Sababu tano za kufa kwa Bongo movie

Sababu tano za kufa kwa Bongo movie

Bongo movie hawana kipya. Hilo liko wazi. Industry iliuawa na wao wenyewe wasanii. Binafsi siwezi kuangalia kazi za ray au Steve nyerere. Kuwepo kwa kazi nyingi sokoni za nje ni kichaka cha kujifichia. Bali watu wanataka ladha mpya. Na ladha hiyo bongo movie hawawezi kuwapa.
Kweli hawana jipya na wanakasoro nyingi lkn wapo wachache wananunua. Kwanini unatetea wengine walipe kodi wengine wasilipe?
 
Kwa kiasi kikubwa waigizaji wa bongo wanazichukulia kazi zao kama platform ya kutangaza biashara nyingine ambayo wanajua ni illegal...

Pili waigizaji pamoja na watunzi wanaichukulia kazi yao ya sanaa kama ya kufanywa na watu ambao uwezo wao sio mkubwa kitaaluma ndio maana hakuna ubunifu wa maudhui wala muktadha katika kazi zao...kwa kifupi, hawatafuti maarifa zaidi ili kuimarisha sanaa yao zaidi ya kukopi kutoka ghana na nigeria.

Tatu, filamu za kibongo zinakosa upatanifu wa muonekano wa waigizaji na maudhui anayowakilisha muigizaji husika. Unakuta binti kavaa kinguo kifupi mapaja yote nje na mgongo wote wazi, lakini nafasi anayocheza maudhui hayaendani kabisa na muonekano wake.
 
Movie inaanza watu wanakumbatiana na kupelekana gesti wanalala wakitoka wanapanda noah au range rover wanaenda beach wakirud wanakaa kwenye masofa movie inaishia hapo watch out part 2 hivi makonda unamshawishije mtu kununua hizi movie uchwara za kibongo
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Zina kera sana movie za sasa hivi angalau kdg hata slivyokuwepo kanumbaa....hawavai uhalisia hat kdg
 
Wakuu tatizo ni fair ground, hata marekani watu walianza kukosa kazi na viwanda kufungwa baada ya bidhaaa kutoka China kufurika kwenye maduka yao.

Akina trump wamepunguza kiasi cha bidhaa zinazoingia US na wanaongeza kodi zaid na la muhimu wamezindua kampeni ya nunua bidhaa za Marekani na ajiri wamarekan.

Kama taifa kubwa vile linafanya kampeni kubwa kuwasaidia wazalishaji na RAIA wake kwann iwe ajabu kwa bongo. Yaani hii inashangaza sana

Unaweza ukawa unaongea apa kumbe ww ni mbumbumbu wa kutupwa kama akina malinzi tu. Hivi kweli mtanzania halisi anaweza kudhihaki hatua anazochukua Makonda. Hatua anazochukua makonda zinapaswa kuchukuliwa kwenye kila sekta ya uzalishaji

Kuna nchi zimepiga marufuku hata soda za cocacola ili kulinda wazalishaji wa ndani. Yaan kila muigizanji na msambazaji anapaswa kuunga mkono hatua hii kwa nguvu zake zote hata bila kujali wapumbavu wachache wanaopiga domo bila kujielewa.

Akina Steve Nyerere ni akili ndogo tu, wanakataa Ku support kwa sabb ya hofu ya kumuudhi yule demu aliekubuhu kwa upuuzi et kwa sabb aligombana na Makonda. Ni ujinga wake Steve, hatakaa atumie akili yake.

Wakubali ,wakatae Makonda ndo RC wa Dar for now na historia itamtambua hivo. Amewasaidia wengi na kiuhalisia kwa kipindi hiki hakuna mtu anaeweza kuuendesha mkoa wa Dar mpaka ukashika adabu yake kama makonda.

Makondo ndo hero wa Dar, wapuuzi wote lazima wainame. Huyo ndo Mwanaume, kawashikisha adamu watu wote pamoja na utajiri wao. Siku akiondolewa ndo mtaelewa naongea nn.

Watu wamuunge mkono. Huyo ndo mkombozi wenu. Hawa wanasiasa wanawadanganya. Mpeni support Makonda. Achen wanasiasa wafanye siasa zao lakini msidanganywe.

