Sababu ya idadi ndogo ya vifo vya COVID-19 Afrika yaelezwa, Tanzania yatajwa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
Idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 Afrika imeendelea kuwa chini huku idadi kubwa ya waathirika wamerudi kwenye hali ya kawaida pamoja na maangalizo mengi ya awali kutoka kwa wanataaluma wabobezi kwamba virusi hivyo vingeubomoa mfumo dhaifu wa afya barani Afrika na kuua watu kwa mamilioni.

Hofu ikazidi kuchagizwa kwamba Virusi vya Corona vinawashambulia zaidi watu wasio na kingamwili madhubuti huku bara la Afrika likiwa na idadi kubwa zaidi duniani la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambavyo hudhoofisha mfumo wa kinga.

Wanasayansi wanajaribu kufumbua fumbo hili la vifo vichache ambavyo havikutarajiwa Afrika ambapo pia waliusahau uzoefu wa afrika kukabiliana majanga kwenye afya ya jamii kama Ebola na virusi vya HIV.

Miezi sita sasa tangu kurekodiwa mgonjwa wa kwanza wa Corona nchini Misri February 14, Afrika imekwepa ubashiri wote madhubuti ikiwa ni bara la pili kwa idadi ndogo zaidi ya watu waliofariki kwa corona baada ya Ocenia ambayo ina idadi ya watu milioni 38 pekee kwenye ulinganifu wa bara la Afrika lenye zaidi ya watu bilioni moja.

Afrika inayobeba asilimia 17 ya watu wote duniani imerokodi vifo 19 kwa kila watu milioni moja ambayo ni takribani mara 34 pungufu ya kiwango cha Amerika ya kaskazini, bara lenye kiwango kikubwa zaidi cha vifo.

Baadhi ya wataalam wana wasiwasi na takwimu zinazotolewa Afrika ikiwa na idadi ndogo ya upimaji na utangazaji dhaifu wa takwimu na vifo vinavyosajiliwa hivyo kuficha ukubwa wa ugonjwa barani Afrika.

Baadhi ya nchi hazipimi umma wake virusi vya corona huku nchi kama Kenya ikiwa imechagua kupima makundi ambayo yako kwenye hatari zaidi ya kupata Corona kama madereva na wahudumu wa afya wakati wengine kama Tanzania wametangaza nchi yao kutokuwa na corona.

Pamoja na upimaji hafifu lakini asilimia ya walioambukizwa ni ndogo sana chini asilimia tano ambayo huwa ni ishara kwamba ugonjwa umezuilika kulingana na WHO.

Kwanini hamna dharura ya afya na namba kubwa ya vifo inayoonekana barani Afrika?
Mshauri wa afya, Dkt. Nicaise Ndembi amesema wakati wanasayansi wanajaribu kufumbua fumbo, ni wazi kwamba kwa sasa Afrika imejiandaa kukabiliana na magonjwa ya umma.

Watu wengi waliopata maambukizi ni vijana ambao hata dalili zinaweza zisionekane. Mathalan nchini Kenya zaidi ya asilimia 82 waliothibitika kupata maambukizi wana umri chini ya miaka 50 ambapo mtu mmoja pekee kati ya 23 ndio amepata dalili za ugonjwa huo.

Mwezi May, WHO ilitabiri kupungua kwa maambukizi ya Corona barani Afrika kulinganisha na mabara mengine ikisema inachangiwa na sababu za kijamii na mazingira pia idadi kubwa ya vijana.

Dkt. Njembi amesema Afrika haijaagana na Corona bado na nini kitatokea kadri nchi zinavyofunguliwa haijajulikana. Amedai picha inaweza kubadilika nchi 25 zilizobaki zikirudi kwenye utaratibu wake.

Maelezo kwa msaada wa ALL Africa
 
Wakati ugonjwa haujafika afrika tulisema ni ugonjwa wa watu weupe tu mara tukawa tunaambiwa watu weusi marekani ndio wanaongoza kwa vifo vya corona,tukasema hao lifestyle na vyakula yao ni tofauti na sie waafrika ndio maana hufa na corona halafu pia wana magonjwa yao mengine. Mara ugonjwa ukaingia afrika hapo tukaanza kuambiwa na sie tulivyokuwa na lishe duni na wengi wana magonjwa bila wao kujua hivyo tutakufa sana tu,ila sasa tunasema corona haina athari sana kwa afrika mara sijui kuna vijana wengi.
 
Yaani wanasayansi wa siku hizi full uchwara dunia mzima. Wakiongozwa na WHO.
Mpaka marekani ikajitoa Ku i sponsor WHO maana hawajielewi. Matangazo meeengi yanabadilika. Walishawahi kusema maski sio muhimu hawa WHO. Mara lazima. Mara Covid sio pandemic. Mara Pandemic.
Full uchwara all over the world.
 
