Hapo mnajaribu kufananisha au kulinganisha visivyo linganishika, mwalimu alimfundisha kijana akaelekea mjini, mambo safi.
Ninavyoweza tafsiri hii picha ni kuwa watu wengi hukimbilia mijini ili kuwa na maisha bora. Hata hawa viongozi wetu tukiwachagua kama wabunge wote wanahamia DAR na kusahau waliowachagua. Kuna msemo unasema "Usiache mbachao kwa msala upitao". Mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa vijijini yanahitaji watu wenye uzalendo, wanaopenda wote tuendelee, wenye mitazamo ya kusaidia masikini.
Wananchi wameshapewa ahadi nyingi na wanasiasa, lakini hawajui nini ni haki yao na nini sio, walimu walipotaka kugoma kisa mshahara ni mdogo, wengi wetu tuliona kugoma sio suluhisho lakini pengine kugoma kungeweza kumsaidia mwalimu huyu walau akaweza kujikwamua. Hapo inaonyesha kesha kata tamaa ya maisha, anasubiri siku zake alale kwa heri. Huyo binti alitamani kuwa mwalimu lakini hana tena matumaini zaidi ya kufikiria kwenda mjini pengine zali litamwangukia.
Tanzania bila CCM inawezekana, kura yako ni ukombozi wako, piga kura kwa kufuata hoja na si kwa mazoea!