Sababu za kufungwa Taifa stars 0 burundi 1

Mimi nasikitika tu wameharibu pitch yetu ya sambusa na biriani. Wasifanye tena campaign zao kwenye uwanja wa Mkapa kwani madhara tumeyaona jinsi pitch ilivyoharibika. Na ukuzingatia viwanja vizuri hapa nchini ni vichache. Kuharibu siku moja, kurudi katika hali yake ya awali labda wiki mbili.
Leo sitaki kumuongelea Samata.
 
Taifa stars ilicheza vizuri ila kuna mapungufu Fulani madogo madogo...ila Mkude naye red yake imeiathiri timu...otherwise....fowadi na viungo marekebisho yanahitajika... Huyu Mkude amedekezwa...angekuwa Jana ndiyo anaichezea Simba kwenye ligi zile kadi mbili za njano asingepata...
 
Ningekua mimi ndiye Kocha wa Timu ya Taifa, nisingekuja kumuita mchezaji asiye na nidhamu kama Jonaa Mkude.
Mwamuzi amewaamulia, badi hakuridhika! Huku ana kadi ya njano tayari!! Ana mchango wake mkubwa tu kwa timu kupoteza kwenye ile mechi.

Ingawa huwezi kuwaacha CCM kwa kuuharibu uwanja baada ya kufanya ule upuuzi wao kuchezea kodi zetu kinyemela.

Na pia mwalimu wa timu kwa kushindwa kuwa anzisha mapema wachezaji wapambanaji uwanjani kwa sasa kama Mzamiru Yasin. Badala yake anawaanzisha wachezaji wanao sugua benchi kwenye timu zao kama Said Ndemla na Idd Seleman.

Bila shaka alipenda tufungwe na timu yake ya Taifa. Maana baada ya mechi kuisha, nilimuona alivyotingwa kwenda kuwapongeza ndugu zake akiwa na furaha tele.

Yaani Taifa kubwa kama Tanzania, eti kocha wa timu yake ya Taifa ni raia kutoka ka nchi kadogo kama Burundi!! Bila shaka kuna mahali tumekosea.
 
Uko sahihi kwa sehemu kubwa...ila Hilo la CCM na uwanja hapana...CCM hawakupewa bure uwanja ule...walilipia na hata uharibifu wake Bila Shaka...halafu mkuu wa nchi anafanya kampeni wewe ni meneja wa uwanja utakataa? Hilo la Ndemla na Iddi Selemani hata Mimi ningewachezesha Kama kuwajaribu..ni lazima tuwe na kikosi kipana Cha national team..ile ni mechi ya kirafiki..kocha alikuwa anapima wachezaji...Hilo la nidhamu ni kubwa Sana kwa wachezaji wetu..huyo Mkude anamkaba mtu Koo..yaani mchezaji mhuni kabisa yule..halafu Samatta ni mtu wa kulishwa mipira Sasa Kama huna watoa pass wazuri hawezi kufunga..Kwanza Samatta huwa hakabi ..yeye ni goal getter ...ila marefa wetu nao kwenye ligi za kwetu wanawaathiri wachezaji kiuwezo...kwa mfano Kuna mchezaji wa Burundi alianguka kwenye penalti na hakutoa penalti...fikiria Kama angekuwa ni Kagere kadondoka vile kwenye ligi..
 
Uwanja umetiwa najisi hata wangefanyaje wasingeshinda. Mechi ijayo wakachezee Chato watashinda
 
Hivi kabisa mnategemea maajabu yeyote kuhusu stars?
Mpira na siasa wapi na wapi? Ndo mana hata Simba na Yanga zinahama kuziweka timu mwenye mfumo was Kampuni kukwepa siasa siasa ndani ya timu.

Wabunge wakijisikia tu wanazialika timu zao pendwa bungeni na si Azam (This is rubbish)

Rais wa TFF kada wa Chama....anapenda siasa na Chama kuliko mpira.
Mechi ya Simba na Yanga imesogezwa kisa watu wawe busy na kampeni...huu ndo ukweli.

Waziri mwakyembe anataka kupunguza wachezaji wakigeni ili wazawa wapate nafasi(Siasa tupu hapa)
Chama pendwa kimeenda kufanya Kampeni kwenye kiwanja cha taifa kinyume na utaratibu....humsikii Mwakyembe wala nani akileta blah blah!(Wote Kimya)...kuna umuhimu gani wa kufungia viwanja vibaya halafu unaenda kuharibu vizuri vichache vilivyobaki.

Binafsi sishabikii Stars wala siizomei...naiona tu kama Motema pembe ya Kongo.
 
Mbona hiyo inafahamika toka zamani kuwa hakuna kitu ambacho Tanzania tuko serious. Ukocha tunajifunza kwa mdomo na uchezaji kwa mdomo ndiyo sababu tunaishia kubondwa. Wahenga walisema mdomo ulikiponza kichwa!
 
CCM hawajalipa hata senti moja kutumia uwanja! Magufuli alitumia madaraka yake vibaya kuamuru kampeni zake zifanyike kwenye uwanja huo.
 
Mimi siwashabikii wakifungwa nakua shabiki wa Taifa wakishinda tu
 
CCM hawajalipa hata senti moja kutumia uwanja! Magufuli alitumia madaraka yake vibaya kuamuru kampeni zake zifanyike kwenye uwanja huo.
How do you know ??.CCM sio wajinga kiasi hicho...usilete uzushi wako kwa watu wanaoelewa...anayeandaa kampeni siyo Magufuli..ni CCM...huwezi kutumia uwanja ule bila kulipia...acheni uzushi bwana...ninachoweza kukubaliana na wewe ni kimoja tu kwamba hivi kilikuwa na umuhimu na ulazima kufanyia kampeni mule? Hilo la kulipia hapana...CCM lazima walipe...na nadhani wamelipa siyo chini ya milioni tano au wamepelekewa bill...

Nyie watu sijui vipi Kila lawama Magufuli, Magufuli, Magufuli...yaani hata ukilala unaota Magufuli tu...amewafanya Nini?! In JPM we have the best President..na uchaguzi huu atashinda...anaweza akapita hata za JK za 2005...
 
Strikers ni tatizo, Mbwana hana jipya - Msuva apewe jahazi kuiongoza Stars MPYA yenye sura za vijana wenye vipaji.
 
Samatta uwezo mdogo, kocha raia wa burundi, ccm wameharibu pitch kwa kucheza kigodoro juzi
safari ya samata kisoka ndiyo inaondoka hiyo!! hana jipya la kumfanya awe tofauti na hawa vijana wetu wanaocheza hapa.

Kuhusu CCM kuharibu uwanja kwa kigodoro cha bure hilo lipo wazi
 
Acha kumwaga povu hapa! Magufuli ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wapi afanye kampeni zake. Pili hakuna fedha yo yote iliyolipwa na CCM hapa wizarani.
 
Yaani hapo mwisho ndio umeongea bonge la point....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…