Ukificha maradhi kifo kitakuumbua. Hatujafa. Pimaneni wenyewe na bioimo vyenu vya kichina waliowaletea virusi vya kichiana. Asome Trump
 
Asante boss,Mungu mkubwa ametunusuru,hilo bara Ocenia ni lipi?
Ocenia/Australia moja ya mabara saba na linajumuisha nchi za Australia, New Zealand, kisiwa cha Fiji na nyinginezo. Ni bara lenye idadi ndogo zaidi ya watu duniani ambapo inabeba chini ya asilimia moja ya idadi ya watu wote(Antarctica halina kiumbe hai)
 
Mungu humpa mtu zigo analoliweza...hilo ni zigo la hao wazungu sisi hatuliwezi ndo maana halionekani kutuumiza yani hatujapewa ..
Wakati huu ugonjwa ndio umechachamaa huko ulaya,nikawa najisemea nafsini mwangu kuwa hiki kitu hakiwezi kutokea afrika.
 
Mafua kuanzia lini yakamuua mwafrika....ukimwi na maralia zinatutosha
Waafrika wanakufa kwa mafua, LAKINI ni wazee. Ni kwa vile we do not do research in most of the observed phenomena around us! .....observational research. Vikonge vijijini wanasumbuliwaga sana na mafua inafikia wakati kukiwa ana mtu mwenye mafua wanasema usimsogelee bibi/babu utamuua!
 
Idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 Afrika imeendelea kuwa chini huku idadi kubwa ya waathirika wamerudi kwenye hali ya kawaida pamoja na maangalizo mengi ya awali kutoka kwa wanataaluma wabobezi kwamba virusi hivyo vingeubomoa mfumo dhaifu wa afya barani Afrika na kuua watu kwa mamilioni.

Hofu ikazidi kuchagizwa kwamba Virusi vya Corona vinawashambulia zaidi watu wasio na kingamwili madhubuti huku bara la Afrika likiwa na idadi kubwa zaidi duniani la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambavyo hudhoofisha mfumo wa kinga.

Wanasayansi wanajaribu kufumbua fumbo hili la vifo vichache ambavyo havikutarajiwa Afrika ambapo pia waliusahau uzoefu wa afrika kukabiliana majanga kwenye afya ya jamii kama Ebola na virusi vya HIV.

Miezi sita sasa tangu kurekodiwa mgonjwa wa kwanza wa Corona nchini Misri February 14, Afrika imekwepa ubashiri wote madhubuti ikiwa ni bara la pili kwa idadi ndogo zaidi ya watu waliofariki kwa corona baada ya Ocenia ambayo ina idadi ya watu milioni 38 pekee kwenye ulinganifu wa bara la Afrika lenye zaidi ya watu bilioni moja.

Afrika inayobeba asilimia 17 ya watu wote duniani imerokodi vifo 19 kwa kila watu milioni moja ambayo ni takribani mara 34 pungufu ya kiwango cha Amerika ya kaskazini, bara lenye kiwango kikubwa zaidi cha vifo.

Baadhi ya wataalam wana wasiwasi na takwimu zinazotolewa Afrika ikiwa na idadi ndogo ya upimaji na utangazaji dhaifu wa takwimu na vifo vinavyosajiliwa hivyo kuficha ukubwa wa ugonjwa barani Afrika.

Baadhi ya nchi hazipimi umma wake virusi vya corona huku nchi kama Kenya ikiwa imechagua kupima makundi ambayo yako kwenye hatari zaidi ya kupata Corona kama madereva na wahudumu wa afya wakati wengine kama Tanzania wametangaza nchi yao kutokuwa na corona.

Pamoja na upimaji hafifu lakini asilimia ya walioambukizwa ni ndogo sana chini asilimia tano ambayo huwa ni ishara kwamba ugonjwa umezuilika kulingana na WHO.

Kwanini hamna dharura ya afya na namba kubwa ya vifo inayoonekana barani Afrika?
Mshauri wa afya, Dkt. Nicaise Ndembi amesema wakati wanasayansi wanajaribu kufumbua fumbo, ni wazi kwamba kwa sasa Afrika imejiandaa kukabiliana na magonjwa ya umma.

Watu wengi waliopata maambukizi ni vijana ambao hata dalili zinaweza zisionekane. Mathalan nchini Kenya zaidi ya asilimia 82 waliothibitika kupata maambukizi wana umri chini ya miaka 50 ambapo mtu mmoja pekee kati ya 23 ndio amepata dalili za ugonjwa huo.

Mwezi May, WHO ilitabiri kupungua kwa maambukizi ya Corona barani Afrika kulinganisha na mabara mengine ikisema inachangiwa na sababu za kijamii na mazingira pia idadi kubwa ya vijana.

Dkt. Njembi amesema Afrika haijaagana na Corona bado na nini kitatokea kadri nchi zinavyofunguliwa haijajulikana. Amedai picha inaweza kubadilika nchi 25 zilizobaki zikirudi kwenye utaratibu wake.

Maelezo kwa msaada wa ALL Africa
Wanatilia shaka ufuatiliaji na utoaji wa taarifa?
Waje wajionee! Maana walitoa maunabii yao kwamba maiti za waafrika zitaokotwa njiani sasa wanashangaa!
Mungu wetu ni mkubwa, anatuchunga kuliko wanavyodhani.
 
Back
Top Bottom