Wakiwa strict baada ya miezi michache mtaona jinsi mauzo yenu yatakavyoanza kupanda.

Hata kwenye sukari walipiga kelele wakajaribu kuhujumu lakin leo hii kila kiwanda kinafanya upanuzi na viwanda vingine vitatu vinajengwa baada ya kupata uhakika wa soko.

Ndivyo maisha yanavyoenda. Kule SA idadi ya watu ni karibia sawa na TZ lakini wazalishaji wao wanauza sana. Ukiangalia bia wanaviwanda zaid ya kumi vikubwa kama Mara tano ya kiwanda cha Tbl apa Dar. Wanaviwanda vya Magari lakini huruhusiwi kuagiza gari kutoka nje. Wafanyakazi wa ngazi Fulani lazim ununue gari na gari likiwa na kilometer idadi fulan huruhusiwi kuendesha, lazima ukanunue lingine. Kwann, ni kwa sabb wanalinda viwanda vyao na ajira za watu wao.

Sasa uku Bongo watu wanataka ajira halafu hawataki kununua bidhaa za kitanzania. Kama sio kulogwa ni nn. Hebu tuamke basi. Mtanzania amka, jitambue. Mama ndalichako nakuomba uongeze ubora wa elimu ili hawa viumbe wajitambue
 
Story zao ni feki sana haziakisi maisha ya kibongo mkuu uzi wako umesimamia kucha director ray mavaz yeye location yeye manager yeye camera yeye kila kitu yeye ray mwenyewe plastic plastic tu wanaover wear kila scene ni kutupia et mama anakunywa chai asubuh haendi kazin unakuta amevaa mahereni makubwa bazee na lipstic ya kufa mtu na viatu kabisa vya mchuchumio siwez kuelezea bongo movie inaniboa balaaa ....
 
Wasanii wa Bongo movie wasubirie 2020 watapata kazi kwenye kampeni za CCM. Kwenye kuigiza hawawezi, hapo mwanzo tuliwabeba tu ili wajiongeze lakini walipopata umaarufu kidogo wakavimba kichwa, na wakageuka wapiga pushup kwenye majukwaa ya CCM na kufanya ufuska huku wakijianika mitandaoni.
 
Bongo movies...Nazichukia kuliko maelezo. Zina maigizo ya kijinga jinga tu. Zimekosa sifa za msingi. Hazielimishi wala hazivutii. Wapenzi wengi wa hizi movie ni wanawake (samahani kwa hilo). Mimi niliacha kuzitazama zaidi ya miaka 10 iliyopita. They are simply nonsense.
 
Siasa imeuwa bongo move wamejichanganya na tamaa zao zao zimewagawa wananchi,
 
Hawa bila kuwaambia ukweli mkuu ipo siku kina man fongo nao wataandamana nao tuache kusikiliza kina kendrick tuwasikilize wao kisa wanalipa kodi
Mfano wako haufanani na hali halisi sab bongo movie hawajagoma kwa sab ya uwepo wa CD za nje Bali uwepo bila kulipa kodi ilhali wao wanalipa. Hata manfongo hawezi kuridhika album yake ilipiwe kodi lakini ya Kriss brown isilipiwe lkn soko ni moja.
 
makaghari,
Uko sahihi kwa asilimia mia moja lkn lazima wapate haki sawa sokoni kwa CD za nje kulipa kodi na tozo zingine kama wao wanavyolipa.
 
CHARMILTON,
yaani Mimi huwa kila nikikumbuka haya masanii yaliyokuwa yakizunguka nchi nzima na lile basi lililopakwa rangi ya kijani na picha ya mzee yule huku wamevaa tisheti za kijani.!
Hata nyumbani kwangu nilishapiga marufuku kuangalia movie na miziki yao.!
Hata familia yangu walishaacha kabisa kama tulivyoacha kuangalia ile televisheni ya Mwanza na ile kuukuu ya Dar.!
Sipangiwi movie wala TV ya kuangalia.
Nishadata kitambo.!
 
Yaani jb namtumbo wote ule kumbe kichwani mabonzo tu,anaandamana amesahau tupo kwenye ubepali aka soko huria
 
Back
Top Bottom