Sababu za CCM kutoanguka tangu Uhuru hadi sasa

Kianguke Mara ngapi ndio ujue?Chama ambacho kinakimbia uchaguzi na kuwategemea akina Kingai Mahita na Goodluck ndio Chama hai?
 
Kianguke Mara ngapi ndio ujue?Chama ambacho kinakimbia uchaguzi na kuwategemea akina Kingai Mahita na Goodluck ndio Chama hai?
 
Kwasababu ina mizizi ilio jichimbia kwa chini sanaaaaa
 
Heading yako ilitosha usubiri ujibiwe. Na jibu ni ili wizi wa kura, unyang'anyi wa ushindi, tume ambayo si huru, na unfear!
 
Nijuavyo technolojia itawaondoa tu, hata kama ni miaka 50 ijayo, itafika mahala tutapiga kura kwa kutumia simu zetu na kila kura inapododoka unaona idadi ya kura zilivyopigwa, kuiba kutakuwa hakuna nafasi, pili wajinga bado ni wengi na maisha bado ni rahisi mno nafikiri unaona walioko mjini ndio uleta kashikashi ila walioko vijijin wengi wanajua Nyerere bado yupo ikulu
 
Mtaji wa CCM ni wananchi masikini na wajinga, ndiyo sababu wanazalishwa kila siku…. usiku utapokwisha.!
 
Umaskini wa watanzania wengi ni mtaji mzuri sana kwa CCM hasa nyakati za uchaguzi
 
Imewekeza UJINGA na UPUMBAVU kwa raia wake, kwa namna hiyo hakuna raia atakayeenda kinyume na matakwa ya CCM. Leo 2022 bado tunatumia katiba ya 1977, miaka 45 iliyopita, katiba ya chama kimoja inatumika na vyama vingi na sisi wananchi tumekaa tu.

CCM ni walafi na waroho wa madaraka hivyo wataendelea kupanda mbegu ya UJINGA na UPUMBAVU miongoni mwa wananchi ili waendelee kuitafuna nchi.
 
Unapigana na anaye kupa silaha ,anakulisha anakupa fedha,Utamuweza kweli?

Ova
 
Unataka ianguke Vipi chama kina mbunge moja Tanzania mzima wewe kwako ni ushindi akili za Bavicha bana.
baada ya kuwaengua wagombea wote wa upinzani, au...?
 
Mtei mwenyewe yuko kwenye system. Huwezi kuwa Gavana wa bank kuu bila kuwa mtu wa serikali kwelikweli.
 
Waache kutumia Polisi waache kutumia DED na watengeneze mfumo rafiki wa uchaguzi uone tukio.
 
Kwa jinsi watanzania wenyewe walivyo na hivyo vyama mbadala vilivyo ni bora ccm iendelee kutawala.
 
WaTanganyika wengi hawajui siasa, na pili hawana sababu ya kuiondoa CCM madarakani.
Kila Mtanganyika wa kawaida utakapomuuliza kuhusu kuiondoa CCM jibu atakwambia Maisha ni Haya haya hata wakija wapinzani hakuna jipya.
 
kama wananchi ni wajinga kiasi hicho, wewe utafanye kuwaelimisha, au ni ule msemo wa ukiwashindwa ungana nao?
 
Siku ukifanikiwa kufika nchi zilizoendelea utajua umuhimu wa elimu.

Mfumo wa elimu wa kitanzania unakumbatiwa na CCM miaka kenda unamjenga mtu kuwa tegemezi wa serikali na asiyejua haki zake za msingi.

Mfano uliwahi kuona wananchi wa Marekani wanamsubiri kiongozi aje kuzindua kisima cha maji?

Kwa Tanzania wengi hawajui haki zao na hisani pia hawajui kipi ni chao kipi si chao,rais ametengenezewa mazingira ya kuonekana mungu mtu.

Polisi na wenzao wote wako chini ya CCM.

Kwa namna gani hapo CCM itatokaje madarakani.
 
WaTanganyika wengi hawajui siasa, na pili hawana sababu ya kuiondoa CCM madarakani.
Kila Mtanganyika wa kawaida utakapomuuliza kuhusu kuiondoa CCM jibu atakwambia Maisha ni Haya haya hata wakija wapinzani hakuna jipya.
Hayo ni matokeo ya kuachiwa kufanyakazi zao kiholela biba buguza na uwepo wa ardhi kubwa ya wazi. Siku ardhi ya wazi ikiisha na serikali kuwataka watu (machinga, wakulima, wafugaji, wavuvi, bodaboda na wachimba madini) wafuate taratibu zote zilizopo na za kisheria utaona timbwilitimbwili lake.
 
Sababu kubwa ni chama dola. Coercive instruments ndio wasindikizaji katika safari yao ya utawala. Si tembo wala simba watakatisha na kuzuia huo msafara... Iko mizinga ya kubomoa miamba, maburdoza ya kuchonga njia, a.k 47 za kusafisha njia, vipaaza sauti vya kutoa onyo yaani full masnondo.
But people's power kitakuwa kisambaratisho na kimechomoza na kinakua...
 
Shida ya vyama vya upinzani ni moja tu, viongozi na wananchi wamejitenga kama maji na mafuta. Hii ni kutokana na viongozi wao kuonekana kama wanaweza kurudi CCM wakati wowote kama vile Lowassa, Slaa, Sumaye, na wengine weeengi walioenda kuunga juhudi viongozi wa ccm. Viongozi na wabunge wa upinzani wanajilimbikizia mali wao wenyewe. Hii ndio maana hata viongozi wakikamatwa na kuwekwa ndani hakuna mwananchi wa kawaida anaejali, maana hawagusi maisha yao ya kila siku kwa lolote kwa chochote. Luzuku haijawahi kuchimba hata kisima kimoja cha maji cha mfano kwenye kijiji/mtaa mmoja, wanakula tu na kumtunzia Mtei na familia yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…