Sababu ya simba kuwa vile vile misimu yote ni, "comfort zone" inawaponza viongozi na mashabiki

Mda utaongea kwa sauti nzuri zaidi kuliko sisi
Ila yanga tuna mtihani mkubwa sana wa kupata 4th trophy Kisha baada ya hapo ndio turudi kwenye mstari wa kukimbilia
 
Mtu wa Kwanza kuadhibu pale Simba ni Msemaji Ahmed Ally. Huyu ndo anawajaza ujinga mashabiki Mbumbumbu na kuwaaminisha Makubwa wakati timu inafanya madogo. Aliwaaminisha mashabiki Mukwala ni Striker mrefu na Bora Sana, akasema mpira ukija *waaa goli", juzi kaonyeshwa Udhaifu wake Leo timu inaongelea kutafuta Striker mwingine kabla ya August 15. Timu imekosa ubingwa wa Ngao ya Jamii anawaambia mashabiki "wala hatuumii maana hatukuwa na haja na Ngao yenyewe" maana ni ubao.
Wa pili wanaoharibu timu ni mashabiki wanaotumika na viongozi kupumbaza wenzao wakiwemo Wachambuzi wanaolipwa kupamba timu Kwa ubora bandia kama Comical Alli wa Iraq wakiongozwa na Goef Lea. Siku viongozi wakiambiwa ukweli mafanikio ya Simba yataanza kuonekana, lakini mkiendelea kuvishana vilemba vya ukoka, ubingwa mtausikia radioni.
 
Wao sasa hivi wanakuambia kapombe na mzamiru ni magarasa, msimu uliopita ilikuwa ni boko saido na baleke.

Unaona kabisa hawa wanashida
 
Uko sahihi mkuu [emoji23].....hawa makolo ni Mbu Mbu mbu
 
Bado azam hajageuka mamelodi? Yanga wanawaza ubingwa wa cafcl? Kumbe unaweza kuchukua ubingwa wa cafcl bila kucheza robo wala nusu fainaili wala fainali? Basi hata maniema anaweza kuchukua ubingwa wa cafcl si na yeye anashiriki.
 
Bado azam hajageuka mamelodi? Yanga wanawaza ubingwa wa cafcl? Kumbe unaweza kuchukua ubingwa wa cafcl bila kucheza robo wala nusu fainaili wala fainali? Basi hata maniema anaweza kuchukua ubingwa wa cafcl si na yeye anashiriki.
Zingatia hoja na maudhui ya uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…