Sababu za kiroho kwanini uvae msalaba ?

Usijisifie ujinga mkuu utakuja kuumbuka mchana kweupe!
 
ndani kama ya mwaka hivi nilipata kuzaliwa upya ki fikra na kufikia hitimisho kuwa dini ni utapeli tu
Ulikimbia mvua, ukajitosa baharini. Ukatoliki ni utumwa kuliko utumwa wenyewe.

Sasa hukutakiwa kuiacha imani, bali usome Biblia ili ikuongoze vizuri kutoka kwenye mapokeo ya wanadamu hadi kwenye mafundisho safi ya Yesu Kristu.

Hauna tofauti na mtu anayechukia parachichi tunda mazima maishani mwake, kisa tu mara ya kwanza alipolionja lilikuwa bado bichi au limeoza - bila kujua kwamba yapo maparachichi matamu kama asali.

Ulifanya kosa kubwa kumtupa jongoo na mti wake.
 
Bila dini au fundisho la uwepo wa Mungu, hakuna kitu kinachoitwa maadili. Hiyo ndiyo hoja kubwa mojawapo inayowachocha sana atheists.

Maadili hutoka kwa Mungu tu. Kama unaamini katika maadili, basi kitaufu (by default) wewe unaamini uwepo wa Mungu - hata kama ungejificha kwenye kauli za kuukanusha ukweli.
 
Ni suala la muda tu kila mtu atachanganyikiwa kwa wakati wake
 
Kuna misalaba aina gapi?
 
Common Sense! Ibilisi anatumia hiyo kuliko wewe, mfano ni pale bustani ya Eden. Kama unaamini kuwa uko vitani hapa duniani, silaha ni muhimu. Hujui unapotembea njiani, barabarani au uko kwenye chombo cha usafiri au uko nyumbani unapishana na viumbe wanaoonekana na wasioonekana. Wako wafuasi wa Ibilisi wanaoonekana na wasioonekana ambao huogopa hizi silaha za kiroho tunazovaa na huchukia sana wanapotuona nazo. Hutafuta kila njia ya kutusahaulisha tuziache ili malengo yao yatimie. 'Common Sense' siyo kinga, imani ndiyo kinga yenye nguvu. Kama unaamini Rosari inakupa kinga, hiyo imani yako ndiyo inayokuponya!
 
Hizo stori za eden huwa naona ni porojo tu, hao viumbe wasio onekana ndio wapi? Wamewahi kufanya kipi cha maana kwenye ulimwengu huu??
 
Sasa kwa nini kuiba sio sahihi ila kudinyana ni sahihi?
Kuiba si ni kuchukua kitu/mali bila idhini ya mmiliki? Suala ambalo hata kwenye kanuni za msingi za jamii yoyote ile iliyo staarabika ni kosa, una compare vipi na suala la kudinyana kitu ambacho watu wawili wamekubaliana kwa akili zao timamu wafanye jambo fulani kwenye miili yao huko faragha?
 
Msalaba ni alama ya kipagani ,hakuna andiko linaagiza uvae msalaba

Acheni ujinga na ushirikina

Degree ya 18 ya Freemason,Ni kitengo maalumu kinashughulika na kuingiza makanisani na madhehebu yote alama mbalimbali za misalaba ,na wamefanikiwa kwa 100% Hadi sasa
 
How do u survive bila kuamini kwenye dini? Unaamini kwenye nini au ni full pagani sahivi unatafuta tu pesaa?
Hizi dini watu wamekuwa brainwashed Hadi kufikia kuamini na kuogopa vitu vya kufikirika, it's just a hoax. Ni uongo, uzushi na utapeli mtupu.
 
Hizo stori za eden huwa naona ni porojo tu, hao viumbe wasio onekana ndio wapi? Wamewahi kufanya kipi cha maana kwenye ulimwengu huu??
Ni suala la kuamini tu! Kama Mungu, malaika, mashetani au pepo wachafu na majini wapo lakini hawaonekani basi hata ndondocha au misukule inawezekana kabisa wasionekane. Unatofautishaje porojo na uhalisia? Nini kigezo porojo?
 
Ni suala la kuamini tu! Kama Mungu, malaika, mashetani au pepo wachafu na majini wapo lakini hawaonekani basi hata ndondocha au misukule inawezekana kabisa wasionekane. Unatofautishaje porojo na uhalisia? Nini kigezo porojo?
Wanakuwaje wapo halafu hawaonekani?? mfano labda umepanda bus alafu jirani yako kwenye seat akakuambia unajua hapa nimekaa juu ya boda boda, wewe ukitizama huoni hiyo boda boda unaona seat ya kawaida, hapo huwezi ukaona huyo jirani yako labda anaweza kuwa na dalili za ukichaa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…