1 Wakorintho 11:6 NENO
Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kukata au kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake.
Ni sababu ya mapambo mengi ambayo mwilini mwao kuanzia kwenye nywele kichwani mpaka kwenye kucha za miguu.
MAPAMBO YOTE HAYO YANAFUNGUA MLANGO WA KUMILIKIWA NA MAPEPO/MAJINI/KUZIMU.
Kwa sababu Mungu hapendezewi nayo na hayatokani na Mungu bali yanatokana na kuzimu/roho ya uasi./mapepo/majini.
Mwanamke wa kikristo ACHA MARA MOJA KUJIPAMBA
Ridhika vile Mungu amekuumba hakukosea.
soma neno la Mungu hapa biblia imekataza mapambo kwa wanawake/wanawake kujipamba ni chukizo kwa Mungu,ni dhambi.
1 Petro 3:3-6
Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.
1 Timotheo 2:9-10
Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu.
1 Wakorintho 11:6 NENO
Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kukata au kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.