Sababu tano za kufa kwa Bongo movie

Sababu zako zina ukweli kwa kiasi kikubwa lkn hakuna ubabe unaotumika kulazimisha kazi zao zinunuliwe bali wanataka fair ground ya kuuzia kazi zao. Kwa mfano maduka ya kkoo wamefunga wenyewe ili wapaze sauti zao kwa serikali.
Wao wanaproduce chenga then wanataka wapewe fair ground na wakorea au wamarekani? acheni utani nyie.
 
Waigizaji wabadirike maana kutulazimisha sio suluhisho kwa kweli. Sababu nyingine ni hii ya kuendekeza skendo hasa za ngono. Hii inawachafulia sifa zao na kuonekana kama ni wahuni tu. Waache kupamba kurasa za mbele za magazeti ya udaku maana bila skendo hizo naona kwako sijui unapoteza sifa za kuwa mwigizaji!
 
Wao wanaproduce chenga then wanataka wapewe fair ground na wakorea au wamarekani? acheni utani nyie.
Fair ground ya soko ni lazima kwanini wengine walipe kodi wengine wasilipe? Kwa sab wanauza cd za korea zenye ubora na utaalam mkubwa?
 
Umelazimishwa nini?
 
Mpinzani wa wema anapokuwa gigy money mpinzan wa Wolper anapokuwa amber lulu ....mpinzani wa monalisa anapokuwa gea habibu ....U still want to see an industry ?
 
Mi nakubaliana kabisa na no. 3.
Uwezo mdogo wa kiakili.
Sanaa ni tasnia inayohutaji uwezo mkubwa wa kiakili.
Sio movies tu. Sanaa kwa ujumla inahutaji uwe na IQ kubwa. Kwetu bongo imekua vice versa wengi wanaoingia kwenye sanaa ni wale ambao wameshindwa kutoka" darasani/ au kimaisha"
Walau kwenye mziki ndio kuna tofauti wapo baadhi/wengi wanaoonekana wanatoa kaz zenye akili( au ni soko linakua limeshawachuja).

Tunatakiwa tuwekeze kwenye sanaa. Ya filamu. Tuwekeze vipaji , tuwekeze watu wenye akili zao.

Ukiangalia watu wanao igiza Hollywood mastaa wengi IQ zao zina range kuanzia 110 hadi 160. No wonder kazi zao zina creativity na factors zote muhimu kwnye kazi za filamu.

Hizi zetu ukiangali ni chache sana ambazo zina convince.
Na wengine ukiangalia uigizaji wao tu. Inakufanya uwe na wasi wasi na IQ zao
 
Fact mkuu
Uzi huu ni maridhawa kwa wapendwa wasanii ambao wakizingatia watatoka hasa kuweka viwango bora vya kazi bila kujali ushindani. Ningeweza taja baadhi ya kazi zenu mbovu lakini sio utu ila nyingi ya kazi zenu nikiwango cha chini sana. katika hii globalized world huwezi ukajifungia chumbani unaogopa ushindani, lakini kubwa wajipime wao kama usanii ndio kazi zao wasichanganye na siasa kwani watu wote wanahitaji burdani lakini ukiudhi kundi moja unapoteza mteja , so jipangeni kutengeneza pesa bila kuudhi kundi lolote. Kama tatizo ni mtaji jengeni utaratibu wa kuupata, hii ni industry kama nyingine ! I hope sijawaudhi!
 
Mkuu CHARMILTON umesahau jambo kubwa na ambalo ndio linalowaangusha ni Mtaji mkubwa wa kufanya filamu yenye high quality!

Mtu anakwambia movie yake mpaka imekamilika ametumia Milioni 6, Sasa unajiuliza hiyo ni Movie au Shooting ya wimbo.
 
Wangekuwa wanalijua hili wangeshachukua hatua.....tatizo la BM ni pamoja na kutokujua matatizo yao pia.
 
Mkuu CHARMILTON umesahau jambo kubwa na ambalo ndio linalowaangusha ni Mtaji mkubwa wa kufanya filamu yenye high quality!

Mtu anakwambia movie yake mpaka imekamilika ametumia Milioni 6, Sasa unajiuliza hiyo ni Movie au Shooting ya wimbo.
Kusema mtaji ni kisingizio cha kushindwa.Unapokuwa creative unaokoa gharama za uzalishaji.Hollywood kuna film za hadi dola M1 lakini zinatoa faida ya ajabu.
 
Kusema mtaji ni kisingizio cha kushindwa.Unapokuwa creative unaokoa gharama za uzalishaji.Hollywood kuna film za hadi dola M1 lakini zinatoa faida ya ajabu.

Sasa mkuu unafananisha Dola M 1 na Milioni 6?

Nimesema hivyo kwasababu msanii atataka kutumia Camera ambazo low quality za bei rahisi ili tu abajetie pesa ndogo aliyoitenga. Matokeo yake unakuja kukuta movie haina rangi nzuri, scene zina cheza cheza n.k
 
Kumbe ndio maana Shilole na Snura wakakimbilia Muziki. Hawa waliona mbali sana na waliuona mwisho wa Bongo Movie
 
Hata hao wanaowekeza zaidi walianza na mitaji midogo.Kwa umri wa bongo movie walitakiwa wawe mbali lakini bado wanadeka na kulia mitaji kama watoto wadogo.
 
pengo la kanumba je! sio sababu ya ku fail kwa bongo movie?
mjamaa alikuwa anawaamsha wenzake kama wamelala, sasa wakuwaamsha hayupo wote wamerudi usingizini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…