Enzi hizo nikiwa Kijana wa Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria Unga ltd ulikuwa huniambii kitu kuhusu Rozari, ilifika hatua hata nikiisahau mahali Rozari yangu lazima niifuate, wakati wa kulala lazima nisali Rozari kwenye Novena ama nisikilize radio maria ndio nilale, ila siku moja nikajiita mkutano na kujiuliza hivi kwaa akili za kawaida tu ni kwanini nakuwa kama mganga yani Rozari imekuwa kama ni kitu nachokiabudu!!!??
Nikaanza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu dini ya ukristo pamoja na Imani ya Kanisa katoliki, nikkanza kuutafuta ukweli kwa kufuatilia mienendo ya mapadri na viongozi wengine wa dini, nikaanza kuipa nafasi Common Sense ifanye kazi kichwani, ndani kama ya mwaka hivi nilipata kuzaliwa upya ki fikra na kufikia hitimisho kuwa dini ni utapeli tu.
Nikaachana na hayo mambo ya Rozari na mambo ya dini kabisa, nikarudi kuishi kwenye misingi ya kawaida ya binaadamu aliye staarabika.
Ni zaidi ya miaka 15 sasa imepita ila sijutii maamuzi yangu.
NB: maneno yangu sio sheria