Sababu ya wastaafu wengi kuishi maisha magumu baada ya kustaafu

steve_shemej

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,175
Reaction score
1,588
Tumeshuhudia kundi kubwa la wastaafu kuishi maisha magumu baada ya kustaafu hii husababishwa na mambo kadhaa miongoni mwa mambo yafuatayo

Kutojiandaa kustaafu
Wafanyajazi wengi huwa hawajiandai kustaafu na wamekuwa wakiishi maisha kama watakuwa waajiriwa maisha yao yote hali inayopelekea kutojijengea misingi ya namna ya kuishi baada ya kustaafu..

Kuegemea mshahara pekee
Hii ni sababu nyingine wafanyakazi wengi hutegemea mshahara wake pekee katika kuendesha maisha anakuwa hana kitegauchumi kingine kitakachompatia pesa baada ya kustaafu

Mshahara milioni, matumizi milioni
Hii hutokea wafanyakazi wengi hutumia mshahara wake wote anaoupata kiasi chakutokuwa na akiba hali inayopelekea kuwa na control ndogo ya pesa mfano anafanyakazi kwa mwez anatumia milioni akistaafu na kszini haendi inamaana matumizi yatazidi milioni moja baada ya muda kupoteza pesa zote za kiinua mgongo

Kufungua biashara baada ya kustaafu
Mtu hajawahi kuwa na biashara hajui changamoto za biashara akistaafu ndiyo anafungua biashara tena baada ya kushauliwa biashara ya kufanya na unavyojua kila biashara inalipa ukisimuliwa kwakuwa hana uzoefu anajikuta anashindwa kuendesha biashara mwisho anapoteza pesa

Hivyo basi mwajiliwa ukianza biashara ukiwa kazini kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa baada ya kustaafu maana kuruka sarakasi hawajifunzi ukubwani.

fd2c64929fad5ba9c84a9d8dbdc2ae89.jpg
 
Mtu akipata tu ajira hana hata kiwanja cha kuanzia , anakimbilia kuzaa watoto basi hapo gharama za maisha zinakuwa kubwa ....Better watu watulie angalie uwe na startup ya kiwanja .

Ukishakuwa na watoto lazima akili iende mbio ndio chanzo cha kukimbilia mikopo , mtu mpaka anastaafua ana mkopo .
 
Nyie nae Kila muda wastafu..wastafu ,Hela ni za kwo, kuonga wanaonga wao ,kufa wanakufa wao ,pensheni ni yao ..nyie kinawauma nini ? .Pangeni budget/plann zenu waacheni wazee wetu watumie hela zao hamjawasaidia kizitafuta ndani ya miaka 30.

Kila mtu atumie hela zake anavyopenda yeye ,hata zikiisha yeye ndio anapata depression na anakufa yeye ,hili swala la kila mtu kuwa msahuri wa wastafuu ni Umama.
 
Badala useme awe na kitega uchumi kwanza unasema kiwanja. Kiwanja kitajijenga chenyewe na kuongeza maokoto..?
 
Nyie nae Kila muda wastafu..wastafu ,Hela ni za kwo, kuonga wanaonga wao ,kufa wanakufa wao ,pensheni ni yao ..nyie kinawauma nini ? .Pangeni budget/plann zenu waacheni wazee wetu watumie hela zao hamjawasaidia kizitafuta ndani ya miaka 30.

Kila mtu atumie hela zake anavyopenda yeye ,hata zikiisha yeye ndio anapata depression na anakufa yeye ,hili swala la kila mtu kuwa msahuri wa wastafuu ni Umama.
Waambie wanapangia watu na hela zao. Ubaya sio wote wastaafu wanateseka.
 
Ni umama wa kiwango cha juu ,mtu ameanza kuteseka enzi za Mwinyi mshara sh 17,630/= Leo hii toto ka elfu mbili kanakuja kushauri babake jinsi ya kutumia hela zake, pumbavu .

Vijana tafuteni hela zenu acheni kiherehere na pensheni ya wazee .
Sure. Wanafanana na hii serikali yetu inayo wapangia wastaafu matumizi. Watu wapewe chao wajifie mbele. Kwani wataishi miaka 100+..?
 
