa wanatabasamu ama kukenua meno???????
 
Back
Top Bottom