Sababu ya simba kuwa vile vile misimu yote ni, "comfort zone" inawaponza viongozi na mashabiki

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Simba na viongozi wake mpaka mashabiki wao huwa hawaangalii wala kujali sanaa matokeo bali wao huangalia kama timu imecheza vizuri tu basi inatosha na ndio furaha yao wao hawajali sana kuhusu matokeo.

Simba ilivyotolewa na wydad kwa mikwaju ya penati kule morocco enzi zile wydad ya moto viongozi na mashabiki walikuwa na furaha kuliko wydad wenyewe kisa tu walicheza vizuri mashabiki wakadai timu yao imekufa kiume huku viongozi wakidai hawana cha kumdai kocha na wachezaji wamecheza vizuri kuliko wydad na kwamba wametolewa kwa figisu na bahati haikuwa yao.

Hapa unaona kabisa hawana dira sio viongozi sio mashabiki. Ndio maana warabu wanatuzidi kila mwaka, wao huwa hawaangalii timu imechezaje bali wao huangalia matokeo ndio jambo kubwa kwao.

Simba ikifungwa na Al ahly viongozi na mashabiki watakuambia walikuwa wanacheza na bingwa mtetezi tumecheza vizuri kibu ni moto.

Ukiwauliza mmejifunza nini wao hilo sio jambo kubwa kikubwa wamecheza vizuri licha ya kuondolewa kwenye mashindano.

Mnakumbuka Yanga aliifunga USMA siku ya fainali ila kikanuni USMA walikuwa washindi kwa goli la ugenini wao walishangilia uwanja mzima kwa sababu kombe ni lao bila kuonyesha aibu yoyote.

Yanga hairidhiki na mafanikio iliyoyapata hata azam nao wameamka, yanga imewaamsha azam. Yanga inaimarika kila msimu imefikia hatua sasa inawaza kuwa bingwa wa CAFCL.

Waulize simba wao wana malengo gani ? Sio viongozi sio mashabiki akili zao ni sawa. Mfano jana wqmefungwa wamepoteza taji la ngao ya jamii walilo kuwa wanalitetea hata haiwaumi wao ndio kwanza wanafuraha kuliko yanga wanakwambia jana tumecheza vizuri kocha Fadlu ni kocha mzuri.

Hii simba ni timu ya burudani au ni timu ya makombe? Mimi naona haina dira. Au ni timu maalumu kwaajili ya kutangaza matangazo ya biashara ?

Sio ajabu mkaishia makundi shirikisho, na mashabiki wakamsifia kocha na kumlaumu mangungu wakisahau kuwa mgunda aliwatumia wachezaji wale wale tena wengine hatukuwa tukiwafahamu mfano akina Balua.

Anayejua dira ya simba na malengo yake atuwekee hapa. Maana naiona simba ya miaka kadhaa mbele ikiwa kama kaizer chiefs huku azam ikigeuka mamelod.
 
msemaji wao anasema wanafuraha nimeshangaa!..😅
Unakumbuka ile siku kwenye mashindano ya AFL wanacheza na Al ahly ?

Msemaji wao, viongozi wao na mashabiki walisema hivyo hivyo.
 
msemaji wao anasema wanafuraha nimeshangaa!..😅
Tatizo furaha yenu batiki Fc mmeiwekeza kwa mashabiki wa Simba kuumia ndo maana mnahangaika mara mabango, mara tshirt lina malaama alama ya 5g. Ni kama mnateseka na kutokuumia kwa mashabiki wa Simba kuliko kufurahia mafanikio yenu.
 
Ewe mwanasimba

Mnasemaga timu yenu ni ya Tano kwa ubora huko CAF

Je mnakombe gani la CAF?
 
Hizi si takwimu za makombe CAF. Fuatilia vigezo boss.

Mimi mtu akishauliza swali kama hilo la kuhusu ubora wa vilabu, then anaishia kusema kwani mnakombe gani la CAF huwa nashindwa kuendelea kuzungumza nae kuhusu Soka?

Nimvumilivu katika mazungumzo/majibizano ya kisoka ila hilo swali huwa linanikata nguvu sana.

Naishia kubaki kuwa msikilizaji tu. [emoji1]
 
Mkuu, nakuelewa.
 
Tatizo furaha yenu batiki Fc mmeiwekeza kwa mashabiki wa Simba kuumia ndo maana mnahangaika mara mabango, mara tshirt lina malaama alama ya 5g. Ni kama mnateseka na kutokuumia kwa mashabiki wa Simba kuliko kufurahia mafanikio yenu.
Hawa tumeshajua dawa yao ni tukifungwa tunacheka na kugonga glass za wine, wanabaki kuhuzunika kuliko sisi
 
Simba na viongozi wake mpaka mashabiki wao huwa hawaangalii wala kujali sanaa matokeo bali wao huangalia kama timu imecheza vizuri tu basi inatosha na ndio furaha yao wao hawajali sana kuhusu matokeo...
Simba ni timu ya CCM, Yanga nayo CCM, AZAM ni CUF.
 
Mimi mtu akishauliza swali kama hilo la kuhusu ubora wa vilabu, then anaishia kusema kwani mnakombe gani la CAF huwa nashindwa kuendelea kuzungumza nae kuhusu Soka?

Nimvumilivu katika mazungumzo/majibizano ya kisoka ila hilo swali huwa linanikata nguvu sana.

