Sababu za Jenerali Ulimwengu kuzinguana na Mkapa hadi kunyang'anywa uraia

Ulevi wa madaraka ulianza muda lakini walau miaka hiyo viongozi walikua na aibu. Ulimwengu kupishana na Rais mitazamo na mawazo na akawa na uwezo wa kumface kumuambia hapa umekosea hapa sio sawa , ukarejea miaka hii ambayo ata ukipishana mawazo na Dc, Rc, waziri tu maisha yako yatakua ya taabu hapo hujamchallenge Rais, pm huko ukigusa ndo kabisa litabaki jina lako tu.
Yes hawakua perfect pia lakin compared to nyakati za leo, tumerudi nyuma maili nyingi sana ki uhuru wa kusema, uhuru wa maoni, na kidemokrasia.
 
Sijawahi kusikia huyu mzee anamponda Kikwete...

Shida yake ni Mkapa na Magufuli...

Was Jakaya a good president to him?
Sidhani kama aliwahi kuponda mtawala yeyote binafsi, makala zake zilijikita kwenye kukosoa utendaji na uendeshaji wa mambo kwenye awamu zote,hujawahi kusoma makala zake hata kwenye gazeti la Raia Mwema enzi za awamu ya 4 ya JK?...
 
Hizi mambo za kuondoleana uraia zipo sana Afrika. Marehemu Chiluba wa Zambia alimwondolea uraia hayati Kenneth Kaunda wa Zambia kwa kudai ni raia wa Malawi. Imagine baba wa taifa anaambiwa sio raia.
 
Sasa si umeona bado yupo

Maana yake uvumilivu bado upo

Siku ukimasta nguvu ya mamlaka utamjengea sanamu hata Samia
 
Kuna kitu kilitokea baina ya ulimwengu na benja , ambacho ulimwengu hawezi abadani kutamka hadharani
Umeongea ukweli mtupu.
Ukisoma habari ina mashimo mengi.
Habari hii ina ukweli na mengine yamefichwa, ni kwakuwa Mkapa hayupo tena kujitetea, hivyo tunalazimishwa tuamini kile alichosema bila kusikia upande wa pili.
 
Jenerali Ulimwengu aliamsha sana wananchi kujua nchi inaenda vipi kupitia makala zake na pia za waandishi wake. Nakumbuka Rai ilikuwa na makala nzito za kizalendo. .Waandishi wake akina Mbwambo,kulikuwa na mzee mseminari mmoja alipenda kulinganisha dola mbali mbali duniani kama Rumi na taifa la Marekani pia alikuwemo jasusi aliyeikimbia nchi anaishi Uskochi evarist Chahali. Nitatafuta majina yote niyaandike humu. Alikuwa tishio kubwa sana la mafisadi hadi TISS wakafanya njama kuu ya kumfilisi na kuiua kampuni,Salva Rweyemamu aliyekuja kuwa mwandishi wa Rais ikulu akaja kulinunua kampuni la Habari Corporation pale Sinza akalichukua Rostam Aziz ikaitwa New Habari Corporation. Jenerali akaanzisha Raia Mwema na kufungua kampuni mpya pale UFI huku akishindwa kufanya biashara ya habari vema. Mzee Jenerali alikuwa na magazeti kama Dimba na Habari Corporation ilikuwa imesheheni ila akawa ameshadondoka maana nguvu zake za ujana zilibebwa na jamaa walioamua kumfilisi. Jenerali alikuwa na kipindi kizuri sana cha TV Channel Ten cha Jenerali On Monday na wengine wazee wenye vipindi makini kama Hamza Kasongo hour.

Kuna makala aliandika kuhusu nchi ya Tanzania kuwa lidude lisilokuwa hata kutambaa halitambai,wala kutembea,wala kukimbia hii pia ilimletea shida kwa Ben. Simlaumu kumkosoa Freemason Ben aliyekuwa na degree zote 33 maana alikuwa haatack mtu binafsi ila uongozi mbaya alikuwa anashirikiana na timu yake kuandika na kukosoa . Akaja Saed Kubenea akawa kama yeye ila wakammwagia Tindikali maTISS wakitumwa na Waziri mkuu kipindi kile Edward Lowassa na mafisadi wengine kama hayati Mwendazake kumnunulia hawara yake nyumba ya serikali. Ufisadi mwingi tuliujua kupitia Rai,Raia mwema na Mwanahalisi na JF hadi JF mafisadi wameamua waifungie kabisa. Jenerali Ulimwengu kijana wa TANU ni mzalendo hasa aliandika kitabu chenye Rai zake na aliendelea kuandikia East African kwa kiingereza very humorous and like a Kenyan or a Ugandan. Wa viwango vyake labda Kabendera Eric lakini kwa sasa waandishi nguli wachache au hakuna KAMA MSTAAFU HUYU.POKEA MAUA YAKO MENGI SANA MZEE WETU JENERALI TWAHA ISSA ULIMWENGU.23
 
Sidhani kama aliwahi kuponda mtawala yeyote binafsi, makala zake zilijikita kwenye kukosoa utendaji na uendeshaji wa mambo kwenye awamu zote,hujawahi kusoma makala zake hata kwenye gazeti la Raia Mwema enzi za awamu ya 4 ya JK?...
Sijawahi kusoma mkuu...

Unaweza kutuwekea hapa, tujisomee!

Maana kuna wakati nahisi(nasisitiza "nahisi") huyu mzee ni mwana mtandao.
 
Hiyo ni baada ya kuona madaraka yao yanazidi kuwa hatarini kadiri muda unavyokwenda
 
Hilo swali hawez uliza ,hapo ni ww ujiongeze kuliuliza akilin mwako na ulijibu mwenyew
 

*Mimi nilimfanyia kampeni nikiamini atatekeleza yale tuliyotangaza, lakini ninavyoona sivyo unavyofanya"
Hawa walikua marafiki,japo stori ni ya upande mmoja lakini yaonekana kampeni meneja alikaraishwa sana na mambo kuendeshwa kinyume na ahadi alizozinadi mbele za wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…