Sababu za CCM kutoanguka tangu Uhuru hadi sasa

Sababu za CCM kutoanguka tangu Uhuru hadi sasa

Hata huko kuiba kura (kama kupo) ni jambo la muda tu, iko siku wananchi hawatakubali hata kura yao moja iibiwe na yeyote. Sasa hivi hawajali wizi wa kura kwakuwa bado kuna uholela katika maisha yao, uwepo wa ardhi ya wazi ya kupumulia na vyama vya upinzani kuwa dhaifu sana na vya kiganga njaa zaidi . Siku uholela ukiisha, ardhi ya wazi hakuna na vyama vya upinzani kuwa stronger hawatakubali kura yao iibiwe hata moja.

Kwanini yatumiwe majeshi , Polisi Na usalama Na tume ya CCM Si waweke tume huru Na wasitumie vyombo vya dola tuone Kama kweli CCM inapendwa Na wananchi
 
Imagine, Mabalozi wa nyumba kumi hawalipwi
mshahara lakini wako tayari kupambana kuhakikisha CCM inashinda😀
wakati wa kampeni na uchaguzi hawa watu wana kazi muhimu sana, hawatoki hivihivi. Orodha ya watakaokwenda kupiga kura na kuhakikisha wanakwenda kupiga kura wanayo wao. Hivyo T-shirts, kofia, khanga na posho zote za kampeni zinapitia kwao.
 
w
Ruzuku ya CCM ni zaidi ya 4B per month inafanya kitu gani?
wao wana serikali hawahitaji kutumia hela yao ya ruzuku. Wanatumia ruzuku kuisimamia serikali yao na kulipa mishahara na poho kwa viongozi wa chama nchi nzima na mikutano yao
 
w

wao wana serikali hawahitaji kutumia hela yao ya ruzuku. Wanatumia ruzuku kuisimamia serikali yao na kulipa mishahara na poho kwa viongozi wa chama nchi nzima na mikutano yao
Mpikie sham ale chakula mambo ya wanaume achana nayo dada angu
 
Sababu kuu CCM kutoanguka ni utekelezaji wa chukua, weka waa........
 
CCM ni chama cha ukombozi, na vyama vingi vilivyopigania Uhuru wa nchi zao havipo tena madarakani lakini CCM bado ipo tu.
Yafuatayo ni baadhi ya michango iliyosababisha CCM iendelee kubaki madarakani:

1. Haina ubaguzi mkubwa wa wananchi wake: Baada ya uchaguzi kwisha Hakuna tofauti kimaisha kati ya walioichagua CCM na wasioipenda CCM, wote wanakufa njaa au wote wanashiba. Hakuna maduka, usafiri, mbolea wala masoko ya wanaCCM na wapinzani.

2. Kuruhusu uholela kwa wananchi: CCM na serikali wake inaruhusu watu wajifanyie mambo yao bila bughuza hata bila kufuata utaratibu, kanuni na sheria. Imeruhusu watu kulima, kufuga, kuvua, kuchimba, kuwinda, kujenga, kuua, kununua, kulipa, kuuza na kununua na kuendesha magari kiholela. Waliiweka serikali na sheria mbali na shughuli za wananchi wake, hivyo watu hawaipati harufu ya uwepo wa serikali na sheria kwenye maisha yao, hivyo hawaoni ubaya wa CCM na uzuri wa vyama vya upinzani. Siku CCM itakapoanza kuwaambia watu wafuate utaratibu na sheria kwenye mambo yao yote itaondoka madarakani siku hiyohiyo.

3. Kushirikisha wanajeshi kwenye serikali na Chama:
Huu ni mtaji mwingine wa CCM kuwafanya wanajeshi wawe sehemu ya maamuzi ya serikali kwao.

4. Udhaifu wa vyama vya upinzani: Viongozi wa vyama vya upinzani ni waganga njaa, hivyo uongozi ni sehemu ya ajira yao. Ndiyo maana unawaona viongozi na wabunge wa upinzani wana majumba, mashamba, makampuni, mahoteli, wanasomesha watoto wao shule bora kabisa badala ya kutumia nguvu za kiuchumi zao kujenga vyama vyao. Hii ndio inayowafanya wasione tabu hata kuhamia vyama vingine wakati wowote kufuata maslahi makubwa zaidi. Wanawatumia wananchi wanaowapigia na kulinda kura zao kama mitaji yao tu.

5. Umasikini wa wananchi:
Maskini hana uchaguzi, akipewa uholela wa kuiba na kuuza hata vyuma vya madaraja, kofia na fulana inawatosha kabisa (Present is known!)

6. Tume ya uchaguzi: Tume ya uchaguzi inayoundwa na mwanaCCM mwenyewe ni vigumu kuidondosha.

Hivyo mtaji mkubwa wa CCM ni kuruhusu uholela kwa wananchi, kutobagua Watanzania, kushirikisha wanajeshi, udhaifu wa vyama vya upinzani, umaskini wa kipato, chakula na elimu wa watu na tume isiyo huru

Siku CCM ikiachana na mitaji hii 6 inaweza kuondoka chaliii

7-Mzimu wa Nyamrunda aka Mwenge!
 
Back
Top Bottom