Naishia kubaki kuwa msikilizaji tu. [emoji1]
Eti wanatupa lecture kuhusu mpira wakati kila siku wanafanya mambo ya hovyo yasiyo na mantiki yoyote. Wanalipia kabisa mabango na kuweka aggr. ya matokeo ya mechi mbili katika ligi ambayo siyo ya mtoano. Unabaki kujiuliza haya mawazo wanatoa wapi hawa viumbe na wanadhani wanachofanya kweli kitatuudhi?
 
Simba na viongozi wake mpaka mashabiki wao huwa hawaangalii wala kujali sanaa matokeo bali wao huangalia kama timu imecheza vizuri tu basi inatosha na ndio furaha yao wao hawajali sana kuhusu matokeo...
Hata ukiwaambia ukweli mtupu huo....HAYAELEWI.
 
Hawa tumeshajua dawa yao ni tukifungwa tunacheka na kugonga glass za wine, wanabaki kuhuzunika kuliko sisi
Tumetoka kuangalia mpira, Unakuta Chura kavimba huku yeye ndo kashinda. Kisa cha kuvimba, mwanasimba kasifia namna Simba ilivyocheza.
 
Simba na viongozi wake mpaka mashabiki wao huwa hawaangalii wala kujali sanaa matokeo bali wao huangalia kama timu imecheza vizuri tu basi inatosha na ndio furaha yao wao hawajali sana kuhusu matokeo.

Simba ilivyotolewa na wydad kwa mikwaju ya penati kule morocco enzi zile wydad ya moto viongozi na mashabiki walikuwa na furaha kuliko wydad wenyewe kisa tu walicheza vizuri mashabiki wakadai timu yao imekufa kiume huku viongozi wakidai hawana cha kumdai kocha na wachezaji wamecheza vizuri kuliko wydad na kwamba wametolewa kwa figisu na bahati haikuwa yao.

Hapa unaona kabisa hawana dira sio viongozi sio mashabiki. Ndio maana warabu wanatuzidi kila mwaka, wao huwa hawaangalii timu imechezaje bali wao huangalia matokeo ndio jambo kubwa kwao.

Simba ikifungwa na Al ahly viongozi na mashabiki watakuambia walikuwa wanacheza na bingwa mtetezi tumecheza vizuri kibu ni moto.
Ukiwauliza mmejifunza nini wao hilo sio jambo kubwa kikubwa wamecheza vizuri licha ya kuondolewa kwenye mashindano.

Mnakumbuka Yanga aliifunga USMA siku ya fainali ila kikanuni USMA walikuwa washindi kwa goli la ugenini wao walishangilia uwanja mzima kwa sababu kombe ni lao bila kuonyesha aibu yoyote.

Yanga hairidhiki na mafanikio iliyoyapata hata azam nao wameamka, yanga imewaamsha azam. Yanga inaimarika kila msimu imefikia hatua sasa inawaza kuwa bingwa wa CAFCL.

Waulize simba wao wana malengo gani ? Sio viongozi sio mashabiki akili zao ni sawa. Mfano jana wqmefungwa wamepoteza taji la ngao ya jamii walilo kuwa wanalitetea hata haiwaumi wao ndio kwanza wanafuraha kuliko yanga wanakwambia jana tumecheza vizuri kocha Fadlu ni kocha mzuri.

Hii simba ni timu ya burudani au ni timu ya makombe? Mimi naona haina dira. Au ni timu maalumu kwaajili ya kutangaza matangazo ya biashara ?

Sio ajabu mkaishia makundi shirikisho, na mashabiki wakamsifia kocha na kumlaumu mangungu wakisahau kuwa mgunda aliwatumia wachezaji wale wale tena wengine hatukuwa tukiwafahamu mfano akina Balua.

Anayejua dira ya simba na malengo yake atuwekee hapa. Maana naiona simba ya miaka kadhaa mbele ikiwa kama kaizer chiefs huku azam ikigeuka mamelod.
GMS, Arafat, Hersi, Ali kamwe n.k... wanamuda wa kutosha kuungana na wachezaji wao na kufurahi pamoja, kuwapa hamasa, kufanya mazoezi pamoja na wachezaji... Hali hiyo inawafanya wachezaji wajiamini na kujiona wanathaminiwa sana na viongozi... Hii hali imefanya hadi mashabiki waione Yanga ni familia, wakicheka wanacheka pamoja, mkilia mnalia pamoja na kufuta machozi kuangalia ya mbele...

Mpira unahitaji usiwe na stress

Upande wa pili sijui kama hali hiyo ipo
 
Kingine, hakuna kitu kinaweza wapa stress wachezaji kama kelele za mashabiki... Kelele zikiwa nyingi mchezaji lazima aingiwe na maradhi ya wasiwasi... Viongozi wa Yanga wamejua kucheza na mashabiki wao, kuwafanya mashabiki wao kuwa mashabiki wa mpira na sio mashabiki wa matokeo... Na ndio maana mashabiki wa Yanga ni wepesi kuridhika

Ukiona kuweka bango, mara supu, mara mchakamchaka ni mambo ya kitoto basi endelea kufikiri hivyo, huku watu wakitengeneza timu yenye base kubwa ya mashabiki wenye furaha na waliokomaa kisoka...
 
Tumetoka kuangalia mpira, Unakuta Chura kavimba huku yeye ndo kashinda. Kisa cha kuvimba, mwanasimba kasifia namna Simba ilivyocheza.
Viumbe wa ajabu sana hawa vyura
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom