Sababu za CCM kutoanguka tangu Uhuru hadi sasa

Sababu za CCM kutoanguka tangu Uhuru hadi sasa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
CCM ni chama cha ukombozi, na vyama vingi vilivyopigania Uhuru wa nchi zao havipo tena madarakani lakini CCM bado ipo tu.
Yafuatayo ni baadhi ya michango iliyosababisha CCM iendelee kubaki madarakani:

1. Haina ubaguzi mkubwa wa wananchi wake: Baada ya uchaguzi kwisha Hakuna tofauti kimaisha kati ya walioichagua CCM na wasioipenda CCM, wote wanakufa njaa au wote wanashiba. Hakuna maduka, usafiri, mbolea wala masoko ya wanaCCM na wapinzani.

2. Kuruhusu uholela kwa wananchi: CCM na serikali wake inaruhusu watu wajifanyie mambo yao bila bughuza hata bila kufuata utaratibu, kanuni na sheria. Imeruhusu watu kulima, kufuga, kuvua, kuchimba, kuwinda, kujenga, kuua, kununua, kulipa, kuuza na kununua na kuendesha magari kiholela. Waliiweka serikali na sheria mbali na shughuli za wananchi wake, hivyo watu hawaipati harufu ya uwepo wa serikali na sheria kwenye maisha yao, hivyo hawaoni ubaya wa CCM na uzuri wa vyama vya upinzani. Siku CCM itakapoanza kuwaambia watu wafuate utaratibu na sheria kwenye mambo yao yote itaondoka madarakani siku hiyohiyo.

3. Kushirikisha wanajeshi kwenye serikali na Chama:
Huu ni mtaji mwingine wa CCM kuwafanya wanajeshi wawe sehemu ya maamuzi ya serikali kwao.

4. Udhaifu wa vyama vya upinzani: Viongozi wa vyama vya upinzani ni waganga njaa, hivyo uongozi ni sehemu ya ajira yao. Ndiyo maana unawaona viongozi na wabunge wa upinzani wana majumba, mashamba, makampuni, mahoteli, wanasomesha watoto wao shule bora kabisa badala ya kutumia nguvu za kiuchumi zao kujenga vyama vyao. Hii ndio inayowafanya wasione tabu hata kuhamia vyama vingine wakati wowote kufuata maslahi makubwa zaidi. Wanawatumia wananchi wanaowapigia na kulinda kura zao kama mitaji yao tu.

5. Umasikini wa wananchi:
Maskini hana uchaguzi, akipewa uholela wa kuiba na kuuza hata vyuma vya madaraja, kofia na fulana inawatosha kabisa (Present is known!)

6. Tume ya uchaguzi: Tume ya uchaguzi inayoundwa na mwanaCCM mwenyewe ni vigumu kuidondosha.

Hivyo mtaji mkubwa wa CCM ni kuruhusu uholela kwa wananchi, kutobagua Watanzania, kushirikisha wanajeshi, udhaifu wa vyama vya upinzani, umaskini wa kipato, chakula na elimu wa watu na tume isiyo huru

Siku CCM ikiachana na mitaji hii 6 inaweza kuondoka chaliii
 
5. Umasini wa wananchi: Masikini hana uchaguzi, akipewa uholela wa kuiba na kuuza hata vyuma vya madaraja, kofia na fulana inawatosha kabisa (Present is known!)

6. TUme ya uchaguzi: Tume ya uchaguzi inayoundwa na mwanaCCM mwenyewe ni vigumu kuidondosha.
 
Kwani unailinganisha serikali ya CCM na serikali gani nyingine iliyowahi kuwepo Tanzania? unaposema haina ubaguzi mkubwa kwa wananchi, ni serikali gani imewahi kuwa na ubaguza kwa wananchi Tanzania?
 
5. Umasini wa wananchi: Maskini hana uchaguzi, akipewa uholela wa kuiba na kuuza hata vyuma vya madaraja, kofia na fulana inawatosha kabisa (Present is known!!!).