Mtu akipata tu ajira hana hata kiwanja cha kuanzia , anakimbilia kuzaa watoto basi hapo gharama za maisha zinakuwa kubwa ....Better watu watulie angalie uwe na startup ya kiwanja .

Ukishakuwa na watoto lazima akili iende mbio ndio chanzo cha kukimbilia mikopo , mtu mpaka anastaafua ana mkopo .
Sasa nyie wasipokopa banks zitaendeshwaje ,maisha tunategemeana ,banks wanategemea watumishi ili waendeshe taasisi vile vile watumishi wanategemea bank kwa mkopo
 
Naona mizee mipumbavu mijuaji isiyoambilika tiyari imevamia uzi. Nakumbuka mzee mmoja alivyostaafu akaoa binti mdogo, akanunua bodaboda na canter. Akienda kilabuni anatukana watu makusudi wakimkaripia haombi msamaha anawanunulia pombe kwa kejeli "wape pombe hawa maskini nitalipa mimi nina hela chafu" na walevi kwa kuwa kipaumbele ni pombe wanashangilia. Akawa chifu mdogo.

Hakukaa hata miaka miwili miradi ilikufa, akaachwa na mke, akaishiwa hela na akafariki kwa stress. Kilichobaki angalau ni nyumba aliyojenga.

Msimamo wake ulikuwa kama huu wa watoto wadogo mtaniambia nini tafuta hela zenu.
 
Sure. Wanafanana na hii serikali yetu inayo wapangia wastaafu matumizi. Watu wapewe chao wajifie mbele. Kwani wataishi miaka 100+..?
Kichwa Cha mleta thread ndio wanakubali ujinga wa kipewa wastafuu hela kiduchu hela zao tena wanapangiwa jinsi ya kitumia wakati kifo nje nje ..mfano mzuri General Mbunge kastafu 2023 na kafa jana ..angepewa hela yake zote familia si wangefaidika..TUACHANE NA GEN MBUGE YEYE ALIKUWA KWENYE HIGH TABLE CAKE AMEACHA VITEGA UCHUMI VINGI ,FIKIRIA MWALIMU WA MAKONDE NDANI NDANI HUKO ALIYESTAFU KAMA MBUGE 2023 ALAFU KAFA JANA PENSHENI IMEMSAIDIA NINI FAMILIA YAKE
 
Mtu akipata tu ajira hana hata kiwanja cha kuanzia , anakimbilia kuzaa watoto basi hapo gharama za maisha zinakuwa kubwa ....Better watu watulie angalie uwe na startup ya kiwanja .

Ukishakuwa na watoto lazima akili iende mbio ndio chanzo cha kukimbilia mikopo , mtu mpaka anastaafua ana mkopo .
Kweli kabisa mkuu.tujiandae kidgo kabla ya kuwa na watoto.
 
Kichwa Cha mleta thread ndio wanakubali ujinga wa kipewa wastafuu hela kiduchu hela zao tena wanapangiwa jinsi ya kitumia wakati kifo nje nje ..mfano mzuri General Mbunge kastafu 2023 na kafa jana ..angepewa hela yake zote familia si wangefaidika..TUACHANE NA GEN MBUGE YEYE ALIKUWA KWENYE HIGH TABLE CAKE AMEACHA VITEGA UCHUMI VINGI ,FIKIRIA MWALIMU WA MAKONDE NDANI NDANI HUKO ALIYESTAFU KAMA MBUGE 2023 ALAFU KAFA JANA PENSHENI IMEMSAIDIA NINI FAMILIA YAKE
Jeshi hawana kikokoteo mkuu.
 
Naona mizee mipumbavu mijuaji isiyoambilika tiyari imevamia uzi. Nakumbuka mzee mmoja alivyostaafu akaoa binti mdogo, akanunua bodaboda na canter. Akienda kilabuni anatukana watu makusudi wakimkaripia haombi msamaha anawanunulia pombe kwa kejeli "wape pombe hawa maskini nitalipa mimi nina hela chafu" na walevi kwa kuwa kipaumbele ni pombe wanashangilia. Akawa chifu mdogo.

