baba bora
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 1,500
- 1,093
Vitabu vya apokrifa. Je umewahi Kusikia biblia yenye Vitabu 72? "Huu ni uvumbuzi Mkubwa watu wengi watakasirika"Habari hii inabadili historia ya ukristo wa mapema"maneno Hayo yenye kuchochea fikra yalisemwa na wasomi Fulani Walio furahi kupata maandishi ya "injili ya yuda"yaliyodhaniwa Kwamba yalikuwa ya mepotea kwa zaidi ya karne 16. Vitabu vitakatifu vya watu wa kiyahudi ambavyo havikujumuishwa kwenye katika Biblia ya waebrania . Ufunuo uliotolewa Kupitia Joseph Smith Nabii huko Kirtland Ohio Tarehe 9march1833 Alikuwa anajishughulisha na tafsiri ya agano la kale Akiwa amefika kwenye sehemu ya maandishi ya kale yaitwayo Apokrifa alimuuliza bwana(Mungu) nakupokea Maelezo ya fuatayo "Apokrifa kwa kiasi kikubwa vimetafsiriwa kwa usahihi lakini kina nyongeza na Mabadiliko yasiyo sahihi"M na M 91:1-3 "Apokrifa zaweza kuwafaa wale wenye kuongozwa na roho"M na M 91:4-6(M na M -Mafundisho na Maagano ya Kanisa la Yesu kristo la watakatifu wa siku za mwisho yenye mafunuo yaliyo tolewa kwa nabii Joseph Smith pamoja na nyongeza zilizo tolewa kwa warithi wake katika uraisi wa kanisa) Neno apokrifa linatokana na neno la kigiriki ambalo lina maanisha kuficha. Mwanzoni neno hili lilimaanisha maandishi ambayo yalisomwa na kikundi cha watu Fulani Waliokuwa na Maoni yaliyo patana na ambayo yalifichwa kutoka kwa watu ambao hawakuwa sehemu ya kikundi hicho. Baadaye neno hilo likatumiwa kamaanisha maandishi ambayo hayakuonwa kuwa katika Vitabu vya biblia vinavyo kubalika. Majina ya Vitabu vya apokrifa ni 1Tobiti 2Yudith 3lmakabayo 4IIMakabayo 5Yoshua bin sira 6Hekima ya sulemani 7Baruku UMUHIMU WA BAADHI YA VITABU. Vitabu hivi daima nivya muhimu katika kuunganisha Agano la kale na jipya na vinachukuliwa katika Kanisa kama Vitabu vya manufaa vinasaidia wanazuoni kufahamu mambo yafuatayo nini kilikuwa kinaendelea katika dini na taifa la kiyahudi katika miaka Ile ya Giza Kati ya malaki na mathayo kufahamu Mazingira ya siasa dini na Tamaduni aliyo zaliwa Yesu kujua chanzo cha Ibada za wafu katika Kanisa katoliki na viongozi Walio anzisha SABABU ZA KUKATALIWA. Havi kukubaliwa na waebrania na dini yao hata wakati Mmoja kitabu cha mapokeo ya wayahudi kinasema baada ya malaki roho mtakatfu aliondoka Israeli hii ina maana unabii au uandishi wowote baada ya malaki ulikuwa Hauna uvuvio wa Mungu maneno yaliyomo katika apokrifa haya kutajwa kwenye agano jipya wanafalsa yosefu na filo wataalamu Walio bobea katika historia ya wakati ule walivikataa Vitabu hivi havikuwa na haviko katika orodha yoyote Ile ya maandiko matakatifu kabla ya mwaka 400kk waaandishii wa Vitabu hivi hawakudai Hata Mara moja kuwa Vitabu hivi ni vya Mungu havipatikani katika mAmbo makuu ya theologia Yesu hakuwahi kunukuu katika Vitabu hivi mitume na manabii hawakuwahi kunukuu Vitabu hivi. VILIANZA LINI KUTUMIKA. Vilianza kutumiwa rasmi na Kanisa katoliki mwaka 1546Bk katika kukabiliana na matengenezo yaliyo kuwa ya kifanywa na Martin Luther na wenzake chini ya papa Paul III . Karibuni Wakuu