Sababu za Diamond Platnumz kutumia itel A37 hizi hapa

Sababu za Diamond Platnumz kutumia itel A37 hizi hapa

Weka na bei niangalie uwezekano Wa kuachana na haka Katecno kangu..

Maana kamezidi kuniumbua, juzi Niko namtongoza demu kenyewe mfukoni kameshajitoa lock, kamesachi namba na kameshampigia Mama Mkwe bila Mimi kujua.
Duh?,mie nusra katume picha x kwenye family group
 
Takribani wiki mbili baada ya itel kumtangaza balozi wake ambaye ni Diamond platnumz, sasa imebainishwa sababu za Diamond platnumz kuipenda simu hiyo ambayo ni tolea jipya la itel A37 ambayo imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa sababu zilizoelezwa na Diamond kuhusu itel A37 ni pamoja na ubora na ukubwa wa skrini ya A37 ambayo ina 5.7” HD+ Waterdrop ikiwa ni full skrini. Kabla ya uzinduzi huo Diamond aliwaambia wafanyabiashara ambao ni wadau wa “itel A37 ni lazima niwe nayo kila siku ina skirini kubwa inatoa mwonekano bomba wa chochote ninachokitazama kwenye skrini ndio sababu naipenda sana na kizuri zaidi simu hii ina face unlock” amenukuliwa Diamond.


Kwa ufafanuzi zaidi face unlock ni mbadala wa fingerprint na hufanya kazi kwa ufanisi na ni salama na rahisi, ili kufungua itel A37 mtumiaji atatakiwa kutazama kwenye skrini ya A37 na simu itajifungua yenyewe.

View attachment 1751731

Mbali na hilo itel A37 imeundwa kwa namna ambayo kama mtumiaji anataka kujipiga picha maarufu sefie na asingependa kubofya kwa kidole basi anaweza kutabasamu tu mbele ya kamera ya itel A37 na hapo atakuwa tayari ameshajipiga picha.

Kikubwa zaidi itel A37 imedizainiwa ikiwa na ukanda maalum mzuri wa kuvutia (ribbon), hii inakumweka mtumiaji kwenye ulimwengu wa fasheni mahali popote anapokuwepo.

Zaidi ya hayo, simu ya itel A37 imewekewa ulinzi wa macho kwa mtumiaji, hii inajulikana kama eye care ambapo mtumiaji atatumia simu hiyo kusoma vitabu ama kutazama chochote kwa mwanga laini usio na mionzi inayoumiza macho.

Simu hii iliyozinduliwa ina rangi tatu ambazo ni, Dark Blue, Light Purple, Gradient Green.

View attachment 1751733

Taarifa zaidi tafadhali tembelea ukurasa wa instagram wa itel tanzania au bofya link hii: Login • Instagram
Itel ni simu au kibebea laini??
 
Yaani hata atumie Trump sina mzuka kabisa la itel ilishawahi tumia simu hizi za itel zikanitesa sana unampigia mtu unaongea unakuta imezima tu bila sabababu
 
Watu mnaponda wengine kutumia tecno, wakati mnajua hali halisi ya watanzania au wengine uchumi wenu mzuri? , mimi natumia cammon 11,mwaka wa tatu iko poa tu au mnataka nitumie kitochi nokia kwa kuwa siwezi kununua simu gharama
 
Watu mnaponda wengine kutumia tecno, wakati mnajua hali halisi ya watanzania au wengine uchumi wenu mzuri? , mimi natumia cammon 11,mwaka wa tatu iko poa tu au mnataka nitumie kitochi nokia kwa kuwa siwezi kununua simu gharama

Ah wala hata ni watu wamechka kutembea na simu inapata moto kama jiko la umeme
 
Back
Top Bottom