Hakukaa hata miaka miwili miradi ilikufa, akaachwa na mke, akaishiwa hela na akafariki kwa stress. Kilichobaki angalau ni nyumba aliyojenga.

Msimamo wake ulikuwa kama huu wa watoto wadogo mtaniambia nini tafuta hela zenu.
We endelea Kutoa somo dogo,tunalielewa Wazee!
 
Banki na mfumo wa riba ndio chanzo za umaskini duniani kote.
Umelazimishwa kukopa ? ,unajaziwa form ?,makato ya riba huoni ? ,umekopa kwa raha zako,umakula Kwa raha zako then unasema ni chanzo cha umaskini..huo ni uzezeta.
Naona mizee mipumbavu mijuaji isiyoambilika tiyari imevamia uzi. Nakumbuka mzee mmoja alivyostaafu akaoa binti mdogo, akanunua bodaboda na canter. Akienda kilabuni anatukana watu makusudi wakimkaripia haombi msamaha anawanunulia pombe kwa kejeli "wape pombe hawa maskini nitalipa mimi nina hela chafu" na walevi kwa kuwa kipaumbele ni pombe wanashangilia. Akawa chifu mdogo.

Hakukaa hata miaka miwili miradi ilikufa, akaachwa na mke, akaishiwa hela na akafariki kwa stress. Kilichobaki angalau ni nyumba aliyojenga.

Msimamo wake ulikuwa kama huu wa watoto wadogo mtaniambia nini tafuta hela zenu.
Alitumia hela zake ,alichezea hela zake,haukumsaidia kuzitafuta ,Kila mtu atakufa,

Alichezea hela zake ..haukumsaidia kuzitafuta..ni pensheni yake...kinachokuuma ni nini kama sio kiherehere..Hakuna atakaye ishi milele alikufa kama

Hela ni zake,alichezea hela zake,akaoa binti mdogo Kwa hela zake, akalewesha watu Kwa Hela zake ..Wewe kinachokuuma ni nini ? .kufa kupo na haikwepeki ulitaka ufe kwa ajili yake?
 
Umelazimishwa kukopa ? ,unajaziwa form ?,makato ya riba huoni ? ,umekopa kwa raha zako,umakula Kwa raha zako then unasema ni chanzo cha umaskini..huo ni uzezeta.

Alitumia hela zake ,alichezea hela zake,haukumsaidia kuzitafuta ,Kila mtu atakufa,

Alichezea hela zake ..haukumsaidia kuzitafuta..ni pensheni yake...kinachokuuma ni nini kama sio kiherehere..Hakuna atakaye ishi milele alikufa kama

Hela ni zake,alichezea hela zake,akaoa binti mdogo Kwa hela zake, akalewesha watu Kwa Hela zake ..Wewe kinachokuuma ni nini ? .kufa kupo na haikwepeki ulitaka ufe kwa ajili yake?
Nakuambia wanajipa mizigo ya familia mpaka wanakopa.
 
Kama unalipwa mil 2 au 1 na Una familia ya watoto 2-3

Kutunza hela inahitaji uwe na nidhamu ya hali ya juu Sana

Points ambayo naona ni muhimu ni kuwa na side hustles

Kuna jamaa ni Mwalimu Ila anavua samaki Ana mtumbwi , ni mpishi wa maharusi ni dereva ana Alphadrd ya kupeleka maharusi Pia

MTU Kama huyu mwisho wa mwaka kwenda Zanzibar na familia yake ni jambo la kawaida.
 
Jeshi hawana kikokoteo mkuu.
Kumbe...kwa hiyo kikokoto haiwahusu ? kwani Polisi wanakwama wapi..au kwa kuwa tunawapatia ya kiwi barabarani Wana compersert .

Kama hawana kikokoto hao ndio wanaume sio hawa watumishi hawaeleweki na viongozi wao wanataka nini ? Wakishawaona wanasiasa wanajipendekeza hata kujitetea inawashinda wanarudi huku kulia lia kama mitoto
 
Back
Top Bottom