Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtu wa Kwanza kuadhibu pale Simba ni Msemaji Ahmed Ally. Huyu ndo anawajaza ujinga mashabiki Mbumbumbu na kuwaaminisha Makubwa wakati timu inafanya madogo. Aliwaaminisha mashabiki Mukwala ni Striker mrefu na Bora Sana, akasema mpira ukija *waaa goli", juzi kaonyeshwa Udhaifu wake Leo timu inaongelea kutafuta Striker mwingine kabla ya August 15. Timu imekosa ubingwa wa Ngao ya Jamii anawaambia mashabiki "wala hatuumii maana hatukuwa na haja na Ngao yenyewe" maana ni ubao.Simba na viongozi wake mpaka mashabiki wao huwa hawaangalii wala kujali sanaa matokeo bali wao huangalia kama timu imecheza vizuri tu basi inatosha na ndio furaha yao wao hawajali sana kuhusu matokeo.
Simba ilivyotolewa na wydad kwa mikwaju ya penati kule morocco enzi zile wydad ya moto viongozi na mashabiki walikuwa na furaha kuliko wydad wenyewe kisa tu walicheza vizuri mashabiki wakadai timu yao imekufa kiume huku viongozi wakidai hawana cha kumdai kocha na wachezaji wamecheza vizuri kuliko wydad na kwamba wametolewa kwa figisu na bahati haikuwa yao.
Hapa unaona kabisa hawana dira sio viongozi sio mashabiki. Ndio maana warabu wanatuzidi kila mwaka, wao huwa hawaangalii timu imechezaje bali wao huangalia matokeo ndio jambo kubwa kwao.
Simba ikifungwa na Al ahly viongozi na mashabiki watakuambia walikuwa wanacheza na bingwa mtetezi tumecheza vizuri kibu ni moto.
Ukiwauliza mmejifunza nini wao hilo sio jambo kubwa kikubwa wamecheza vizuri licha ya kuondolewa kwenye mashindano.
Mnakumbuka Yanga aliifunga USMA siku ya fainali ila kikanuni USMA walikuwa washindi kwa goli la ugenini wao walishangilia uwanja mzima kwa sababu kombe ni lao bila kuonyesha aibu yoyote.
Yanga hairidhiki na mafanikio iliyoyapata hata azam nao wameamka, yanga imewaamsha azam. Yanga inaimarika kila msimu imefikia hatua sasa inawaza kuwa bingwa wa CAFCL.
Waulize simba wao wana malengo gani ? Sio viongozi sio mashabiki akili zao ni sawa. Mfano jana wqmefungwa wamepoteza taji la ngao ya jamii walilo kuwa wanalitetea hata haiwaumi wao ndio kwanza wanafuraha kuliko yanga wanakwambia jana tumecheza vizuri kocha Fadlu ni kocha mzuri.
Hii simba ni timu ya burudani au ni timu ya makombe? Mimi naona haina dira. Au ni timu maalumu kwaajili ya kutangaza matangazo ya biashara ?
Sio ajabu mkaishia makundi shirikisho, na mashabiki wakamsifia kocha na kumlaumu mangungu wakisahau kuwa mgunda aliwatumia wachezaji wale wale tena wengine hatukuwa tukiwafahamu mfano akina Balua.
Anayejua dira ya simba na malengo yake atuwekee hapa. Maana naiona simba ya miaka kadhaa mbele ikiwa kama kaizer chiefs huku azam ikigeuka mamelod.
Wao sasa hivi wanakuambia kapombe na mzamiru ni magarasa, msimu uliopita ilikuwa ni boko saido na baleke.Kingine, hakuna kitu kinaweza wapa stress wachezaji kama kelele za mashabiki... Kelele zikiwa nyingi mchezaji lazima aingiwe na maradhi ya wasiwasi... Viongozi wa Yanga wamejua kucheza na mashabiki wao, kuwafanya mashabiki wao kuwa mashabiki wa mpira na sio mashabiki wa matokeo... Na ndio maana mashabiki wa Yanga ni wepesi kuridhika
Ukiona kuweka bango, mara supu, mara mchakamchaka ni mambo ya kitoto basi endelea kufikiri hivyo, huku watu wakitengeneza timu yenye base kubwa ya mashabiki wenye furaha na waliokomaa kisoka...
Na sisi tunakubali eti tuna raha🤣🤣msemaji wao anasema wanafuraha nimeshangaa!..😅
Kilete leo tena baada ya game
Zingatia hoja na maudhui ya uziBado azam hajageuka mamelodi? Yanga wanawaza ubingwa wa cafcl? Kumbe unaweza kuchukua ubingwa wa cafcl bila kucheza robo wala nusu fainaili wala fainali? Basi hata maniema anaweza kuchukua ubingwa wa cafcl si na yeye anashiriki.