6. TUme ya uchaguzi: Tume ya uchaguzi inayoundwa na mwanaCCM mwenyewe ni vigumu kuidondosha.
chama kilicho imara na misingi sabiti huwezi kilinganisha na vyama chumia tumbo wanaoibiana wenyewe kwa wenyewe halafu wanashangilia ccm ni chama imara
 
Katibu Mkuu wa Chama alishasema chama kinategemea dola kubaki madarakani.
bora hata huyu anaongea hivi wa chadema mara ya mwisho kuongea ni lini? nakumbuka tangu alivyoambiwa na halima mdee kaingia chadema na ndala hana hamu tena ya kuongea
 
CCM ilishaanguka miaka mingi ila policcm ndio waliong'ang'ania madaraka. Siku wananchi wakifufuka utaona
 
Japo haisemwi sana lakini CCM inejibalance sana kidini. CUF kilikuwa na nguvu lakini kilionekana kama cha waislamu. CDM kilikuwa na nguvu lakini kilionekana cha wakristo. ACT kinaonekana kama cha waislamu. Lakini ukikiangali CCM ni ngumu kukipa sura ya kidini. Wapinzani wakiweza hapo watatoboa.
 
Unataka ianguke Vipi chama kina mbunge moja Tanzania mzima wewe kwako ni ushindi akili za Bavicha bana.
 
Japo haisemwi sana lakini CCM inejibalance sana kidini. CUF kilikuwa na nguvu lakini kilionekana kama cha waislamu. CDM kilikuwa na nguvu lakini kilionekana cha wakristo. ACT kinaonekana kama cha waislamu. Lakini ukikiangali CCM ni ngumu kukipa sura ya kidini. Wapinzani wakiweza hapo watatoboa.
Uongo
 
Kwani unailinganisha serikali ya CCM na serikali gani nyingine iliyowahi kuwepo Tanzania? unaposema haina ubaguzi mkubwa kwa wananchi, ni serikali gani imewahi kuwa na ubaguza kwa wananchi Tanzania?
Ubaguzi ninaouzungumzia ni ubaguzi kwenye kutoa huduma kwa wananchi, shule, zahanati, polisi, magereza, mahakama na umachinga haiangalii wewe ni CCM au ni chama gani, wote sawa tu.
 
kwani kuna nchi inaongozwa na serikali mbili?
Sheria ya kwanza ukilinganisha lazima pawepo na vitu viwili, naona mleta kalinganisha penye kitu kimoja pekee.
 
CCM ilishajenga msingi imara uliojengwa na Muasisi wake Nyerere na hivi vyama vya upinzani ni mapandikizi ya CCM kila chama kinachozaliwa CCM inapeleka mtu wake pale tena inahakikisha anafika katika ngazi za juu za uongozi katika hicho chama mwisho wa siku anakiharibu na kuanza upya ona NCCR Mageuzi (Mrema), CUF (Lipumba), CDM (Zitto) na ACT (Marehemu Anna). Kwahiyo tutasubiri sana CCM kuanguka
 
Katibu Mkuu wa Chama alishasema chama kinategemea dola kubaki madarakani.
hiyo ndiyo shida ya akili ndogokutafsiri kaneno kamoja yaani ndiyo imekuwa kama wimbo sasa kuna chama kinaweza kushinda bila dola?
 
CCM ilishajenga msingi imara uliojengwa na Muasisi wake Nyerere na hivi vyama vya upinzani ni mapandikizi ya CCM kila chama kinachozaliwa CCM inapeleka mtu wake pale tena inahakikisha anafika katika ngazi za juu za uongozi katika hicho chama mwisho wa siku anakiharibu na kuanza upya ona NCCR Mageuzi (Mrema), CUF (Lipumba), CDM (Zitto) na ACT (Marehemu Anna). Kwahiyo tutasubiri sana CCM kuanguka
hilo hawalijui watabaki kusubiri sana
 
Tatizo lipo kwa raia, wengi wamekosa elimu hasa ya uraia.
 
Back
Top Bottom