Sababu ya kumkinai mkeo

StudentTeacher

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2019
Posts
4,153
Reaction score
4,301
Unakuta mkeo ni mrembo na ni mtu mwema sana kwako hadi raia mtaani wanatamani wakupore lakini cha ajabu wewe mwenye Mke mwenyewe umeshamkinai mtoto wa watu kitambo. (Hapa ndipo shetani anapojichukuliaga point 3 muhimu katika mkakati wake wa kuzivamia na kuzivuruga ndoa nyingi).

Sasa basi,kwa kuwa Mimi Student Teacher kwa asili siyo mchoyo wa Maarifa ngoja nikupe sababu ya wewe kumkinai mkeo licha ya urembo na wema wake kwako.

Umemkinai Kwa sababu tangu mwanzo ulimuoa kwa kusukumwa na tamaa za mwili wako tu pasi na Upendo.

Kumbuka tamaa yoyote ile ina kawaida ya kuexpire. Kitu kama hauna unatamani sana kukipata,na ukikikipata pole pole unaanza kukizoea hatimaye kukikinai kabisa. Kinakuwa hakikusisimui tena(Hapa ndipo shetani anapatumia sana kuijaza Jehanamu). Na anaijaza sana tu!

Upendo hauchuji,hauchachi wala kuexpire.

Muwe na siku njema🤝
 
Kutamani nako ni suna lakini
 
Ndugu natambua fika kwamba kuna wake wa hovyo(wanaokinaisha). Zingatia kwamba mada yangu haijajikita kupoteza muda kujadili watu waliamua kupinda. Elewa Neno Mke mwema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…